Umesahau juu ya conflict moja ya majukumu ya serikali na bunge.
Kuna huu mfuko wa maendeleo wa jimbo CDF . Binaffsi naona si sahihi sijui Dr slaa anasemaje. Pili sababu CDF io tayari basi Tumwombe Dr slaa awaagize wabunge wote wa CDM wawe wanachapisha matumizi ya pesa zile za majimbo yao kwenye magazeti kila baada ya miezi mitatu au sita. Hii itasaidia kuonyesha uwajibikaji wa wabunge wa CDM kwa wnanchi tofauti na wa CCM
Mkuu huo ushauri uliompa Dr Slaa sidhani kama ni sahihi. Kuwalazimisha wabunge wachapishe matumizi ya fedha ni sawa na kuhalalisha CDF ambayo imeanzihwa kimakosa. Ushauri wangu kwa serikali ni kufuta kabisa CDF. CDF tumenakili Uganda bila hata kufanya uchambuzi wa kutosha.
Kwa kifupi, CDF imekuwepo Kenya kuanzia 2003, Uganda tokea 2005 na Tanzania nafikiri 2008 kama sijakosea. CDF ilianzishwa Kenya kutokana na nguvu ya wabunge wa upinzani baada ya kuona kuwa majimbo yao yalikuwa hayapati fedha za maendeleo za kutosha toka serikalini kitu ambacho kilikuwa kinasabanisha maeneo hayo kuwa chini kimaendeleo na wananchi kukosa huduma muhimu. CDF ilianzishwa Uganda baada ya mikutano mingi kati ya Rais na wabunge kuwasaidia wabunge kutimiza ahadi walizowahaidi wapiga kura wao. Tofauti na Kenya, wabunge wa Uganda wao wenyewe walipokea cash ya sh milioni 10 za Uganda.
Rais Kikwete naye alisema CDF itaanzishwa kuwasadia wabunge kufanikisha projects za maendeleo na kupunguza kile alichokiita "daily nuisances" ambazo wabunge walikuwa wanakutana nazo majimboni mwao. Rais Kikwete alisema ni aibu kwa wapiga kura kuwataka wabunge wao wachangie kifedha kwenye shughuli za maendeleo wakati hawana fedha za kufanya hivyo. Hii ni pamoja na kuwa wakati wa kampeni wabunge wengi huwa wanatoa ahadi za kifedha.
Hata hivyo Rais Kikwete alisema wabunge wanaweza kusaidia majimbo yao kwa fedha zao kama kulipia watu ada za shule kama wakiombwa, lakini hili lisiwe jukumu lao. Badala yake wabunge waangalie zaidi kwenye masuala kama kuna shule na vifaa vya elimu vya kutosha majimboni mwao ili kuwawezesha watoto wapate elimu. Lakini ukiangalia wale wabunge wanaotetea posho wengi wao huwa wanasema kuwa hizo posho zinawasaidia sana wakiwepo majimboni mwao.
Ukiangalia model ya CDF ya Kenya ni tofauti na ya Uganda labda pia na ya Tanzania. CDF ya Kenya ilianzishwa kwa sheria iliyopitishwa na bunge, baada ya wabunge wa upinzani kulalamika bungeni kuwa majimbo yao yalikuwa yanaponjwa fedha za maendeleo kwa kuwa na wabunge wa vyama vya upinzani. CDF ya Uganda ni mazungumzo tuu kati ya Rais na wabunge fulani ambao nafikiri wapiga kura wao waliwajia juu kwa kushindwa kutimiza ahadi walizotoa. CDF ya Tanzania, Rais Kikwete ndio hivyo alisema itasaidia wabunge kuepukana na "daily nuisances" majimboni mwao.
Watu wanalalamika wabunge ku-manage CDF. Lakini wapo wanaosema kuwa suala zima la CDF is completely useless. Unless tu- abolish local governments, their role will be redundant. Ukiangalia nchi zilizoendelea, local government ndio iko responsible zaidi na local developments. Tatizo tulilonalo kwetu ni kutokuwepo kwa uhusiano wa kutosha kati ya ofisi ya mbunge jimboni na local governments. Sidhani kama CDF itasaidia, badala yake inaweza kuleta matatizo mengine. Utaenda kwa local government watakuambia nenda kwa mbunge wako anazo fedha, hasa pale kama mbunge mmoja huko Singida anaweza kugawa sh 50,000 sijui kwa walimu? (nisahihishe kama nimekosea).
Kuanzisha CDF ni sawa na kusema decentralisation (ambayo ni nzuri kulinganisha na ile ya Kenya) imeshidwa kuleta maendeleo kwa hiyo tutafute mbadala. Serikali kuu na wabunge inabidi wabakie kushughulikia masuala nyeti yanayoathiri system nzima kwa ujumla kupitia MKUKUTA au VISION 2025. Vinginevyo tutakuwa tuna "commercialise" siasa kwa kufanya wapiga kura wategemee misaada ya kifedha toka kwa wabunge kwa kuwapigia kura. CDF itafanya kura za wabunge ziwe zinauzwa.
Kwa nini serikali iwapatie wabunge fedha? Kwa nini wasipewe local governments au NGOs ambazo zinafanya kazi at the district level? Kama alivyosema mbunge mmoja huko Uganda suala la maendeleo ni la kitaifa, amabalo linabidi lipangwe na kutatuliwa kitaifa. Huwezi kutatua tatizo la mandeleo ya nchi kwa kuwapa baadhi ya individuals fedha kwa kutumia CDF. Hata kama ukimpa kila mbunge bilioni 10 hazitaleta maendeleo jimboni kwake.
Kazi za mbunge ni kupitisha sheria na ku-scrutunize matumizi ya serikali. Sasa kama mbunge ni mmoja wa watumiaji sijui ata-scrutunise kivipi matumizi. Kazi ya mbunge kwa mpiga kura sio kugawa fedha kwa wapiga kura wake. Kazi ya mbunge ni kusikiliza matatizo na maoni mpiga kura wake na kuya-channel kwenye vyombo husika.
Nim –quote pia Mzee Msekwa: "Inside his constituency, the MP is expected to carry out the normal duties of meeting and talking to constituents regularly...But again there have developed certain unscheduled expectations of treating their MP as a provider of financial assistance. This can and has created problems for those MPs who are unable to respond adequately to such expectations. For as the old adage goes, ‘members of parliament are men and women of high rank, [but] they have nothing in the bank!"
Alivyosema Msekwa ndivyo inavyotakiwa kuwa. Unfortunately, this is not the case. Wabunge wenyewe wana create unscheduled expectations majimboni kwa kutoa ahadi ambazo hawataweza kuzitimiza.
Sorry kwa post ndefu.