Majibu ya Kigwangalla: Kwa Nini Sikusaini Hoja ya Mhe. Zitto Zuberi Kabwe (MB)!

Hongera kwa kuingia kwenye baraza la mawaziri! Umetumia technic ya kutosaliti chama chako. Ila chama chako ndio kimepelekea yote haya, yaani ule msemo wa 'maisha bora kwa kila mtanzania' unaenda vice versa na hata mtu asiye na elimu ya msingi analitambua huku mkitulazimasha tuamini vinginevyo kwa matakwimu yenu ya macro-economics.
Anyway, jua tu idadi ya wajinga inapungua, na siasa za kupelekwapelekwa zinafika mwisho! We r watching you.
Hoja ya Zitto hata watoto wanaosoma uraia shule ya msingi waliilewa. Wabunge wanauwezo wa kumwajibisha waziri mkuu (hata kwa kosa la waziri wake), au ulitaka waendelee kulalamikalalamika kama vikao vingine vya bunge na baadae yaishie kwenye record za bunge!? Kwani tuhuma za ufisadi na udhaifu wa mawaziri zimeanza kikao kilichopita!?
One more step was needed honorable and Zitto showed the way.

Big UP mkuu, umemjibu ipasavyo. Alitaka wabunge walalame tuuu halafu iwekwe kapuni. Hakika mwisho wao waja, na kitambo si kirefu tutawahukumu kwa maovu yao juu ya nchi na wananchi. People are getting smarter each and every second gone by.
 
mnafiki tu ww ishia huko, umesahau issue ya madaktari nusura ikutoe kwenye chama! umepigwa mkwara na wanakuangalia ukirudia kupayuka payuka wana kupiga chini ndio maana unajitia kujenga hoja ya kuwa mawaziri watano na sio waziri mkuu, sasa kama ww mbunge unauwezo gani wa kuwangoa hao mawaziri? idiot ulikariri shule nini?

wasomi wa kibongo hawa duh! ww nyamaza kuwa kama wenzio wa viti maalumu upige makofi bungeni siku zako ziende, umesahau ulivyotuandikia kwenye ukurasa wako wa facebook. hii nchi yetu haiwezi kuendelea tukiwa tunavichwa kama vyako na wenzio akina lusinde.
 
Mh.K,naomba nikuulize japo haihusu unamjua mbunge wangu anaitwa Sereweji? je kunautaratibu gani wakuzungumza hadi yeye ankuwa azungumzi tangu kachaguliwa huku unguja?plz naomba unisaidie kwa hili.
 
kikao gani hicho? Kwa mara ya kwanza leo ndiyo nasikia kutoka kwako. Huwa sichangii changii kwanza kwenye vikao na nikichangia huwa na-impress! (blowing my own trumpet!) na sasa hivi naandika PhD thesis ya maana na imejaa nondo za ukweli, na pia ninaandika kitabu, na nilipo hapa nimeanzisha biashara from nothing na leo imesimama...sitaki kujua na wewe una nini cha kuonesha katika maisha yako yenye 'maturity'...acha dharau brother! Hunijui vizuri, achana na mimi.

Bila shaka biashara unayotufahamisha hapa kwamba umeianzisha from nothing lakini sasa imesimama ni MSK solutions Ltd, kwani ndiyo kampuni ikliyosimama kwa kuwadhulumu wakulima wa pamba pamoja na kujipatia fungu la stimulus package kimagumashi. Biashara halali uliyofanya ni ya saloon na tax labda utuambie hizo bado zimesimama?

Unajisifia kwa kuwaibia watanzania masikini, unajisifia kwa kuwaibia wapiga kura wako, unajisifia kwa kuwaibia wananzengo wenzako, wewe ni hasara kwa wananzega na taifa kwa ujumla.

Hata kama ukiandika thesis ya PhD tano lakini kama akili yako ndio hii haitakusaidia chochote wewe mwenyewe wala taifa zaidi ya kuwa mnafiki na mwizi wa rasilimali za watanzania.
 
Hivi wewe Dr umelogwa? Sasa umekuja kujitetea nini hapa zaidi ya kumwaga pumba?Najua ulikuwa unamuogopa Hawa Ghasia mana kipindi cha mgomo wa madaktar ulipigwa za uso ukakaa kmya bado kidogo ungevuliwa ubunge. Kutokana na kuwa kigeugeu usitegemee kurud tena bungeni 2015. We endelea kujichekesha na kujipendekeza kwa Jk ili angalau aukupe uwaziri wa watoto jinsia na Wanawake. MERDE
 
Halafu nyie!! Mie Mwenzenu nimistuka! Nilidhani ni Dr aliyekokotoa shule kumbe ni Dokta wa MITISHAMBA! .. Tumemsikia, tumemwelewa Na tutatumia maneno Haya Haya kuwapelekea wana Mbokandogo(Nzega).. Wahukumu.
 
Mzee Mwanakijiji,
Ni sheria gani inayoelekeza kwamba wabunge wakipiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu na kura zikakidhi mahitaji ya kikanuni ili kumng'oa waziri mkuu Raisi atawajibika kulivunja bunge?
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Hoja ni kusaini kwa ajili ya kukidhi matakwa za kanuni za Bunge ambalo lilimptisha waziri mkuu. Mawaziri walichaguliwa na Rais ndiye madaraka ya kuwawajibisha.

Inatia shaka uwakilishi wako, ni hakika si wa wananchi bali ni wawaliokuupa uwakilishi (CCM). Ukishakula nyama ya mtu huachi inaleta maana kwako inadhirisha kuwa omezoea kutafuta kwa gharama yo yote hata kwa ghilba; nina shaka kama dini ya kiislam unaielewa au unaiimba kama kasuku.

Haya wenzio wabunge wa CCM NEC wameitekeleza hoja ya zitto kwa vitendo na Rais anaitekeleza kabla haijawasilishwa mezani bungeni wewe upo wapi?

Misifa ya elimu ya vyeti vingi kichwani hamnazo. Hata Lusinde anakushinda

KWELI CCM NI KOKOLO
 


Tatu, msisahau kitu kimoja cha muhimu kabisa. Kwamba, mimi ni Mbunge kutokea CCM na kama walivyo wengi wenzangu hatukusaini kwa sababu hatuwezi kuiangusha serikali ya CCM kwa hoja inayoletwa na Mbunge wa Kambi ya Upinzani! Mbunge wa Chama Tawala kuamua kuiangusha serikali ya chama chako ni sawa na kuamua kukata tawi la mti uliokalia,


hapo kwenye RED that is very low from MD holder, bora ulivyokimbilia siasa hospital ungekuwa watoa Wrong diagnosis daily... hivi inamaana upo hapo mjengoni kuwakilisha chama na si wananchi..! ?! nilitegemea kijana kama wewe utakuwa mstari wa mbele kusaficha chama chetu tawala.. vijana wa CCM hebu muigeni malema
 
Nadhani nimejiweka wazi bila unafiki,

Kweli umejiweka wazi bila unafiki kuwa wewe unapigania maslahi yako na unapigania kile unachotaka wewe na nafsi yako na sio hata wale waliokuchagua
Wale waliokuchagua hawajakutuma kuwa mkalindane na mkalinde serikali ya chama chenu mtakapoona mambo hayaendi the way mnavyotaka
Kweli wewe sio mnafiki


Mkuu unimenichekesha sana lol! umempa vizuri huyu kijana(Mb).
 
Ndugu zangu wanabodi,

Nimeamua kuja kujibu kama ambavyo mngependa nifanye. Mimi sijawahi kuwa mnafiki, at least kwa alama tatu za mnafiki kama tunavyofundishwa sisi waislamu. Kwa faida ya mjadala huu, niseme alama zenyewe. Moja ni kuwa akitoa ahadi hatekelezi. Mbili, ni akiaminiwa anahalifu na tatu, akizungumza husema uongo. Namshukuru Mungu sina hata moja ya alama hizi na hivyo kushindwa mtihani wa kuwa 'mnafiki'. Ungeniita mnafiki kama nisingekuwa tayari kutoa maelezo ya maamuzi yangu, ama kama ningewasaliti CCM na kupeleka siri za huku kule, ama kama ningeahidi kuunga mkono hoja hiyo kisha nikakimbia. Leo hii mimi niko chama kimoja tu, CCM, na nitafanya mambo yanayokubalika ndani ya CCM. Siku nikihamia CHADEMA/CUF/NCCR basi nitafanya ya huko bila kusaliti kule na kurudisha CCM ama kupeleka kokote kule kinyume na utaratibu. Huo ndiyo msimamo wa ukweli na siyo unafiki.
.....Jamani toka kule kwenye Mada yenyewe niliwaambia kuwa huyu jamaa ana kesi ya kujibu Mahakama ya Wilaya Ya Nzega kwahiyo hawezi kuchangia kuchangia la maana badala ya kusubiri hukumu yake.

 
- Mheshimiwa Dr. Hamis, this is great, umekuja hapa JF na kuweka msimamo wako na kutetea bila woga wala kubabaika, sasa ni kukubali kutokubaliana na ni matumaini yangu in the future utakuja tena, na muhimu wafahamishe huko mjengoni kwamba wanakaribishwa wote hapa kuja kusimamia misimamo yao,

- Yaaani ninaheshimu uamuzi wako wa kuja hapa to the point kwamba nimeamua kutoichambua kabisa post yako, zaidi tu ya kukuombea UBARIKIWE!

William.

You are wrong Lemtuz! anatakiwa kusimama kwa miguu yake yote miwili na kuwatetea wananchi walomchagua na si madudu yanayofanywa na serikali kupitia mgongo wa chama chake.
 
Sikutegemea kama ungeleta pumba kama hizi,ni bora ungekaa kimya tu ona sasa ulivyoharibu hali ya hewa,
Wewe ni mnafiki period.
 
Operasheni Amka Nzega ilimshinda leo hilo la Zito, hana lolote ndio Maana hajibu chochote
 
Kigwangala, busara au ujinga wa mtu hujionesha pale atakapoongea/andika kupresent fikra zake. Sifikiri kama ulitumia muda mwingi kuruhusu kichwa yako kufikiri maana kilichomo katika maelezo yako na wakati tuliopo havishabihiani. Huwezi kutetea wezi hata kama wanatoka katika familia yako; huwezi kutetea mtu mmja anayeuwa mamilioni ya watu kwa kusababisha uchumi kuwa mbaya/umasikini hata kama muhusika anatoka ndani kwako. Kumbuka una jukumu la kuwawakilisha wananchi katika jimbo lako ambao wanahitaji maendeleo. Ukifikiri kiundani sana Zitto japo amekibomoa CCM lakini hapo 2015 mkichanga karata zenu vizuri mnaweza kubaki na japo wabunge kadhaa otherwise itakuwa ni mbaya zaidi. Naamini wewe ni kijana usiburutwe na wazee wa CCM wana muda mfupi waliobakisha kulitumikia taifa hili, tumia muda huu kupingana nao kwa ujenzi wa Chama. Unakubali kwamba kuna mawaziri wameboronga lakini unatetea waziri mkuu ambaye ni mkuu wao asiwajibike kwa kutowawajibisha wahusika unatufunza nini? tukuchukie? Bro next time usifanye maamuzi ya namna hiyo jifunze hata katika nchi zilizoendelea namna wabunge ndani ya chama kimoja wanavyounga hoja za chama kingine cha upinzania bila kuogopa so long as ni kwa maslahi ya nchi. Nafikiri hata katika Baraza jipya la mawaziri haufai bro japo kuwa JK huwa hana maono aweza kukuchagua, Ukichaguliwa good luck lakini ukatende kazi na kuacha mawazo potofu tekeleza hata mawazo ya wapinzani kama yanajenga. Kwa maendeleo ya jimbo lako shirikiana na wapinzani na utumie hoja zao nzuri katika ujenzi wa taifa. Tunaumia sana bro kusikia hoja dhaifu kutoka kwa msomi kama wewe japo kuwa kudesa napo kupo mashuleni huko. Good luck bra
Ndugu zangu wanabodi,

Nimeamua kuja kujibu kama ambavyo mngependa nifanye. Siyo kwamba nimekimbia JF, la hasha. Siwezi kukimbia na wala sina sababu ya kufanya hivyo. Ni kwamba gadget yangu ninayotumia kwa mawasiliano ilipata mushkeri na nikawa nalazimika kutumia kompyuta na bahati mbaya sana kwa jinsi nilivyokuwa bize na ujenzi wa Taifa nilijikuta nakosa muda wa kukaa kuanza ku-surf. Nisamehewe kwa hilo.

Mimi sijawahi kuwa mnafiki, at least kwa alama tatu za mnafiki kama tunavyofundishwa sisi waislamu. Kwa faida ya mjadala huu, niseme alama zenyewe. Moja ni kuwa akitoa ahadi hatekelezi. Mbili, ni akiaminiwa anahalifu na tatu, akizungumza husema uongo. Namshukuru Mungu sina hata moja ya alama hizi na hivyo kushindwa mtihani wa kuwa 'mnafiki'. Ungeniita mnafiki kama nisingekuwa tayari kutoa maelezo ya maamuzi yangu, ama kama ningewasaliti CCM na kupeleka siri za huku kule, ama kama ningeahidi kuunga mkono hoja hiyo kisha nikakimbia. Leo hii mimi niko chama kimoja tu, CCM, na nitafanya mambo yanayokubalika ndani ya CCM. Siku nikihamia CHADEMA/CUF/NCCR basi nitafanya ya huko bila kusaliti kule na kurudisha CCM ama kupeleka kokote kule kinyume na utaratibu. Huo ndiyo msimamo wa ukweli na siyo unafiki.

Kuna uwezekano wa kuwa na tafsiri tofauti kutokana na pre-conceptions zetu vichwani, siwezi kulizuia hilo hata kidogo. Kwa kuwa ninakalia kiti cha uwakilishi, nina-feel ninawajibika kwenu kutoa maelezo ya msimamo wangu kwenye hili, na wala sintomumunya maneno.

Kwanza, hoja yenyewe siikubali. Kwa sababu ninaamini serikali ya Chama Changu (CCM) haijashindwa kufanya kazi ya watanzania kiasi cha kung'olewa madarakani kwa namna hiyo. Pili, naamini na ninakubali, na kwa hakika ninakerwa na baadhi ya watu waliopewa dhamana za kuongoza baadhi ya ofisi nyeti za umma wametuangusha watanzania, na hivyo naunga mkono hoja ya kutaka kuwatoa hawa. Mhe. Zitto Kabwe (MB) alipokuwa akijumuisha hoja yake, alitaka serikali iwawajibishe baadhi ya mawaziri na watendaji wakuu wa Wizara na Mashirika ya umma, na akasema kama serikali haikufanya hivyo kufikia J3 iliyofuata basi sisi (Bunge) tuna uwezo na WM na kwamba atapitisha karatasi ya kukusanyia saini 70 ili kukidhi matakwa ya kikanuni ya kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na WM; kwa tafsiri yangu ni kwamba Mhe. Mbunge alilenga kuweka presha kwa serikali, kuitaka iwajibike kwa kuwawajibisha mawaziri hao (watano) kama alivyowataja yeye. Kwanza mwanzoni nilielewa hivyo. Baadaye jinsi ilivyopokelewa na wadau mbalimbali nikaona kama hoja inahama sasa na kwamba si mawaziri hao watano wenye tuhuma mbalimbali, ni PM na kwa maana hiyo ni serikali yote Bungeni! Hili mimi siliungi mkono na silikubali. Nasema wazi hivyo kwa sababu, mimi nina imani na WM, nina imani na Rais - aliyemchagua WM, na nina imani na Mawaziri wengine wengi wazuri tu kwenye serikali hii, na msimamo wangu huu uko wazi sana tu.

Mbili, sioni sababu ya kuiingiza nchi kwenye wasiwasi wa kiutawala kiasi hiki. Na kwa kuwa wabunge wa CCM kwenye party caucus tulikuwa tayari tumeishaambiwa kwamba kuna mawaziri wameamua kujiuzulu wenyewe (tena siyo wale watano, ni wanane kabisa) kutokana na tuhuma hizo na presha kutoka kwa wabunge wa CCM na wengine, sikuona sababu ya mimi kusaini hoja ya Zitto (ambayo kikanuni ilikuwa imekosewa - kitendo kilichonidhihirishia wazi kwamba hakuwa na u-seriousness wa kutaka kweli kumuondoa WM bali ni baadhi ya mawaziri, sema alichomeka tu hiyo kauli ili kutia presha zaidi!). Zaidi ya hapo, ninaamini hoja hiyo ni nzito na kimsingi, kwa sasa, imegeuka kuwa ni mchezo wa kisiasa na media na haitofika popote! Kama Mhe. Mbunge Zitto alikuwa na nia ya dhati ya kumuondoa WM asingekurupuka kiasi kile, angewashirikisha watu wengi zaidi, hususani wabunge wa CCM, na kimkakati zaidi angewapa wabunge wa CCM walioibua hoja hizo za kuwataka mawaziri wang'olewe na hapo angefanikisha malengo ya kumuondoa WM na serikali yake Bungeni. Kwa namna ilivyo hawezi kupata support ya wabunge wa CCM na kwa kuwa sisi ndiyo majority, hoja hiyo haitopita - na hii itaturudisha kule kule kwenye nilichokisema kule twitter kwamba hoja hii ni ......politically right but technically flawed!

Jamani, hoja ya kumuondoa WM madarakani siyo kitu kidogo, siyo kitu cha mchezo, ni lazima ujipange. Ukweli ni kwamba rafiki yangu Mhe. Zitto hakujipanga kuifanikisha (bila shaka yeye mwenyewe analielewa hili vizuri - he is smarter than this, I know him!)

Tatu, msisahau kitu kimoja cha muhimu kabisa. Kwamba, mimi ni Mbunge kutokea CCM na kama walivyo wengi wenzangu hatukusaini kwa sababu hatuwezi kuiangusha serikali ya CCM kwa hoja inayoletwa na Mbunge wa Kambi ya Upinzani! Mbunge wa Chama Tawala kuamua kuiangusha serikali ya chama chako ni sawa na kuamua kukata tawi la mti uliokalia, kwa vyovyote vile utaanguka nalo! Simple logic! Mfumo wa Bunge letu ni wa Westminster, na hivyo kuna kambi ya Upinzani (yenye interest ya kutaka kuiangusha serikali inayotawala) na Kambi ya Serikali (ambayo ina interest ya kutaka kuilinda serikali yake). Kwa maana hiyo sisi wabunge wa CCM tuna jukumu la kuilinda Serikali inayopatikana kutokana na sisi kuwa majority. Serikali ni lazima i-enjoy majority status ndani ya Bunge ili nchi itawalike kwa amani na utulivu, japokuwa haimaanishi kuruhusu ubadhirifu na ndiyo maana kwenye Party Caucus wabunge wana nguvu na fursa ya kusema chochote dhidi ya serikali ya Chama Chao. Kuna wengine wanataka Bunge liwe Bunge huru (ama 'An Indipendent Power House') disregarding political opinions/inclinations/affiliations na serikali iwe serikali, hii haiwezekani kwa katiba tuliyonayo leo. Tubadilishieni kwanza katiba na mfumo wa kufanya kazi ndipo mtutake tufanye hayo mnayoyatamani.

Nadhani nimejiweka wazi bila unafiki, sasa tujadili kwa hoja siyo kwa hisia na matusi kama hatukwenda shule vile.

Wakatabahu,
HK.
 
Back
Top Bottom