Ndugu zangu Wakurya, Naomba mnieleweshe kuhusu zile ndoa zenu za Mwanamke kumuoa mwanamke.

mtoto mdogo sana

JF-Expert Member
Apr 16, 2020
460
1,337
Habarini ndugu zangu.
Aidha nitoe angalizo kuwa nia yangu sio kukosoa tamaduni za kabila hili. Ila topic ya ndoa ya aina hii kidogo inanipa tabu kidogo kuelewa.
Nimeona jambo hili linafanyika sana kwa jamii karibu zote za kikurya na category zake (Maana hawa wenzetu kidogo wamejigawanya katika sub-categories za kikabila. Kwa mfano kwa wenyeji wa wilaya ya Serengeti Kuna Waisenye, Wanatta, Wangurimi, wakurya wenyewe, wairamba n.k. japokuwa mimi binafsi naona wote ni wakurya tu. Mniwie radhi kwa kuwa sijakusudia insult.

Sasa kwa category zote hizo kuna aina hii ya ndoa ambayo mwanamke anaweza kuamua kwenda kutafuta binti, akamtolea posa, akamleta kwaake kisha akawa anampa huduma zote za kimaslahi kisha here and there, mwanamke anapata mimba anazaa watoto.

Sasa watoto hao yule mwanamke ambaye sasa ndio tuseme 'mume' ndio ana jukumu la kuwatunza na kuwapa huduma wale watoto n.k

sasa jambo nisiloelewa ndugu zangu. Si wale watoto wwanakuwa na baba zao kabisa Biological? huwa haileyi shida huko mbele ya baba ku claim damu yake? au pengine, si inaweza kuleta changamoto ya heshima kwa muoaji kwa kuwa 'mume' kazi yake ni kuhudumia, kisha wataalamu usiku wanakuja kuvizia kitonga cha ut3lezi?

Au ndugu zangu huwa kuna utaratibu wa 'mume' kumchagulia mke wanaume gani azae nao?

Nimetazama hii namna hasa kwenye jamii zinazoishi kaskazini mashariki mwa serengeti hasa hasa maeneo yaa kuzunguka mto Mara sijaelewa.

naombeni wazawa wa huku mnipe ufafanuuzi.

Maana pia huwa nakutana na watu wana middle name za majina ya kike kama Matinde, Bhoke, Ghati nk, japokuwa mengine nimeambiwa yanatumika kote.

ila naombeni kidogo muongozo.
 
MAJIBU NI HAYA HAPA.

Kwanza hakuna sehem wala ukweli wowote kuwa mwanamke anaowa mwanamke mwezie katika kabila la kikurya wakurya ni moja ya tamaduni za watu ambao Ant-Homosexual kwa hiyo msiwe na dhana hiyo kwamba mwanamke anauoa mwanamke mweziwe.

Ila sasa mwanamke anaetambulika kama muoaji kwa makabila yenu sisi kwetu anatambulika kama mama mkwe ambae Mme ni hewa. Ila kijamii anakuwepo na anajulikana isipokuwa kwenu waswahili ndio mnaamini hamna mwanaume.

Nitaelezea kiurefu kidogo na sababu ya kwanini hiyo inatokea,

KWANZA, katika kabila la wakurya ni watu wanaamini katika urithi sana,

PILI, Kabila la wakurya ni watu wanaoamini katika muendelezo wa kizazi,

TATU, Katika kabila la kikurya Mwanamke halitishwi na wanaamini mwanamke hawezi kuendeleza kizazi cha familia aliyozakiwa kwa kuwa mwanamke anaolewa na kwenda kuendeleza kizazi katika familia alioolewa na sio kwao.

KUNA AINA MBILI ZA NDOA ZA AINA HIYO ZOTE ZIKIWA NA LENGO MOJA ILA ZINATOFAUTIANA KIMAZINGIRA NA KWA MAJINA,

NYUMBA MBOKE, hii nyumba mbokeh inatokea kama kijana mkubwa katika familia ambae tayari alikuwa amepitia hatua za kiutu uzima kwa maana ya jando, kwa sababu wakurya kwao jando haifanyiki kama usafi tu bali inafanyika kama hatua ya kumvusha kijana katika utoto na kuingia katika utu uzima, ndio maana wakurya tukio hilo hulifanya kama kipimo cha ujasiri kwa kijana na kama kipimo cha mtu ambae ataweza kukabiliana na changamoto za utu uzima na familia, tukio la SUNA hufanyika bila Ganzi na moja ya sheria inatakiwa mhusika anaefanyiwa asijitikise wala kupepesa jicho asimame wima hadi zoez litakapomalizika, tuachane na hili la suna.

Hivyo inapotokea kijana amepitia hatua ya utu uzima kwa maana ya sunna hapo anatakiwa kuowa na kuendeleza kizazi chake, sasa ikitokea kijana huyu akapitiwa akafariki au akapata tatzo lolote la kiafya ambalo hawez tena kuowa,

Hapo ni jukumu familia yake kwa maana ya wanafamilia yake kukaa chini na kutafta mke anaolewa kuja katika familia hiyo kwa lengo la kuendeleza kizazi cha marehem ndugu yao, hii wanaitumia kama moja ya njia za kum'enzi marehemu lakini pia kuendeleza kizaz chake na kuamini kuwa bado wapo nae,

Suala hapa ni yupi anaepaswa kuchukua jukum la kulea huyu mwanamke ambae anaolewa kwa niaba ya marehem, Hapa kinakaa kikao cha familia kisha anachaguliwa mmoja amabae atachukua jukum la kuowa huyo mwanamke na kisha atamhudumia yeye na atazaa nae ila watoto watakaozaliwa sio wake tena bali wataitiwa jina la marehem baba yao ambae hakuwazaa,

Ubaya wake ukiteuliwa na ukakataa huwa familia inakuacha ila mke utakaemuowa wewe mtaendelea kuishi nae ila kuna siku utaambiwa haujaowa kwa kuwa mke ulienae ni mke wa marehem ndugu yako, maana mara nyingi pia anaechaguliwa kufanya hivyo anakuwaga mdogo wa marehem, na kijamii ya wakurya mdogo hatakiwi kuowa kabla ya kaka yake hivyo utaambiwa uliowa kabla ya kaka yako na mke wako sasa atakuwa mke wa marehem, na hata ukikataa haitasaidia kwa kuwa jamii itaamini wewe bado haujaoa, na hauna watoto, kwa hiyo kwa kunusuru hilo inakubidi uowe mwanake mwingine ili unusuru ulienae katika ndoa na abaki kuwa mkeo anaetambulika kijamii, na ukigoma ujue siku ukifa wew ndio utahesabiwa haukuowa na hautazikwa kwa heshima ya alieoa.

2. NYUMBA TOBHU, Hii ndio inakalilika kuwa ni mwanamke anaowa mwanamke mwezie ila kwa sisi wakurya hatuamini hivyo na haiko hivyo,
Hii inatokea kama kijana aliowa na hawakubahatika kupata kijana wa kiume, au mama hakuzaa kijana wa kiume, kama awali nilivyowaambia kuwa wakurya hawaamini katika mwanamke kurithishwa mali za familia kwa kuwa wanaamini mwanaume ndie anaebaki nyumban na mtoto wa kiume ndie anapaswa kuendeleza familia hiyo huwalazimu kutafta binti na kumtolea mahari na hapo huchaguliwa kijana mmoja katika ukoo ili azae nae na huyo binti alieolewa katika familia hii akizaa watoto wakiume ndio wanakuwa warithi halali wa mali za familia na kuendeleza kizazi, lakini pia hapa huyo binti anapewa uhuru wa kutafta mwanaume yoyote atakaemuamini na kumtambulisha na kuwa kama mme wake na kuzaa nae ila sharti watoto atakaozaa huyo mwaname sio wake pia hatakuwa na mamlaka yoyote juu yao Bali watoto hao wataitiwa majina ya familia ya alipoolewa binti,
Yeye BAba watoto mshahara wake ni mbususu tu.

AINA YA WANAWAKE AMBAO NI KAPAUMBELE KATIKA NDOA HIZI NI.

Mabinti waliozalia Nyumbani (singlemothers) ambao katika kabila la kikurya huchukuliwa kama laana na aibu katika familia zao, na wale dada zetu wenye sura kama yule mama aliekuwa waziri wa Elimu miaka flani katika taifa la kusadikia, pia wale mabinti ambao wametoka katika familia zenye kashfa mbayambaya ambazo kuoleka kwao ni vigumu.

MYTAKE: Naunga mkono tamaduni hii kwa100% kwani husaidia familia ya mfiwa kuamini bado ndugu yao wako nae,
Lakini pia husaidia kuendeleza vizazi na koo za watu pontential katika jamii,
Pia husaidia mabinti ambao ni rejected kupata uhifadhi kwa maana ya ndoa, lakini pia finally huheshimisha single mothers na watoto wao kupata care nzuri na kupata misingi mizuri pia tofauti na kama wangeolewa na wanaume ambao wangewatenga watoto hawa wasio na hatia.
 
🤣🤣🤣🤣
 
Na kuhusu middle name za kike haimaanishi tunatumia mfumo wa matrinual ila hayo majina Bhoke, matinde, Chacha , etc ni majina universe hayana jinsia kama unavyodhania wew, na wakurya pia hupenda kuwaita waototo wao majina ya ndugu zao waliotangulia mbele ya haki so unaweze kuta mama mtu alikuwa anaitwa Ghati, au Bhoke, na baada ya kufariki ndugu yake naweza kumpa mwanae wa kiume jina la mama yake kama kumbukumbu na heshima kwa marehem so kijana huyo aliepewa jina la mama yake akikuwa na akawa na watoto hapo ndipo tutegemee kuona watoto wake wanakuwa na second name ya kike ila linakuwa jina la baba yao. Na hii ilianza kitambo ndio maana majina haya kwa sasa yamekuwa universe ila asili yake yalianza hivo. Huyo mtoto akikuonesha baba yake na ukamdadisi huyo baba utakutwa alipewa jina la urithi la mama yake baba yake.
 
Mkuu ikiwa mwanamke ameolewa na hajabahatika kupata mtoto taratibu zipi huwa zinafuata.
 
Hii nimeshudia Kijiji kwetu tena jirani na nyumbani Mama mmoja hakupata aliolewa hakupata Mtoto, akaoa Mkamwana naye hakupata Mtoto, mukamwana akaoa mukamwana akapata Watoto yule Mama naye akaoa tena na akapata Watoto
Bro kwema!
 
Mkuu ikiwa mwanamke ameolewa na hajabahatika kupata mtoto taratibu zipi huwa zinafuata.
Ikitokea alieolewa asipate mtoto wa kiume ataoa tena, na ikishindikana kabisa watatafta mwanamke ambae ni single mother ambae tayari ana mtoto wa kiume wanamuoa na kijana atarasmishwa kwa majina ya familia husika, na kisha atarithishwa hata kama akiwa mkubwa
 
MAJIBU NI HAYA HAPA.

Kwanza hakuna sehem wala ukweli wowote kuwa mwanamke anaowa mwanamke mwezie katika kabila la kikurya wakurya ni moja ya tamaduni za watu ambao Ant-Homosexual kwa hiyo msiwe na dhana hiyo kwamba mwanamke anauoa mwanamke mweziwe.

Ila sasa mwanamke anaetambulika kama muoaji kwa makabila yenu sisi kwetu anatambulika kama mama mkwe ambae Mme ni hewa. Ila kijamii anakuwepo na anajulikana isipokuwa kwenu waswahili ndio mnaamini hamna mwanaume.

Nitaelezea kiurefu kidogo na sababu ya kwanini hiyo inatokea,

KWANZA, katika kabila la wakurya ni watu wanaamini katika urithi sana,

PILI, Kabila la wakurya ni watu wanaoamini katika muendelezo wa kizazi,

TATU, Katika kabila la kikurya Mwanamke halitishwi na wanaamini mwanamke hawezi kuendeleza kizazi cha familia aliyozakiwa kwa kuwa mwanamke anaolewa na kwenda kuendeleza kizazi katika familia alioolewa na sio kwao.

KUNA AINA MBILI ZA NDOA ZA AINA HIYO ZOTE ZIKIWA NA LENGO MOJA ILA ZINATOFAUTIANA KIMAZINGIRA NA KWA MAJINA,

NYUMBA MBOKE, hii nyumba mbokeh inatokea kama kijana mkubwa katika familia ambae tayari alikuwa amepitia hatua za kiutu uzima kwa maana ya jando, kwa sababu wakurya kwao jando haifanyiki kama usafi tu bali inafanyika kama hatua ya kumvusha kijana katika utoto na kuingia katika utu uzima, ndio maana wakurya tukio hilo hulifanya kama kipimo cha ujasiri kwa kijana na kama kipimo cha mtu ambae ataweza kukabiliana na changamoto za utu uzima na familia, tukio la SUNA hufanyika bila Ganzi na moja ya sheria inatakiwa mhusika anaefanyiwa asijitikise wala kupepesa jicho asimame wima hadi zoez litakapomalizika, tuachane na hili la suna.

Hivyo inapotokea kijana amepitia hatua ya utu uzima kwa maana ya sunna hapo anatakiwa kuowa na kuendeleza kizazi chake, sasa ikitokea kijana huyu akapitiwa akafariki au akapata tatzo lolote la kiafya ambalo hawez tena kuowa,

Hapo ni jukumu familia yake kwa maana ya wanafamilia yake kukaa chini na kutafta mke anaolewa kuja katika familia hiyo kwa lengo la kuendeleza kizazi cha marehem ndugu yao, hii wanaitumia kama moja ya njia za kum'enzi marehemu lakini pia kuendeleza kizaz chake na kuamini kuwa bado wapo nae,

Suala hapa ni yupi anaepaswa kuchukua jukum la kulea huyu mwanamke ambae anaolewa kwa niaba ya marehem, Hapa kinakaa kikao cha familia kisha anachaguliwa mmoja amabae atachukua jukum la kuowa huyo mwanamke na kisha atamhudumia yeye na atazaa nae ila watoto watakaozaliwa sio wake tena bali wataitiwa jina la marehem baba yao ambae hakuwazaa,

Ubaya wake ukiteuliwa na ukakataa huwa familia inakuacha ila mke utakaemuowa wewe mtaendelea kuishi nae ila kuna siku utaambiwa haujaowa kwa kuwa mke ulienae ni mke wa marehem ndugu yako, maana mara nyingi pia anaechaguliwa kufanya hivyo anakuwaga mdogo wa marehem, na kijamii ya wakurya mdogo hatakiwi kuowa kabla ya kaka yake hivyo utaambiwa uliowa kabla ya kaka yako na mke wako sasa atakuwa mke wa marehem, na hata ukikataa haitasaidia kwa kuwa jamii itaamini wewe bado haujaoa, na hauna watoto, kwa hiyo kwa kunusuru hilo inakubidi uowe mwanake mwingine ili unusuru ulienae katika ndoa na abaki kuwa mkeo anaetambulika kijamii, na ukigoma ujue siku ukifa wew ndio utahesabiwa haukuowa na hautazikwa kwa heshima ya alieoa.

2. NYUMBA TOBHU, Hii ndio inakalilika kuwa ni mwanamke anaowa mwanamke mwezie ila kwa sisi wakurya hatuamini hivyo na haiko hivyo,
Hii inatokea kama kijana aliowa na hawakubahatika kupata kijana wa kiume, au mama hakuzaa kijana wa kiume, kama awali nilivyowaambia kuwa wakurya hawaamini katika mwanamke kurithishwa mali za familia kwa kuwa wanaamini mwanaume ndie anaebaki nyumban na mtoto wa kiume ndie anapaswa kuendeleza familia hiyo huwalazimu kutafta binti na kumtolea mahari na hapo huchaguliwa kijana mmoja katika ukoo ili azae nae na huyo binti alieolewa katika familia hii akizaa watoto wakiume ndio wanakuwa warithi halali wa mali za familia na kuendeleza kizazi, lakini pia hapa huyo binti anapewa uhuru wa kutafta mwanaume yoyote atakaemuamini na kumtambulisha na kuwa kama mme wake na kuzaa nae ila sharti watoto atakaozaa huyo mwaname sio wake pia hatakuwa na mamlaka yoyote juu yao Bali watoto hao wataitiwa majina ya familia ya alipoolewa binti,
Yeye BAba watoto mshahara wake ni mbususu tu.

AINA YA WANAWAKE AMBAO NI KAPAUMBELE KATIKA NDOA HIZI NI.

Mabinti waliozalia Nyumbani (singlemothers) ambao katika kabila la kikurya huchukuliwa kama laana na aibu katika familia zao, na wale dada zetu wenye sura kama yule mama aliekuwa waziri wa Elimu miaka flani katika taifa la kusadikia, pia wale mabinti ambao wametoka katika familia zenye kashfa mbayambaya ambazo kuoleka kwao ni vigumu.

MYTAKE: Naunga mkono tamaduni hii kwa100% kwani husaidia familia ya mfiwa kuamini bado ndugu yao wako nae,
Lakini pia husaidia kuendeleza vizazi na koo za watu pontential katika jamii,
Pia husaidia mabinti ambao ni rejected kupata uhifadhi kwa maana ya ndoa, lakini pia finally huheshimisha single mothers na watoto wao kupata care nzuri na kupata misingi mizuri pia tofauti na kama wangeolewa na wanaume ambao wangewatenga watoto hawa wasio na hatia.
Nashukuru sana kwa majibu na ufafanuzi.

kila nilipoomba watu wanieleweshe, naona kama walikuwa hawawezi kwa sababu sio jambo geni wala la ajabu kwao. ndo maana hawakuweza kufanya maelezo yao yaeleweke.
 
Ikitokea alieolewa asipate mtoto wa kiume ataoa tena, na ikishindikana kabisa watatafta mwanamke ambae ni single mother ambae tayari ana mtoto wa kiume wanamuoa na kijana atarasmishwa kwa majina ya familia husika, na kisha atarithishwa hata kama akiwa mkubwa
Mkuu nimekuelewa. Hizi taratibu za wakurya nimezipenda haijalishi marehemu kafariki bila mtoto ama hana uwezo wa kumpa mwanamke mimba sheria lazima kizazi kiendelezwe kwa.
 
Back
Top Bottom