Kuhusu mifuko ya hifadhi ya jamii

Kuhusu mifuko ya hifadhi ya jamii

Technologiest

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2017
Posts
3,727
Reaction score
4,060
Habarini wanajamvi!
Wakubwa zangu shikamooni!

Nijikite kwenye hoja ya sheria/kanuni za namna ya kukokotoa mafao ya Watumishi wa serikali kitu kinachopelekea Watumishi ambao wanafikia ukomo wa ajira zao kupata malipo ya mkupuo wa 25% na kiasi cha 75%kinachobaki kulipwa kidogo kidogo kwa muda wa miaka 12.5 hii inamaana kuwa Mstaafu ikiwa atastaafu katika umri wa miaka 55 inamaana atanufaika mpaka anapofikisha miaka 67½ na kama atastaafu na miaka 60 atanufaika mpaka anapofikisha miaka 72½ kitu ambacho kitaleta maisha magumu sana kwa wazee wetu na Wastaafu watarajiwa.

Binafsi nauona huu mpango hauna nia njema ya kujali afya na maendeleo ya Wastaafu(wazee).Wastaafu wengi katika kipindi walichokua kazini walikuwa wakipoteza masaa mengi kutumika na serikali hivyo nguvu, muda na maarifa yao wamewekeza huko pia wanakabiliwa na majukumu mbalimbali kama kusomesha,wategemezi,kujiendeleza,nk. Kitu kilichowafanya kufanya kazi huku wakilipa mikopo mbalimbali kama ya kujiendelezea kitaaluma, kusomeshea watoto,kufanya shughuli ndogondogo za kiuchumi.

Hapa nasema shughuli ndogo ndogo kwakua hata mikopo wanayoipata ni midogo hivyo haiwezeshi kufanya miradi midogo midogo ambayo haiwafanyi kuwa na akiba za kutosha. Hata inafikia wakati wengine wanastaafu hawana nyumba ya maana ya kupumzikia,tegemeo lao ilikua ni akiba waliyojiwekea kwa kipindi chote wanafanya kazi kwa mpango ulioratibiwa na serikali kwa nia njema kabisa.

Lakini inapokuja sintofahamu kuwa haya malipo ambayo ni AKIBA ya Mtumishi huyu kwa miaka yote wala siyo MKOPO au MSAADA kutolewa robo tu kwa mkupuo siyo sawa nadhani turudi nyuma kidogo tuangalie wapi tumejikwaa badala ya kuangalia tulipodondokea. Tukizingatia hali ya maisha inavyobadilika kila siku, gharama za maisha, huduma mbalimbali zinapanda lakini mtumishi huyu anaestaafu leo anapokea ¼ ya pensheni yake ataenda kununua nyumba/kujenga wapi kwa gharama hizi zinazozidi kupanda kila leo? Kama haitoshi umri wa kuishi wa mtu huyu umepungua sana kisha tunamrudishia ¼tu ya pesa alizotupatia tumhifadhie, tunategemea kuwa na wazee siku za hapo mbeleni kweli??

Nilitegemea tungekuja na mpango mkakati madhubuti kuwa kwakua hawa watu wanatunza fedha zao kwetu kwa muda upatao miaka 25-35+ basi tuweke na riba kidogo hata kama ni 2% kwakua tunazifanyia biashara/Uwekezaji.Ama laa tumeshindwa kabisa tuwape mikopo mikubwa wafanye maendeleo mapema kabla hawajafika uzeeni ili tusijekua na kizazi cha wazee wategemezi, hohehahe wasiojiweza.Kama bado tunaiona ngumu basi kila Mtumishi pensheni yake mara anapoanza kazi ikatwe na kuwekwa moja kwa moja kwenye fixed account ya benki yake huko atapata walau faida ya kila mwaka pia atafaidika na michango yake aliyohifadhi. Mwisho, kinachotia simanzi zaidi hii sheria inataka mstaafu akifariki kabla ya miaka 12.5 watoto wake wachukue kwa niaba yake pesa ya kila mwezi kwa muda wa miaka mitatu(3) tu!

Hii haijakaa sawa, chondechonde tusianze kumtafuta mchawi baadae! Tutegemee ongezeko la wagonjwa wa akili, wizi, ufisadi na uzembe kazini kuongezeka.
Nawasilisha!
 
Hii hoja Tundu Lissu ameifafanua vizuri na Ndugai naye amejitetea kwa kadiri anavyoona. Tusubiri serikali tuone wanakaza shingo au wataona soo. Nia haikuwa nzuri hata kidogo.

Hii ni fursa ya wananchi kujua ni watu gani watetezi wao, na wepi ni wasaliti wao. Japo nathubutu kusema watawala wa nchi hii wana bahati nzuri, kwa sababu % kubwa ya wananchi ni wajinga (uelewa wao ni mdogo kuhusu haki zao).
 
Inahitaji moyo sana kuwa mwajiriwa ktk kipindi hiki... Ushauri wa wazi kwa wafanyakazi ni kuandaa mazingira bora ya kustaafu pasipo kutegemea mafao uliyowekeza ktk mifuko ya hifadhi. Tofauti na hapo ni kuumizana vichwa manake watawala wameshaamua. Hakuna namna
 
Mazingira Bora ya kustaafu atayaandaje ilhali hakuna posho wala annual increment? Hii Sheria Ni ya kulaaniwa
 
Kwa wale waliohusika na utungaji wa sheria hii, wasiposikia sauti za kilio cha watu kuhusu sheria hii na kufanya haraka KUIBATILISHA, Mungu ataamuru mawe yalie badala ya watu.

Hapo ndipo kila aliyehusika kwa namna moja au nyingine kutunga na kuridhia sheria hii atakapojutia maamuzi yake.
 
Hivi tatizo ni mini!?? Mbona taifa linakua katili kwa watumishi tulio masikini!??? Inastaajabisha sana kwakweli yani sijui ni upole kupita kiaso WA watz!??au nn!??,
 
Habarini wanajamvi!
Wakubwa zangu shikamooni!

Nijikite kwenye hoja ya sheria/kanuni za namna ya kukokotoa mafao ya Watumishi wa serikali kitu kinachopelekea Watumishi ambao wanafikia ukomo wa ajira zao kupata malipo ya mkupuo wa 25% na kiasi cha 75%kinachobaki kulipwa kidogo kidogo kwa muda wa miaka 12.5 hii inamaana kuwa Mstaafu ikiwa atastaafu katika umri wa miaka 55 inamaana atanufaika mpaka anapofikisha miaka 67½ na kama atastaafu na miaka 60 atanufaika mpaka anapofikisha miaka 72½ kitu ambacho kitaleta maisha magumu sana kwa wazee wetu na Wastaafu watarajiwa.
Binafsi nauona huu mpango hauna nia njema ya kujali afya na maendeleo ya Wastaafu(wazee).Wastaafu wengi katika kipindi walichokua kazini walikuwa wakipoteza masaa mengi kutumika na serikali hivyo nguvu, muda na maarifa yao wamewekeza huko pia wanakabiliwa na majukumu mbalimbali kama kusomesha,wategemezi,kujiendeleza,nk. Kitu kilichowafanya kufanya kazi huku wakilipa mikopo mbalimbali kama ya kujiendelezea kitaaluma, kusomeshea watoto,kufanya shughuli ndogondogo za kiuchumi.Hapa nasema shughuli ndogo ndogo kwakua hata mikopo wanayoipata ni midogo hivyo haiwezeshi kufanya miradi midogo midogo ambayo haiwafanyi kuwa na akiba za kutosha. Hata inafikia wakati wengine wanastaafu hawana nyumba ya maana ya kupumzikia,tegemeo lao ilikua ni akiba waliyojiwekea kwa kipindi chote wanafanya kazi kwa mpango ulioratibiwa na serikali kwa nia njema kabisa.
Lakini inapokuja sintofahamu kuwa haya malipo ambayo ni AKIBA ya Mtumishi huyu kwa miaka yote wala siyo MKOPO au MSAADA kutolewa robo tu kwa mkupuo siyo sawa nadhani turudi nyuma kidogo tuangalie wapi tumejikwaa badala ya kuangalia tulipodondokea. Tukizingatia hali ya maisha inavyobadilika kila siku, gharama za maisha, huduma mbalimbali zinapanda lakini mtumishi huyu anaestaafu leo anapokea ¼ ya pensheni yake ataenda kununua nyumba/kujenga wapi kwa gharama hizi zinazozidi kupanda kila leo? Kama haitoshi umri wa kuishi wa mtu huyu umepungua sana kisha tunamrudishia ¼tu ya pesa alizotupatia tumhifadhie, tunategemea kuwa na wazee siku za hapo mbeleni kweli?? Nilitegemea tungekuja na mpango mkakati madhubuti kuwa kwakua hawa watu wanatunza fedha zao kwetu kwa muda upatao miaka 25-35+ basi tuweke na riba kidogo hata kama ni 2% kwakua tunazifanyia biashara/Uwekezaji.Ama laa tumeshindwa kabisa tuwape mikopo mikubwa wafanye maendeleo mapema kabla hawajafika uzeeni ili tusijekua na kizazi cha wazee wategemezi, hohehahe wasiojiweza.Kama bado tunaiona ngumu basi kila Mtumishi pensheni yake mara anapoanza kazi ikatwe na kuwekwa moja kwa moja kwenye fixed account ya benki yake huko atapata walau faida ya kila mwaka pia atafaidika na michango yake aliyohifadhi. Mwisho, kinachotia simanzi zaidi hii sheria inataka mstaafu akifariki kabla ya miaka 12.5 watoto wake wachukue kwa niaba yake pesa ya kila mwezi kwa muda wa miaka mitatu(3) tu!
Hii haijakaa sawa, chondechonde tusianze kumtafuta mchawi baadae! Tutegemee ongezeko la wagonjwa wa akili, wizi, ufisadi na uzembe kazini kuongezeka.
Nawasilisha!
Kweli kabisa Naunga mkono hoja asilimia mia moja. Hapa wawakilishi wetu bungeni ndiyo wa kulaumiwa' kwa nini wanakubali hizi kanuni kandamizi ambazo hazina tija kwa wastaafu? Hii inaonyesha jinsi gani wabunge wasivyo kuwa makini na sheria pamoja kanuni zizopitishwa kwenye chombo hicho! Labda zinapokuwa zinahusu masilahi yao tu! Mbona wao wabunge wakistaafu wanalipwa kiinua mgongo chao chote, tena bila masharti? Tunataka na wafanyakazi nao iwe hivyo hivyo mfanyakazi akiacha kazi apewe stahiki zake zote, bila kupangiwa masharti.
 
Hapa hutamwona Bashe, Kigwangala wala Makamba wanaojidaigi wanahuruma na wananchi wakitetea wananchi kuhusu haya mafao
 
Inahitaji moyo sana kuwa mwajiriwa ktk kipindi hiki... Ushauri wa wazi kwa wafanyakazi ni kuandaa mazingira bora ya kustaafu pasipo kutegemea mafao uliyowekeza ktk mifuko ya hifadhi. Tofauti na hapo ni kuumizana vichwa manake watawala wameshaamua. Hakuna namna
Hata kama mfanyakazi atajiandalia mazingira mazuri baada ya kustaafu bado mafao yake ni haki yake lazima ayapiganie. Haya mambo ya kusema sijui jiandae, mara eti usitegemee mshahara ni namnamna ya kupumbaza watu wasione umuhimu wa kudai mafao stahili. Duniani kuna mgawanyo wa kazi , kuna wafanyabiashara, wafanyakazi (waajiriwa),na wajisiliamali so kila kundi lina umuhimu wake.
 
Habarini wanajamvi!
Wakubwa zangu shikamooni!

Nijikite kwenye hoja ya sheria/kanuni za namna ya kukokotoa mafao ya Watumishi wa serikali kitu kinachopelekea Watumishi ambao wanafikia ukomo wa ajira zao kupata malipo ya mkupuo wa 25% na kiasi cha 75%kinachobaki kulipwa kidogo kidogo kwa muda wa miaka 12.5 hii inamaana kuwa Mstaafu ikiwa atastaafu katika umri wa miaka 55 inamaana atanufaika mpaka anapofikisha miaka 67½ na kama atastaafu na miaka 60 atanufaika mpaka anapofikisha miaka 72½ kitu ambacho kitaleta maisha magumu sana kwa wazee wetu na Wastaafu watarajiwa.
Binafsi nauona huu mpango hauna nia njema ya kujali afya na maendeleo ya Wastaafu(wazee).Wastaafu wengi katika kipindi walichokua kazini walikuwa wakipoteza masaa mengi kutumika na serikali hivyo nguvu, muda na maarifa yao wamewekeza huko pia wanakabiliwa na majukumu mbalimbali kama kusomesha,wategemezi,kujiendeleza,nk. Kitu kilichowafanya kufanya kazi huku wakilipa mikopo mbalimbali kama ya kujiendelezea kitaaluma, kusomeshea watoto,kufanya shughuli ndogondogo za kiuchumi.Hapa nasema shughuli ndogo ndogo kwakua hata mikopo wanayoipata ni midogo hivyo haiwezeshi kufanya miradi midogo midogo ambayo haiwafanyi kuwa na akiba za kutosha. Hata inafikia wakati wengine wanastaafu hawana nyumba ya maana ya kupumzikia,tegemeo lao ilikua ni akiba waliyojiwekea kwa kipindi chote wanafanya kazi kwa mpango ulioratibiwa na serikali kwa nia njema kabisa.
Lakini inapokuja sintofahamu kuwa haya malipo ambayo ni AKIBA ya Mtumishi huyu kwa miaka yote wala siyo MKOPO au MSAADA kutolewa robo tu kwa mkupuo siyo sawa nadhani turudi nyuma kidogo tuangalie wapi tumejikwaa badala ya kuangalia tulipodondokea. Tukizingatia hali ya maisha inavyobadilika kila siku, gharama za maisha, huduma mbalimbali zinapanda lakini mtumishi huyu anaestaafu leo anapokea ¼ ya pensheni yake ataenda kununua nyumba/kujenga wapi kwa gharama hizi zinazozidi kupanda kila leo? Kama haitoshi umri wa kuishi wa mtu huyu umepungua sana kisha tunamrudishia ¼tu ya pesa alizotupatia tumhifadhie, tunategemea kuwa na wazee siku za hapo mbeleni kweli?? Nilitegemea tungekuja na mpango mkakati madhubuti kuwa kwakua hawa watu wanatunza fedha zao kwetu kwa muda upatao miaka 25-35+ basi tuweke na riba kidogo hata kama ni 2% kwakua tunazifanyia biashara/Uwekezaji.Ama laa tumeshindwa kabisa tuwape mikopo mikubwa wafanye maendeleo mapema kabla hawajafika uzeeni ili tusijekua na kizazi cha wazee wategemezi, hohehahe wasiojiweza.Kama bado tunaiona ngumu basi kila Mtumishi pensheni yake mara anapoanza kazi ikatwe na kuwekwa moja kwa moja kwenye fixed account ya benki yake huko atapata walau faida ya kila mwaka pia atafaidika na michango yake aliyohifadhi. Mwisho, kinachotia simanzi zaidi hii sheria inataka mstaafu akifariki kabla ya miaka 12.5 watoto wake wachukue kwa niaba yake pesa ya kila mwezi kwa muda wa miaka mitatu(3) tu!
Hii haijakaa sawa, chondechonde tusianze kumtafuta mchawi baadae! Tutegemee ongezeko la wagonjwa wa akili, wizi, ufisadi na uzembe kazini kuongezeka.
Nawasilisha!
Tatizo tunaviongozi wa OVYO mno hizi nchi zetu za Afrika. Pia Mtanzania ni mtu muoga hata kwenye haki yake mwenyewe.
 
Hii hoja Tundu Lissu ameifafanua vizuri na Ndugai naye amejitetea kwa kadiri anavyoona. Tusubiri serikali tuone wanakaza shingo au wataona soo. Nia haikuwa nzuri hata kidogo.

Hii ni fursa ya wananchi kujua ni watu gani watetezi wao, na wepi ni wasaliti wao. Japo nathubutu kusema watawala wa nchi hii wana bahati nzuri, kwa sababu % kubwa ya wananchi ni wajinga (uelewa wao ni mdogo kuhusu haki zao).
Watanzania ni watu wa OVYO sana mie ndio maana naona bora kukaa kimya wanyoshwe hata wabunge hawana maana ni bora waondolewe tu 2020 kusiwe na uchaguzi.
 
Inahitaji moyo sana kuwa mwajiriwa ktk kipindi hiki... Ushauri wa wazi kwa wafanyakazi ni kuandaa mazingira bora ya kustaafu pasipo kutegemea mafao uliyowekeza ktk mifuko ya hifadhi. Tofauti na hapo ni kuumizana vichwa manake watawala wameshaamua. Hakuna namna
Huyo mtawala ni nani na anaamua dhidi ya nani??
 
Kama hii sheria mpya ni kwa ajili ya manufaa ya wafanyakazi kwa nini wasiipindue ile iwe ya wakubwa waweze kufaidi zaidi na walalahoi tuchukue ile ya wakubwa? CCM wameanza lini kuwa wema kwa wafanyakazi?
 
Kwa wale waliohusika na utungaji wa sheria hii, wasiposikia sauti za kilio cha watu kuhusu sheria hii na kufanya haraka KUIBATILISHA, Mungu ataamuru mawe yalie badala ya watu.

Hapo ndipo kila aliyehusika kwa namna moja au nyingine kutunga na kuridhia sheria hii atakapojutia maamuzi yake.
Tutapishana nao kwenye corridors za mahospitali, tukiwa ktk wheel chsirs, sisi wastaafu tukiwa tumepooza kwa frustration wanazotusababishia, na wao wakiwa na wanaugua kisukari baada ya kula walivyojilimbikizia kutokana na jasho letu!!!
Hivi nani aliwaambia michango tuliyokuwa tunatoa miaka yote ilikuwa bima???
 
Habarini wanajamvi!
Wakubwa zangu shikamooni!

Nijikite kwenye hoja ya sheria/kanuni za namna ya kukokotoa mafao ya Watumishi wa serikali kitu kinachopelekea Watumishi ambao wanafikia ukomo wa ajira zao kupata malipo ya mkupuo wa 25% na kiasi cha 75%kinachobaki kulipwa kidogo kidogo kwa muda wa miaka 12.5 hii inamaana kuwa Mstaafu ikiwa atastaafu katika umri wa miaka 55 inamaana atanufaika mpaka anapofikisha miaka 67½ na kama atastaafu na miaka 60 atanufaika mpaka anapofikisha miaka 72½ kitu ambacho kitaleta maisha magumu sana kwa wazee wetu na Wastaafu watarajiwa.

Kwanza tukiachana na hili la mkupuo wa 25% hili la kuweka ukomo wa mafao yaani 12.5yrs baada ya kustaafu ililenga nini?
Yaani ni sawa na kuombea wastaafu wote wafe baada ya hapo siyo ??
 
Ni fedheha sana! Watu tuna wazee wetu walishastaafu tangu miaka 2000 mpaka leo wapo, means wameishi miaka 78 mpaka sasa yaani miaka 18+ baada ya kustaafu, uzuri bado wanalipwa kwa ile sheria ya zamani sipati picha kama ustawi wao ungekua mzuri mpaka leo ikiwa wangekua frustrated na aina hii ya unyama unaoanza sasa. Na inshallah wataendelea kuishi zaidi, sasa leo tunapimiwa umri wa kuishi.
 
Kwa mwendo huu tunaendelea kupalilia rushwa kwa hali ya kutisha. Watumishi wanaanza kuwaza kesho yao ya 61-75yrs. Mafao Bora ni sehemu ya kuimarisha utumishi usiokuwa na mawaa (Kuitumikia Nchi kizalendo)
 
Back
Top Bottom