MAJINA: Watanzania tudumishe mila

WAZO2010

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
1,610
3,738
Wadau katika uchunguzi wangu mdogo nime gundua huenda Tanzania likaja kuwa Taifa namba moja Ulimwenguni kumiliki malimbukeni wa tamaduni za kigeni. Kila kitu, tuna dai kimepitwa na wakati, mara ni imani za kichawi, kishirikina, mizimu , nk.

Binafsi, nimechukua kipengele kidogo tu cha Majina (NAMING). Zamani Babu na Bibi zetu wali muita mtoto wa kiume au Kike jina kutokana na:
1. Mavuno
2. Nyakati...asubuhi/mchana/ usiku
3. Mtawala (mfalme)- Mkama au Omukama.
4. Mazingira ya sehemu aliko zaliwa. Mfano nje ya nyumba, nk.
Mfano: Wamasai- Nolari-wakati wa Mavuno, Nanyori-Upendo, Nasiku- Asubuhi.

Mjaluo- Otieno-kiume-Usiku/Atieno-Ke- usiku,
Opiyo- Haraka, Akinyi-Asubuhi,
Mjita/Mruri/Mkwaya- Malima- Wakati wa Kilimo, Masatu-me-/Nyasatu-ke - nyakati za sato kupatikana sana, Nyangeta-ke-Usiku, Nyanyama-ke- hapa kulikuwa na nyama, nk.
Wa kurya: Marwa, Mwita, Maswi, Ghati, Wankyo,
Wasukuma: Mabula, Masanja, nk

Nigeria: Obasanjo, Okonkwo, Amefuna, Abeo, nk.
Kenya: Chepkirui, Chebukati, Gachagua, Odinga, Kirui, Maina, nk.
Uganda: Mirembe, Ochen, Mukasa, Namazzi, Kizza, nk.

Tanzania zamani tulipata.majina mazuri ya upekee ya kutambulisha wewe au ukoo wako. Mfano: Nyerere, Kikwete, Magufuli, Kingunge, Makamba, Membe, Ngofilo, Mgogo, Mwijaku, Mwandosya, Mwaipaya, Lissu, Mbowe, Zitto, Mbatia, Mrema, Makinda, Migiro, Tibaijuka, Ole-Sendeka, nk.
Hii ili rahihisha kumbukumbu ya matukio, kutambulika kirahisi, na utambulisho wa U Taifa wako, hata ku enzi Ndugu zako. Jina liki tajwa hata ajalini, tiyari ndg wana anza kuulizana kama ni ndg yao au vp. Kenya mwezi ulio pita Mortuary ya Taifa ilikuwa na maiti zaidi ya 200 ime koswa ndugu kisa hawajulikani! Majina kama Angel, Ephraim, nk.

Vijana wa rika letu miaka 1980s to 2022 watoto wetu wana Naming mpya: Joseph, Anne, Miriam, Joyce, Angel, Gilbert, Peter, Alexander, Brian, nk.

Wachungaji, Ma padre, Ma pastor, ma nesi na Madaktari, wame kuwa waongo na waoga kusimamia ukweli. Aki kuta hata Mkanda mweusi ki unoni au mkononi mwa mtoto eti ana ita hiri, akati yeye ili msaidia hadi kakua hivyo ikizuia magonjwa, nk. Wazungu wana tumia Dini, Lugha, na Globalization, kuteka Dunia. Angalia Nchi kama Japan, N. Korea, Brazil, China, Singapore, Madagascar, Nigeria, Somalia,Russia, nk bado wana tamaduni zao.

Je Tanzania tuna tatizo gani? Ebu tuache Ujinga wa kueneza tamaduni za kizungu na kuzika utamaduni wa Ki Africa, hasa wa Kitanzania tuki jidai eti ni kustarabika. Tubadilike, huu siyo Ujanja ni Ujinga!
 
Tatizo letu utumwa wa kiakili. Watumwa pekee ndiyo hulazimika kupewa majina ya mabwana zao wanaowamiliki wa kiarabu au kizungu.
 
Tembea kwa miguu hadi Dodomq,kutokea mkoa mwingine. Achana na mabasi/ndege za wakoloni.
 
Back
Top Bottom