Majibu ya Tuhuma Dhidi Yangu!

Mkuu HKigwangalla,
Nakubaliana na wewe kwa mambo mengi uliyosema....kwamba si dhambi kwa Mbunge kupata misamaha ya kodi na si za dhambi kwa yote uliyosema kwamba si dhambi! In fact, si dhambi vile vile hata kama ingekuwa ni kweli unamiliki 78% ya hisa na Shemeji akawa anamiliki 22%......NARUDIA, sio DHAMBI na yeyote anayeona hayo ni dhambi basi hatupe hoja za maana hapa!!

Hata hivyo, bado hapa umetenda dhambi, tena dhambi iliyotajwa hata kwenye Misahafu ya Dini; dhambi ya UONGO!
VOICE......SAUTI inakushitaki! Waandishi wa Riwaya/Tamthilia/Scripts(sana sana Scripts ambazo zinabeba Dialogue nyingi zaidi) nazani watanielewa zaidi ninapozungumzia suala la SAUTI! Unaweza kujiona kwamba kilichopo mbele yako ama unachokitoa mbele yako ni MAANDISHI tu lakini kwa mwandishi wa Script anaweza kuisikia kabisa sauti yako kutokana na maandishi yaliyopo mbele yake!

Hapa nilichogundua ni kwamba umedanganya kusema wewe unamiliki 40% na Wife anamiliki 11%. Hapa wala siwezi hitaji uthibitisho wa BRELA coz' I know huko BRELA ndivyo inavyosomeka, Kwamba HK anamiliki 40% na Mrs. HK anamiliki 11%! Swali ni dogo tu; je, 49%(au sehemu yake) umemmilikisha nani kwa niaba yako? Kuwa mkweli hapa ili upunguziwe madhambi ya Uongo ingawaje bado nitataka kufahamu ni kwanini ummilikishe mtu mwingine kwa niaba yako! Unakwepa nini?
 
Last edited by a moderator:
Mnavyo muuliza maswali magumu mnataka asirudi tena kujibu hoja, kwani anahako kadesturi
 
chuo ni chake, na ni binafsi. kampuni ni yake. then anapata msamaha wa kodi. apa kuna walakini. PCCB wanatakiwa kufanya uchunguzi wa kina
 

Waswahili wanasema [Al] muhitaji hanith.i walau kama rijali

Sasa yeye anahitaji watu kisha anajitia urijali kwao watu hao hao

Au ndio shukurani ya punda?
 

Kama mimi niko bize na kupiga mahesabu kodi ya mapato serikali imepunguza ngapi
 
Hivi hii emegent africa ltd. ni kampuni ya ujenzi? Swali kwako ndugu hamisi

Kwa jinsi alivyo chakazwa hapa sidhani kama atakuwa na guts za kurudi hapa na kujibu hata swali moja alilo ulizwa.....Gingwala umelikoroga zaidi sasa itabidi ulinywe..
 

Naona wewe JF inakukosesha usingizi kabisa hizo tuhuma zimetolewa kwenye magazeti huyo GAMBA HK kaamua kuzijibu umu sasa JF imeharibiwa kivipi unataka tukubaliane na utetezi wake wa kitoto unatakiwa kujua tuliopo umu tuna bongo nzuri za kufikiria hatuwezi kusikiliza utetezi wa kipuuzi kama wa HK.
 
jamani CCM tuoneeni huruma muda mwingine... kuna life after death..wananchi wenu mnawaomba kura vizuri wakati wa uchaguzi na baada ya hapo mnawasulubisha..so far,ukifa huendi na kitu my dear!!!!i feel sorry for you
 
halafu kinachosikitisha zaidi ni mtu kupost kitu halafu hajibu chochote after that..its better kukaa kimya kuliko kuleta thread ambayo huwezi kujibu watu later..damn
 


Mhe.Mbunge.
Kama unadhani haya ndiyo majibu dhidi ya wanaokutuhumu/kusema uongo kama ulivyojitetea basi kuna uwalakini.

Maelezo yako hayaonyeshi kushawishi kujenga ukweli na zaidi umejenga maswali mengine kuliko majibu na hujaguzia baadhi ya madai yaliyotolewa na gazeti husika hivyo unaongeza nguvu ya hoja kwa tuhuma zilizoandikwa dhidi yako.


Mfano mdogo wa baadhi ya maswali mapya angalia maneno yenye uwekundu kwenye bandiko lako.
Pili unataka kushawishi watu eti wapi risiti kweli unazungumza kwa hadhi ya Udokta/Mbunge-Wapi umeona mlipa rushwa anadai Risiti ? au mpokeaji anatoa Risiti? acha utani labda umeteleza mawazo.
 
Kigwangala hana makosa tatizo ni mfumo tulio nao, jakuna jinsi ya kuzuia conflict of interest, je mheshimiwa ametaja kampuni hiyo.
 

Mkuu CHAMA na wewe unaunga mkono upuuzi huu.Ifike mahali tuweke pembeni itikadi zetu za kisiasa kwa ajili ya kuliokoa Taifa letu.Mbali na tuhuma anazo tuhumiwa nazo ziwe za kweli zisiwe za kweli.Ukiyasoma maelezo yake inaonekana ni mtu mwenye uwezo mkubwa sana kifedha.Mtu ambae hakusitahili hata kusamehewa kulipa kodi na serekali yetu kama ingekuwa makini kama alisamehewa kweli kwa mjibu wa maelezo yake yasiyo na ushahidi.Huu ni upuuzi mwingine tunao upinga unaofanywa na serekali yetu.Mtu mwenye uwezo mkubwa kabisa wa kulipa kodi anasamehewa kulipa kodi huku mwananchi ambae ni masikini kabisa ambae anatakiwa kusaidiwa anapelekewa mgambo kupigwa mabuti ili aweze kulipa kodi kwa nguvu pengine na kufungwa kabisa.Eti tajilri mkubwa kabisa mwenye nazo anasamehewa kulipa kodi na yeye bila hata chembe ya aibu anajitokeza hadharani nimesamehewa kulipa kodi na serekali kwa kisingizio cha kujenga Chuo cha afya.Hicho chuo cha afya kitakuwa kinatoa huduma bure kwa mwananchi?.
 
Last edited by a moderator:

Ambazo ukizijumlisha ni 51% ambazo kwa pamoja zinawafanya wawe majority shareholders wenye ku influence maamuzi ya kampuni, ukiacha zake pekee 40%. Mh. Hamis hajui hata elementary company law & corporate governance ndiyo sababu anatoa majibu mepesi hivi!
 
Hkingwangala

Ni kweli jina unalotumia sio lako.
Ni kweli unaasili ya nje ya Tanzania na uraia wako unawalakini.
Ni kweli unahisa kwenye kampuni tajwa.
Ni kweli kampuni tajwa ni ndogo hivyo wewe na mke wako mnashiriki moja kwa moja kwenye utendaji wa kila siku.

Ni kweli kabisa uliichongea mchongo kupata tender husika.
Ni kweli ilikwepa ushuru na kuagiza vitu vingi vya biashra yako visvyokwenye tender.

Malezo yako marefu yamethibitisha ufisadi mkubwa kwenye kampuni yako unayoyafanya ukitumia kofia ya ubunge. Hakuna ulichokataa.

H kingwangala ni Fisadi kama RA, EL nk mnatofautiana kwenye tarakimu tuu.

Huna uadilifu wala hadhi ya kuwa Mbunge. Mwizi ni mwzi hata akiiba kalamu.
 

katiba mpya mtasusia? au mlikuwa mnapima hali ya hewa?
 
Huyu jamaa amewai kutishia kujiuzulu ubunge.
Kumbe ilikua mkwara tu, ccm ndio inayombeba.
 

Kumbe hata hivyo ulipewa nafasi ya kueleza – japo si kwa mapana, Mbunge wangu! Umenisikitisha kwa kutuonyesha kuwa mara zote umekuwa ukiyamaliza na wahariri – japo swali ni je maongezi haya hayakuhusu ‘bahasha’ ili wasiendelee kukuanika?

Nimependa unavyowaingiza CDM kiaina ili ku-win sympathy yao, I suppose!

Mwaga ushahidi tuliouzoea wa documents!

Sijui huu ujumbe unawapa CCM au watu gani na kwa nia ipi! Nawaachia wachambuzi makini watudadavulie zaidi
 
Kaka Saidi Bagaile, unathibitisha mwendelezo wa kifo cha ccm, kama yule RC wa Arusha. Umeanza kuzikana kampuni zako, halafu baada ya kutuorodheshea uharam wa utajiri wako umekuja kukiri kwamba wewe ndo "Major Stakeholder" Yaan ni sawa na Dowans tu ya Rostam Aziz kutuambia kwamba yeye sio mmiliki ila amepewa "Power of Attoney 100%" Halaf wewe na huyu jamaa wote hamna asili ya Tz. Watz tuamke. Mwanamke wa JF amka
 
FROM BEN SAANANE POST

3:VIJANA WALIOPEWA DHAMANA


Kuna vijana waliopewa dhamana lakini wameishia kuwa mafisadi wakubwa.Hawa ni wasaliti na ni kikwazo kwa vijana wengi kuaminiwa na kupewa dhamana.

Gazeti moja leo limeripoti Dr.kigangallah kutumia vifaa vilivyolipiwa ushuru kwa ajili ya kujengea hospitali na badala yake akafungua dukaa la vifaa vya ujenzi kupitia kampuni anayomiliki hisa asilimia 78 inaitwa emergent african Limited na kuuzia wafanya biashara mbali mbali na miongoni mwao ambaye ni mojawapo wa wanachama wa kundi la Stop Ben Saanane (SBS) ni MRISHO GAMBO.Huyu ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe

Inashangaza sana mkuu wa wilaya tena kijana kama huyu anashirikiana na mafisadi kuhujumu Afya ya walalahoi

Vigae (Tiles zilizoingizwa nchini) na Emergent Africa ya Dk Kigwangala tokea China na kupewa msamaha wa kodi Mrisho Gambo Mkuu wa Wilaya ya Korogwe aliuziwa mabox 114 kwa shilingi 22,OOO. Mtu ambaye anashirikiana na Mbunge wa CCM kuibia nchi, kununua bidhaa haramu zisizolipiwa ushuru, zilizoonekana ni mali za kituo cha afya ana usafi gani wa kuendelea kuongoza wananchi? Aseme arudishe vigae vya Kituo cha afya cha Nzega alivyotumia kujengea nyumba yake.


Sasa aje hapa abishe tulete ushahidi.Nashangaa watu wanajifaragua na ID humu kutusi watu kumbe wao ndiyo mafisadi wakubwa.Wao wanasema uongo juu yetu,Sisi tutasema ukweli juu yao hadi watakapoweka makombora yao ya uongo chini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…