Majibu ya Kigwangalla: Ama kweli masikini akipata...

Majibu ya Kigwangalla: Ama kweli masikini akipata...

Azarel

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2016
Posts
29,020
Reaction score
40,846
Habarini Wadau,

Ni Ukweli na Uwazi kuwa watumishi wengi wa serikali, hasa wale walioitumikia serikali kwa miaka mingi wapo katika simanzi kutokana na tamko lililotoka serikalini kuhusu mafao yao.

Mtu ambaye alitegemea kupata asilimia zote za akiba yake aliyoweka na kuwekewa kila mwezi tangu aajiriwe leo hii anapewa 25% pekee na kisha kudunduliziwa visenti vidogo kila mwezi.

Hiyo kwangu naona ni unyanyasaji mkubwa kwa watumishi hawa.

LAKINI PIA, nimeona comment ya Mh. Hamisi Kigwangala ninayoiita ni DHIHAKA, au DHARAU na KEBEHI kubwa kwa watumishi hawa kwa kuwaambia kuwa kama walitaka akiba si wangehifadhi pesa zao wenyewe kisha waje kutumia uzeeni.

Hayo sio maneno ya busara hata kidogo.

Hamisi Kigwangala anasahau yeye alipotoka. Anatamka kana kwamba yeye alizaliwa mahala penye neema tu na hajui shida.

IMG-20181201-WA0001.jpeg
 
Dr. Hamis Kigwangala ajitathmini na tweets zake (read matamshi yake) ambayo huwa yanamrudi vibaya. kuna lile la maChoko na hili tena.
 
Wanajisahau hao na wakituchukulia sisi RAIA ni viumbe tusio na akili timamu. Wasubiri #2020 maneno yao yatawatokea puani safari hii.

Dr. Kigwangalla hana busara wala akili ya kupima uzito wa maneno yake, CHEO CHAKE hakiendani na akili yake, mtu anaandika na kuropoka anachojisikia tu bila kutafakari IMPACT yatakayo leta kwa jamii, ila wanasahau watarudi URAIANI soon, kuna watu wana akili na busara (Mfano Hussein Bashe huyu hua anasimamia hoja za wananchi wake hata kama CCM hawaendani nazo, mpaka kufikia hatua wananchi huko kwao wanamuita Rais Wa Nzega, hata CCM wakimpiga chini #2020 akiingia upinzani anachukua, jamaa ana hoja kali sana).

Mtu ana cheo na elimu ya DAKTARI, ila akili haina tofauti na mwanafunzi wa darasa la 7. Aibu gani hii.

Juu ya yote kuna wapumbavu hawana hata aibu kusema "Dr Kigwangalla ni Presidential type". Huyu??? Wa kupewa Urais??? Mungu atustiri na JANGA HILI wana Tanzania.[emoji53]

Waombe mungu sana JIWE atawale milele (Japo hana ubavu huo), ila atakapo achia ngazi basi watasimulia na kuimba segerea.[emoji53]
 
Huyu ndio Dr. Uchwara mwingine.
Wanajisahau hao na wakituchukulia sisi RAIA ni viumbe tusio na akili timamu. Wasubiri #2020 maneno yao yatawatokea puani safari hii.

Dr. Kigwangalla hana busara wala akili ya kupima uzito wa maneno yake, mtu anaandika na kuropoka anachojisikia tu, ila wanasahau watarudi URAIANIV soon, kuna watu wana akili na busara (Mfano Hussein Bashe).
 
Mkuu sio watumishi wote wa serikali ni CCM, usikariri hivyo.
Ni kweli Mkuu ila hawa watumishi wa serikai ndio walikua na nafasi kubwa sana kubadilisha maisha yetu, yaani wao wakiamua basi serikali haina ujanja, yaani wao wanapokonywa haki zao wanatazama tu, wanalizimishwa mambo ya mwenge na wao wanakubali eti kulinda kazi, kwa mshahara gani,? Mimi mwanangu yeyote hatokuja kuwa mtumishi wa umma hata siku moja, na siku akiwa basi mimi siyo baba yake na nitamuachia laana.
 
Wanajisahau hao na wakituchukulia sisi RAIA ni viumbe tusio na akili timamu. Wasubiri #2020 maneno yao yatawatokea puani safari hii.

Dr. Kigwangalla hana busara wala akili ya kupima uzito wa maneno yake, CHEO CHAKE hakiendani na akili yake, mtu anaandika na kuropoka anachojisikia tu bila kutafakari IMPACT yatakayo leta kwa jamii, ila wanasahau watarudi URAIANIV soon, kuna watu wana akili na busara (Mfano Hussein Bashe).

Mtu ana cheo na elimu ya DAKTARI, ila akili haina tofauti na mwanafunzi wa darasa la 7. Aibu gani hii.

Waombe mungu sana JIWE atawale milele (Japo hana ubavu huo), ila atakapo achia ngazi basi watasimulia na kuimba segerea.[emoji53]
Eti naye ni miongoni mwa wanao utaka urais wa nchi yangu. Kuachwa kwa watu kama jamii za vigwangala lazima taifa lihesabu hasara!
 
Amejisahau sana huyu docta fake, anadhani yupo ahela kumbe ni uwaziri tu anashindwa kujua uwaziri unapita tu
 
Eti naye ni miongoni mwa wanao utaka urais wa nchi yangu. Kuachwa kwa watu kama jamii za vigwangala lazima taifa lihesabu hasara!
Huyo alivyokua hana akili akipata urais anaweza akahamishia IKULU kwenda NZEGA VIJIJINI kwao, halafu bunge likawa TABORA.[emoji53]
 
Ni kweli Mkuu ila hawa watumishi wa serikai ndio walikua na nafasi kubwa sana kubadilisha maisha yetu, yaani wao wakiamua basi serikali haina ujanja, yaani wao wanapokonywa haki zao wanatazama tu, wanalizimishwa mambo ya mwenge na wao wanakubali eti kulinda kazi, kwa mshahara gani,? Mimi mwanangu yeyote hatokuja kuwa mtumishi wa umma hata siku moja, na siku akiwa basi mimi siyo baba yake na nitamuachia laana.
Hasa waalimu,ila niwaoga sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom