Majibu ya Kigwangalla: Kwa Nini Sikusaini Hoja ya Mhe. Zitto Zuberi Kabwe (MB)!

hili lijamaa ni hatari sana, akiwa waziri tumekwisha.
nami pia nilionaga thread moja hapa akiwa anaelezea mambo katika njia ambayo niliiona ni ya kitoto zaidi lakini nikadhani labda alipitiwa tu.

Sasa hii taarifa aliyotoa hapa inaonekana hata hivyo vyeti vya udaktari alivipata katika 'affirmative plan' labda. Kweli nazidi kuamini zaidi ya nilivyokuwa nikiamini kuwa nchi ya Tanzania imejaa matatizo!
 
You are wrong Lemtuz! anatakiwa kusimama kwa miguu yake yote miwili na kuwatetea wananchi walomchagua na si madudu yanayofanywa na serikali kupitia mgongo wa chama chake.

Mkuu usishangae Le mutuz kumpongeza HK,hao wote akiri zao zinafanana tofauti zao ni miili tu.
 

Tatu, msisahau kitu kimoja cha muhimu kabisa. Kwamba, mimi ni Mbunge kutokea CCM na kama walivyo wengi wenzangu hatukusaini kwa sababu hatuwezi kuiangusha serikali ya CCM kwa hoja inayoletwa na Mbunge wa Kambi ya Upinzani! Kwa maana hiyo sisi wabunge wa CCM tuna jukumu la kuilinda Serikali inayopatikana kutokana na sisi kuwa majority.


Mkuu hapo kwenye RED nimekuelewa sasa vizuri. ww ndo mnafiki wa hali ya juu. Hoja yoyote inayotoka Upinzani bila kujali uzuri/ubora/maslahi ya hoja yenyewe hutaunga mko (Simply coz it comes from opposition side).

Kwenye BLUE Umepoteza dhana na haki ya kuwa Mbunge kwa kuvunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayokutaka KUISIMAMIA NA kUIWAJIBISHA SERIKALI (ww umekiri kukilinda hence you dont have the CREDIBILITY OF BEING MP)
.
 
Wacha ubukanga wako wewe hata ujumbe wa nyumba kumi huuwezi. Wewe inaonesha hata u prefect au monitor wa shule hujawahi kuwa nao.

Mkuu usikurupuke na kujudge watu kwa maandishi...

Huyo kilaza yuko field yet amdeliver lipi la maana zaidi ya kunyemelea vyeo??

Ukiwa kipofu tokana na dini yako jaribu kuwa mkweli na muwazi ndivyo sisi wa upande wa pili tunavyofundishwa, kwa ujinga uliojazwa kichwani mwako huko magharibi hata ukiona mtu ana fail kiasi gani utatetea tu, wewe pia uko katika kundi la 'vilaza'!!

Mimi siwezi kuamini kwa maneno yake kwamba huyu ni kiongozi shupavu, la hasha!! Na lazima ni conclude kwamba hawa wanaojiita vijana ndani ya magamba wanajifahamu kabisa wakitoka nje ya hilo genge hakuna wa kuwabeba na kuwawezesha kuiba kura na kupata ridhaa ya wananchi kwa haki kabisa, wote walio huko ni waganga njaa..

Hawa wehu kama wewe wamegeuza nchi yetu kuwa Tom Tiddler's Ground, siwezi kutiwa kichefuchefu na watu kama nyie!!
 
Mbunge Zitto alikuwa na nia ya dhati ya kumuondoa WM asingekurupuka kiasi kile, angewashirikisha watu wengi zaidi, hususani wabunge wa CCM, Mhe. Zitto is smarter than this, I know him!
... mimi ni Mbunge kutokea CCM na kama walivyo wengi wenzangu hatukusaini kwa sababu hatuwezi kuiangusha serikali ya CCM kwa hoja inayoletwa na Mbunge wa Kambi ya Upinzani!

Wakatabahu,
HK.

Dr. mzima unajikanyaga kanyaga kiasi hicho au kwa vile uko CCM huna point za kujitetea. Wewe ulitaka Zito awashirikisheje, kwa kuwapa rushwa? Kaitisha saini mkakataa, unataka afanye nini zaidi! If you appriciate his smartness why didn't you sign for the sake of the Country? Umeonyesha kutojiamini zaidi ya kutanguliza maslahi yako binafsi kwa mgongo wa Chama Magamba!

Umeshidwa kisimamia maslahi ya Taifa aka wananchi una fuata upepo wa wenzako wengi ambao ni wanafiki! Kumtosa WM siyo kuangusha serikali Dr-we vipi? EL aliondoka serikali haikuyumba, kumbuka Nyerere alisema "nchi itayumba kama Rais akiondoka! Sokoine aliondoka bila serikali kuyumba! Nyie ndo mliotufikisha hapa, eti kwa vile hoja imetolewa na wapinzani hata kama ina maslahi kwa Taifa mnapinga tu-Hovyo mnafiki wewe nyamaza hulindi maslahi ya Taifa! Una-anika unafiki wako humu, unashindwa hata kuungana na kijana mwenzako Filikunjombe!
 
I keep quiet so that my brain can cool for future use instead of using it here and sustain a ban
 
MD, MPH, MBA.....halafu anatoa Statement hii kwenye Public??????? Hivi ni vyeti vya wapi? Dah! Ama kweli, unahitaji kuwa na akili ya maiti kutetea Chama cha Magamba! Na hapa ndipo Kigwangalla amedhihirisha kuwa tayari yeye ni maiti.

R.I.P. Janga la Taifa! Pambaf..........
Ndugu zangu wanabodi,

Nimeamua kuja kujibu kama ambavyo mngependa nifanye. Siyo kwamba nimekimbia JF, la hasha. Siwezi kukimbia na wala sina sababu ya kufanya hivyo. Ni kwamba gadget yangu ninayotumia kwa mawasiliano ilipata mushkeri na nikawa nalazimika kutumia kompyuta na bahati mbaya sana kwa jinsi nilivyokuwa bize na ujenzi wa Taifa nilijikuta nakosa muda wa kukaa kuanza ku-surf. Nisamehewe kwa hilo.

Mimi sijawahi kuwa mnafiki, at least kwa alama tatu za mnafiki kama tunavyofundishwa sisi waislamu. Kwa faida ya mjadala huu, niseme alama zenyewe. Moja ni kuwa akitoa ahadi hatekelezi. Mbili, ni akiaminiwa anahalifu na tatu, akizungumza husema uongo. Namshukuru Mungu sina hata moja ya alama hizi na hivyo kushindwa mtihani wa kuwa 'mnafiki'. Ungeniita mnafiki kama nisingekuwa tayari kutoa maelezo ya maamuzi yangu, ama kama ningewasaliti CCM na kupeleka siri za huku kule, ama kama ningeahidi kuunga mkono hoja hiyo kisha nikakimbia. Leo hii mimi niko chama kimoja tu, CCM, na nitafanya mambo yanayokubalika ndani ya CCM. Siku nikihamia CHADEMA/CUF/NCCR basi nitafanya ya huko bila kusaliti kule na kurudisha CCM ama kupeleka kokote kule kinyume na utaratibu. Huo ndiyo msimamo wa ukweli na siyo unafiki.

Kuna uwezekano wa kuwa na tafsiri tofauti kutokana na pre-conceptions zetu vichwani, siwezi kulizuia hilo hata kidogo. Kwa kuwa ninakalia kiti cha uwakilishi, nina-feel ninawajibika kwenu kutoa maelezo ya msimamo wangu kwenye hili, na wala sintomumunya maneno.

Kwanza, hoja yenyewe siikubali. Kwa sababu ninaamini serikali ya Chama Changu (CCM) haijashindwa kufanya kazi ya watanzania kiasi cha kung'olewa madarakani kwa namna hiyo. Pili, naamini na ninakubali, na kwa hakika ninakerwa na baadhi ya watu waliopewa dhamana za kuongoza baadhi ya ofisi nyeti za umma wametuangusha watanzania, na hivyo naunga mkono hoja ya kutaka kuwatoa hawa. Mhe. Zitto Kabwe (MB) alipokuwa akijumuisha hoja yake, alitaka serikali iwawajibishe baadhi ya mawaziri na watendaji wakuu wa Wizara na Mashirika ya umma, na akasema kama serikali haikufanya hivyo kufikia J3 iliyofuata basi sisi (Bunge) tuna uwezo na WM na kwamba atapitisha karatasi ya kukusanyia saini 70 ili kukidhi matakwa ya kikanuni ya kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na WM; kwa tafsiri yangu ni kwamba Mhe. Mbunge alilenga kuweka presha kwa serikali, kuitaka iwajibike kwa kuwawajibisha mawaziri hao (watano) kama alivyowataja yeye. Kwanza mwanzoni nilielewa hivyo. Baadaye jinsi ilivyopokelewa na wadau mbalimbali nikaona kama hoja inahama sasa na kwamba si mawaziri hao watano wenye tuhuma mbalimbali, ni PM na kwa maana hiyo ni serikali yote Bungeni! Hili mimi siliungi mkono na silikubali. Nasema wazi hivyo kwa sababu, mimi nina imani na WM, nina imani na Rais - aliyemchagua WM, na nina imani na Mawaziri wengine wengi wazuri tu kwenye serikali hii, na msimamo wangu huu uko wazi sana tu.

Mbili, sioni sababu ya kuiingiza nchi kwenye wasiwasi wa kiutawala kiasi hiki. Na kwa kuwa wabunge wa CCM kwenye party caucus tulikuwa tayari tumeishaambiwa kwamba kuna mawaziri wameamua kujiuzulu wenyewe (tena siyo wale watano, ni wanane kabisa) kutokana na tuhuma hizo na presha kutoka kwa wabunge wa CCM na wengine, sikuona sababu ya mimi kusaini hoja ya Zitto (ambayo kikanuni ilikuwa imekosewa - kitendo kilichonidhihirishia wazi kwamba hakuwa na u-seriousness wa kutaka kweli kumuondoa WM bali ni baadhi ya mawaziri, sema alichomeka tu hiyo kauli ili kutia presha zaidi!). Zaidi ya hapo, ninaamini hoja hiyo ni nzito na kimsingi, kwa sasa, imegeuka kuwa ni mchezo wa kisiasa na media na haitofika popote! Kama Mhe. Mbunge Zitto alikuwa na nia ya dhati ya kumuondoa WM asingekurupuka kiasi kile, angewashirikisha watu wengi zaidi, hususani wabunge wa CCM, na kimkakati zaidi angewapa wabunge wa CCM walioibua hoja hizo za kuwataka mawaziri wang'olewe na hapo angefanikisha malengo ya kumuondoa WM na serikali yake Bungeni. Kwa namna ilivyo hawezi kupata support ya wabunge wa CCM na kwa kuwa sisi ndiyo majority, hoja hiyo haitopita - na hii itaturudisha kule kule kwenye nilichokisema kule twitter kwamba hoja hii ni ......politically right but technically flawed!

Jamani, hoja ya kumuondoa WM madarakani siyo kitu kidogo, siyo kitu cha mchezo, ni lazima ujipange. Ukweli ni kwamba rafiki yangu Mhe. Zitto hakujipanga kuifanikisha (bila shaka yeye mwenyewe analielewa hili vizuri - he is smarter than this, I know him!)

Tatu, msisahau kitu kimoja cha muhimu kabisa. Kwamba, mimi ni Mbunge kutokea CCM na kama walivyo wengi wenzangu hatukusaini kwa sababu hatuwezi kuiangusha serikali ya CCM kwa hoja inayoletwa na Mbunge wa Kambi ya Upinzani! Mbunge wa Chama Tawala kuamua kuiangusha serikali ya chama chako ni sawa na kuamua kukata tawi la mti uliokalia, kwa vyovyote vile utaanguka nalo! Simple logic! Mfumo wa Bunge letu ni wa Westminster, na hivyo kuna kambi ya Upinzani (yenye interest ya kutaka kuiangusha serikali inayotawala) na Kambi ya Serikali (ambayo ina interest ya kutaka kuilinda serikali yake). Kwa maana hiyo sisi wabunge wa CCM tuna jukumu la kuilinda Serikali inayopatikana kutokana na sisi kuwa majority. Serikali ni lazima i-enjoy majority status ndani ya Bunge ili nchi itawalike kwa amani na utulivu, japokuwa haimaanishi kuruhusu ubadhirifu na ndiyo maana kwenye Party Caucus wabunge wana nguvu na fursa ya kusema chochote dhidi ya serikali ya Chama Chao. Kuna wengine wanataka Bunge liwe Bunge huru (ama 'An Indipendent Power House') disregarding political opinions/inclinations/affiliations na serikali iwe serikali, hii haiwezekani kwa katiba tuliyonayo leo. Tubadilishieni kwanza katiba na mfumo wa kufanya kazi ndipo mtutake tufanye hayo mnayoyatamani.

Nadhani nimejiweka wazi bila unafiki, sasa tujadili kwa hoja siyo kwa hisia na matusi kama hatukwenda shule vile.

Wakatabahu,
HK.
 
Ndugu zangu nimefurahishwa na huyumchumiatumbo niwazisasa ccm itakufa hivikaribuni je huyuakipewauwazili atatusaidianini sawanamakamba nawenginewote ndani ya ccm nivigumu kupata mtumwenyemasilahi ya taifa siyoolesendeka wala yeyote yule maanahuwezi ukavumilia uchafu unaofanywa ccm kama epa, richimondi,maliasiri,bandari,wizara ya fedha,luzuku,mbolea, nawizi mwingine eti ukawamlinzi wamasirahi ya taifa.ndiyomaana nasema ccm niwachumia tumbo na sijui kamakuna msafi ielewekehivi hakuna msafianayeishi na kulia chooni ni wanafiki wakubwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Huyu jamaa anatafuta nafasi kwenye baraza jipya hana lolote,
Jamani, kama anatafuta uwaziri kwenye baraza jipya tumuombee apate, kwani hamuoni kuwa ile biashara ya viungo vya albino imepungua sana tokea Mheshimiwa aukwae Uheshimiwa?
 
Bila shaka biashara unayotufahamisha hapa kwamba umeianzisha from nothing lakini sasa imesimama ni MSK solutions Ltd, kwani ndiyo kampuni ikliyosimama kwa kuwadhulumu wakulima wa pamba pamoja na kujipatia fungu la stimulus package kimagumashi. Biashara halali uliyofanya ni ya saloon na tax labda utuambie hizo bado zimesimama?

Unajisifia kwa kuwaibia watanzania masikini, unajisifia kwa kuwaibia wapiga kura wako, unajisifia kwa kuwaibia wananzengo wenzako, wewe ni hasara kwa wananzega na taifa kwa ujumla.

Hata kama ukiandika thesis ya PhD tano lakini kama akili yako ndio hii haitakusaidia chochote wewe mwenyewe wala taifa zaidi ya kuwa mnafiki na mwizi wa rasilimali za watanzania.
ukiona mtu anasifia elimu aliyonayo kuna walakini ndani ya ubongo wake, HK ana matatizo makubwa si kidogo.
 
Mzee Mwanakijiji,
Ni sheria gani inayoelekeza kwamba wabunge wakipiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu na kura zikakidhi mahitaji ya kikanuni ili kumng'oa waziri mkuu Raisi atawajibika kulivunja bunge?

Okhoreeeeeeeee bhuya tata!!!kho bhuhene tukalatuna sana M/kijiji "Kura ya kutokuwa na Imani na Waziri Mkuu ni dhidi ya Rais na Chama tawala" Nkamutebya iga agambe ghayo akogamba lakini reno la Waziri Mkuu ghatiba itana longolongo ohoo buswahili bhuyo akughamba.Niighaa Waziri Mkuu ano aratemerwe ikura aruho na ararwe atighe Rais atune ohonde kuikarhaa ko gitumbe kiyo.Gu gisungu ndagamba iga sank u bere machi for sati brillianti question NI SHERIA GANI?
 
Yawezekana ulivoandika na kujibu hoja ulijiona iko sahihi sana kumbe haukuwa hivo,umeweka wazi hisia zako juu ya chama kuliko wananchi,kutokana na maelezo yako huko radhi kuona chama kinapanga mikakati ya kumuangamiza mwananchi na ukakaa kimya,umeshindwa kuelewa kwamba ww ni mwakilishi wa wananchi lakini ni mfuasi wa chama umeshindwa kukumbuka kwamba waliokuweka madarakani ni wananchi na wala vyo chama chako kwanini tunakuwa wachiyo wa fadhila kiasi hiki,kwa hiyo baya likifanywa na serikali yako linakuwa zuri kwa sababu limefanywa na serikali ya chama cha mapinduzi,kwanini tunashindwa kuwa na fikra na mtazamo huru kwanini tunashindwa kusimamia kilicho sahihi,eti tusingeunga mkono hoja na wala hoja isingepita sababu sisi ndo wengi bungeni shame on u unadhihilisha ni kwa jinc gani hoja mnapitisha kwa ushabiki
 
"wengi wenzangu hatukusaini kwa sababu hatuwezi kuiangusha serikali ya CCM kwa hoja inayoletwa na Mbunge wa Kambi ya Upinzani!"

....yaani dokta, unategemea kauli kama hii isipandishe watu jazba? Kwamba ishu kwako si hoja bali chama, inadhihirisha hata zile kelele za madini jimboni kwako hazikuongozwa na what is ultimately JUST, bali maslahi. We na wenye mawazo km haya ni WABAYA kuliko kina Mkulo na RA. Maana ndio mnawapa viburi kufanya ufedhuli wakijua the Majority will not let them down.

Kwa mnaimtetea, incl. Mzee Mwanakijiji, kwani kuna kipi kipya alichosema tusichotegemea mwanaCCM butu yeyote asingesema? Tofauti ya PHD na elimu ya Saba has to show lots of differences folks!
 
Mi nadhani angekaa kimya tu,kuliko kuweka uwezo wake wa kufikiri uchi.kama kusoma ndio huko kazi bado ipo,maana hawa ndio wasomi wetu.
 
Duh kweli wanasema kua uyaone!!
Kama huu ndo uwezo wa kufikiri wa viongozi tulionao tutarajie nini wanapopewa dhamana ya kufanya maamuzi kwa maslahi ya taifa?Yaani mtu ambaye hata hajitambui kia kili leo anapewa zawadi ya ubunge na bado hataki kuficha upoyoyo wake anakuja kutetea madudu!!

Huyu ni mnafiki mkubwa kutokana na definition yake mwenyewe!!Hivi majuzi tu aliipinga serikali yake wakati wa mgomo wa madaktari kwa kuwaunga mkono leo hii anasema hawezi kuiangusha serikali ya chama chake na ni huyu huyu anatakwa tuendelee kumwamini.Kesho akipewa uwaziri unatarajia nini toka kwake?Takataka
 
A stupid msomi, tungetegemea wasomi walikombo taifa kumbe mnalikumbatia, CCM kifo kimefika sasa, Tunangoa na mti uliopanda stupid doctor
 
We jamaa ovyo kabisa
Huu utetezi wako haujakaa sawa.
Naomba hata rais asikuteue kuwa waziri umesha onyesha wazi wazi huwezi kazi na huwezi tetea wanyonge.

Hawa ndio CCM wanawapenda na ndio wanaoteuliwa. ukiwa mtetezi wa wanyonge utakaa bench mpaka ukome,
 
Back
Top Bottom