kenyamanyori
JF-Expert Member
- Feb 9, 2014
- 734
- 326
CCM WANATAKA KICK WASIYOISTAHILI. WAMEKWISHA. NDIO MAADUI WA TAIFA HILI.
Hakuna hoja za Msingi alizotoa zaidi ya takataka tupu!!We Mhaya hopeless and useless, stop ad homine arguments, stop arguing by character assassination. ametoa hoja jibu hoja. Matusi hayajibu hoja! Utaahira unatoka wapi?
Na wala hawajawahi............Nakumbuka kilichotukuta kwenye samaka wa magufuli kwa ajiri ya mjinga na mkurupukaji mmojaKamwe ccm hawana wema na nchi hii
ccmTwambie sasa nani siyo corrupt?
ccm wanatupigisha mark time for >50 years of moving backward....Eti wanajifunza kwa makosa kila mwaka huku wakiumiza watzWakati miswada ya kipuuzi ya madini ikipitishwa bungeni Mhe. Raisi Magufuli alikua mbunge if m keeping my records well hakuwahi kusimama kupinga..
Hana lolote huyo tumeshamzoea na maneno yake kama vuvuzela!
Na mimi ni Mtanzania pia.
Tofauti kati yangu mimi na wewe na Magufuli ni hii: Mimi nimepigania nchi yangu katika masuala haya tangu mwaka '99.
Wakati huo tulikuwa na mgodi mmoja tu wa dhahabu, Resolute Golden Pride Nzega. Bulyanhulu ilikuwa haijajengwa. Geita ndio kwanza walikuwa wanafukuza wanakijiji wa Mtakuja.
Nadhani nilikuwa wa kwanza katika nchi hii kupiga yowe kwamba tutaibiwa sana kwenye sekta ya madini.
Wewe sijui ulikuwa wapi wakati huo. Najua Magufuli alikuwa wapi: upande wa MaCCM na wawekezaji hawa.
Nimepigana na wawekezaji hawa mahakamani, kwenye medani ya kisiasa ndani na nje ya nchi hii kwa zaidi ya miaka 15. Nimetetea wananchi completely free of charge Bulyanhulu, Tarime, Nzega, Geita, n.k.
Sijui wewe ulikuwa wapi lakini najua Magufuli alikuwa upande wa nani: wa MaCCM na wanyonyaji hawa.
Soma Rai ya tarehe 17 Julai, 2001, uone tulimwambia nini Mkapa siku anaenda kuzindua Mgodi wa Bulyanhulu.
Sijui ulikuwa wapi lakini najua Magufuli alikuwa wapi: alikuwa anatetea tumbo lake na matumbo ya wanyonyaji hawa.
Nilikamatwa na kushtakiwa kwa uchochezi kwa sababu ya Bulyanhulu. Hiyo ilikuwa December 2002. Nilikaa na kesi hiyo mahakamani Kisutu kwa miaka sita.
Sijui ulikuwa wapi ila najua Magufuli alikuwa wapi: upande wa watesi wa wananchi na wanyonyaji wa rasilmali zetu.
Leo Magufuli anajifanya mzalendo na anahoji uzalendo we yeyote anayepingana nae.
Ni muongo. Anatafuta umaarufu wa kisiasa kwa wasiojua na wasiokumbuka. Ataupata. Kwa siku chache tu. Mark my words: ataumbuka na mtaumbuka.
Mimi ninampinga hadharani. Sio mnafiki, na sijahongwa. Ninampinga kwa sababu atatusababishia matatizo makubwa zaidi kuliko tuliyonayo sasa.
Huo mchanga atauachia upelekwe ambako umepelekwa kwa miaka 16 iliyopita. Kama sheria ndiyo hiyo na mikataba ndiyo hiyo hana pakwenda.
Tatizo ninaloliona ni kwamba by the time anawarudishia mchanga wao, Tanzania itakuwa imekuwa a basket case kama Zimbabwe.
Na tutakuwa tumelipishwa mapesa mengi kama fidia na arbitral tribunals za kimataifa kwa kuvunja mikataba na wawekezaji hawa.
Kama kuna anayefikiri uzalendo ni kufumbia macho masuala haya basi huyo na amuunge mkono Magufuli kwenye upofu wake wa kujitakia.
Ripoti ya Prof. Mruma haitamaliza hata nusu saa under serious scrutiny. Zaidi ya majina ya maprofesa walioiandaa, ripoti hii haina credibility yoyote. Ni kazi ya kisiasa iliyopakwa rangi ya usomi.
Kama umefuatilia taarifa za kitaalamu za Bulyanhulu hata kabla ya Barrick Gold kuingia mwaka '99 utajua ninasema nini.
Sutton Resources, Outukumpu Oy na hata STAMICO walishafanya utafiti mkubwa juu ya utajiri wa Bulyanhulu. Taarifa zipo na zimekuwepo kwa hata mbumbumbu wa jiolojia ya madini kama mimi.
Hiki alichoambiwa Magufuli ni rubbish, hata kama ni ya kiprofesa. Rubbish. Hatuibiwi kwenye mchanga, that's the rubbish fed on the unlettered.
Tunaibiwa kwenye sheria. Kama hamuoni hilo then God have mercy on us.
CCM . . CCM . . . CCM . . . . CCM CCM . .Kwani hapa kelele za msingi ni nini kuhusu hiyo report ya Magu?
Ni mikataba mibovu au ni udanganyifu kwenye report husika ...?
Usitegemee mtu tabia yake eti abadilike, tena kama yeye ni mmojawapo kati hao je una imani kama asingefanya madudu. Asikudanganye mtu mwizi haachi wizi.Nani kakwambia siasa ni uadui?kila kiongozi anaweza kubadili tabia kama amekusudia
Takriban miongo miwili Lissu amekuwa akipinga wizi unaofanywa na wachimbajihuyu ni chizi tuu aseme kama mikataba iliyo sainiwa ina halalisha kudanganya kiasi cha madini kilichomo ndani ya mchanga....
Tahira huyu
Wewe labda utakua hujasoma alichoandika lissu au kama sivyo basi unajitia upofu wa makusudi. Lissu amekua very clear...kwamba hatuibiwi kwenye mchanga, tunaibiwa kwenye sheria. Recommendation yake ni clear kwamba tukarekebishe sheria yetu ya madini. Bila hivyo haya mambo ya michanga ni sawa na kutwanga maji kwenye kinuTatizo la Lissu anaongea sana bila kurecommend au kuingia kusaidia nini kifanyike ili kushinda Vita hii.
Maneno makali na kebehi hayatasaidia kuiokoa nchi yetu dhidi ya unyonyaji wa nje.
Rais ameanzisha Vita ambayo huko nyuma anakokulalamikia Lissu hakuwa na misuli hiyo.
Lissu aungane na timu ya Magufuli, tusonge mbele.
Ushindi wa JPM ni wetu sote, kushindwa kwake ni hasara yetu sote mpk ya Lissu mwenyewe
Yani! ku-deal na ccm inachosha sana... embu shauri ni jisi gani Lissu (practically) anaweza kutumia uanasheria wake kututoa kwenye hili, embu eleza ni steps gani Lissu anazotakiwa kufwata ili ccm iweze kumruhusu kutumia uanasheria wake kutuchomoa kwenye huu msala... Please fafanua ni nini anachotakiwa kufanya? Je ni bungeni? Inawezekana kwa Lissu kutumia uanasheria wake bungeni kuishauri serikali?We umeandika kiungwana sana na ndo inavyotakiwa wakati unaitetea nchi yako siwezi kukujibu ujinga kwa sababu hubishani umetoa ukweli wako,bnafsi simchukii Lisu wala post zake,ila nachomaanisha mimi ni ushiriki wake wa moja kwa moja bila kujali makosa yalifanywa na nani tukaingia mikataba uchwara manake kama ni hasara itatukuta wote so, kipi bora,atumie uanasheria wake kutuchomoa huku tulipo au aendelee kuilaumu serikali ya CCM na kututabiria anguko!!?