Majibu kwa Nape, Ridhiwan Kikwete na wengine kuhusu elimu yangu na niliposoma

Nape! Kwani first degree yake kama siyo diploma ilikuwa ya nini vile? Kuna darasa mwalimu jk huwa mademu 90%! kasoma hil
 
Safi jembe letu la cdm amwambie lukuvi aonyeshe vyeti vyake?
kujibizana na nape ni kupoteza muda,kwanini ashihoji elimu ya pr.maji marefu au deo sanga? Hii yote inaonyesha jinsi baadhi ya viongozi wa ccm walivyo kosa hoja!
 
Na wewe jee? unataka kila mmoja awe mpayujaki hovyo kama huyo kilaza wenu. Mwenye elimu hawezi kutumia maneno elfu kusema ukweli kuwa "sijamaliza chuo".
Wewe huwezi kujilinganisha na Mnyika hata kidogo huna lolote kwenye Nchi hii zaidi kuwinda mapadri
 
Hata kama mazingira ya Tambaza sio mazuri kwa mtu aliyezoea kutafuniwa kama huko Maua, amesema alichaguliwa kwenda Ilboru hii inatosha kuonyesha kuwa yeye ni kipaji unaweza kutoa sababu ya hata kuiba mtihani akiwa form 4 halafu kumbuka A tisa ni baada ya mtihani wa kwanza kufutwa.Na kama unafikiri ni yalikuwa mashirika ya kidini yalimsponsor BADO Hujaleta facts unaspeculate the truth.... Nimepapenda hapa uliposema "Ni ukweli usiopingika kuwa uamuzi wako wa kutokuendela na masomo ulikuwa zaidi juu ya masuala ya kisiasa" ....Ni ukweli usiopingika wewe hujawahi wala hujui ghiriba za serikali yako naamini ukionyeshwa maovu yote ya state bado unaamini kuwa Serikali yako ni Takatifu... Hapa ndio nimeshangaa mawazo yako.... "maana kuna watu wengi ambao walishawahi kufukuzwa vyuo na wengine kudisco kabisa lakini sasa wana PhD". Duh Bado unaspeculate the truth, hao wengi unaowasema wangapi waligombea Ubunge na kuleta ushindani kama Mnyika? Usipapase lete evidence... Sasa hizi ni siasa...
Ombi langu kwa wanasiasa si kila jambo linahitaji kuendeshwa kisiasa, tujipe Muda tujadili maendeleo ya Taifa,...This is no game ndugu Naamini bado hujaelewa majibu ya Mheshimiwa Mbunge... Ni kwa sababu ya kutetea maendeleo ameamua kujibu huu ujinga wa elimu ilibidi wewe uanze kuwaambia hiyo serikali yako Takatifu kuwa wananchi wa Ubungo wanasubiri Februari 13 ifike lakini wewe unaendeleza siasa Maana kama leo... Bado Mnyika is another class siamini ni sahihi kuziunderate harakati zake kwa mfano kama huu "tutasema tunaacha kusoma kwa ajili ya siasa kesho watoto wetu watasema wanaacha kusoma kwasababu wanataka kucheza soka, mwingine kuwa mwimbaji, na kwasababu hana Muda kwasababu soko litamtupa mkono then hataki hata kusomea huo Muziki ambao ndo anaona unalipa". Kumbuka Mnyika wakiwa sekondari wakati wewe upo darasani Tambaza anatengeneza mazingira ya mdogo wako apate mkopo halafu leo unamlaumu alipata shida chuo ili ndugu yako asiye na shirika la dini aweze kupata nafasi Leo unasema anaweka mfano mbaya kwa ajili ya kukufanyia wewe mwenye Phd ambapo sijaiona imesaidia nini kwa maana kizazi kijacho kitakushangaa ni Phd ambayo haijaibadilisha nchi wala kizazi chako. Naamini ungekuwa na msaada mkubwa kama ungeelekeza mchango wako kwa ajili ya kutusaidia sisi wananchi kuona Ubungo inapata maendeleo. Wasomi wapo lakini mfumo mzima umeelekea ktk ubinafsi sio utaifa hebu elekeza mawazo yako huko


Salute Mkuu Gibbs. Umemjibu huyu jamaa kitaalam sana. Sioni kitufe cha "like". Btw, pokea tano mkuu.
 
sasa huyu RIDHIWAN anahoji elimu ya MNYIKA kama nani,?
hili ndo tatizo la watoto wa viongoz wa afrika baba akiwa kiongoz nawe unajiona kama kiongoz basi angekuchagua uwe makam wa rais 2jue1.
mi katika uongoz wa BUSH wa MAREKAN mpaka amemaliza muda wake siwajui watoto wake lkn hapa kwe2 kimbembe.
kwa ushauri RIDHIWAN ungekaa pemben masuala ya kisiasa hayakuhusu kama unataka siasa ingia., acha chokochoko.
 

Elimu yangu sio siri, nimegombea ubunge mara mbili mwaka 2005 na 2010 na mara zote nimeeleza kuhusu suala hili; Nape na Ridhwan wangetumia tu elimu yao wangetafuta kwenye mitandao na kukuta majibu wanayoyatafuta. Nieleze kwa muktasari tu; nimesoma shule ya msingi Mbuyuni Dar Es Salaam (nilikuwa mwanafunzi wa kwanza kwa mkoa wa Dar es Salaam).
Ningeweza kwenda shule yoyote ya Serikali ya kidato cha tano na sita yenye mchepeo ambapo ningeutaka; lakini niliamua kubaki Dar es Salaam shule ya Tambaza kwa sababu nilitaka kusoma huku nikiendelea na harakati ambazo nilizianza kabla.

Naamini wananchi wa Jimbo la Ubungo walinichagua kwa uwezo na uadilifu wangu, na walijua pia kwamba nilikuwa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwa miaka mitatu. Naamini elimu ni kitu muhimu sana kwa kiongozi, lakini wapo wenye elimu kubwa ya vyeti lakini hawajaelimika na wapo wenye elimu ndogo sana ya vyeti lakini wanaelewa mkubwa wa kutimiza majukumu yao ya uongozi.


JJ

Mhe. Mnyika, mimi ni mmojawapo wa watu ninakuamini kwa umakini wako. Na siku zote nilikuwa najua kuwa wewe lazima utakuwa ni graduate kama siyo una masters. Umeeleza hapo kwenye nyeusi vizuri sana kwamba wananchi wa ubungo hawachakuchagua kwa sababu ya elimu yako. Kinachonipa shida ni kwamba NAPE na RIZ1 walitaka tu ueleze ELIMU YAKO
Badala yake wewe umeandika INSHA NDEFU, ambayo mimi sioni hata umuhimu wake.
Nilitegemea uwe very clear kwamba wewe ELIMU YAKO NI FORM SIX, KWISHNEY. Umeanza kujitetea as if hiyo elimu uliyo nayo ni ndogo sana na haitoshi kutekeleza majukumu yako na hivyo inabidi uongeze na sifa nyingine kitu ambacho SI SAHIHI
KUANZIA LEO FAHAMU KUWA WEWE NI JEMBE KUMZIDI HATA PROF. MAGHEMBE
 
Modern commercial institute imetoa offer ya degree kwa Mh Mnyika.

Hapa mtaani kwetu,wananchi wakisikia Mh. Mnyika ataongea bungeni basi mtaa wote wanasubiri kupata lecture ya ukweli. Hongera Mnyika kwa kukubali kuwa mwalimu wa watanzania wengi,
 
Na wewe jee? unataka kila mmoja awe mpayujaki hovyo kama huyo kilaza wenu. Mwenye elimu hawezi kutumia maneno elfu kusema ukweli kuwa "sijamaliza chuo".
Tufanye tu kwamba ulichosema uko sahihi, ok pamoja na maelezo hayo marefu Mnyika amemalizia na hoja ya tatizo la maji litakuwa Histori Dsm ahadi iliyotolewa na JK, sasa mshaurini na JK naye aje kutujibu hapa alidanganya au alimaanisha?
 
Composed, poised, and polished!

Dogo wa Kikwete na Nape sidhani kama wanaweza kuandika kama alivyoandika Mnyika hapa!

Mkuu Nyani Ngabu!

Heshima kwako!!

Saa hizi wanaigilizia huo mtiririko wa Mh. Mnyika. Kitakacho badilika ni maneno tu. Vinginevyo hawana akili hiyo ya kuandika insha yenye maelezo yaliyoshiba uweleweka.

Mipasho ndiyo kazi yao. si mwalimu wao ni yule malkia wa Mipasho!!!
 
Mhe. Mnyika, mimi ni mmojawapo wa watu ninakuamini kwa umakini wako. Na siku zote nilikuwa najua kuwa wewe lazima utakuwa ni graduate kama siyo una masters. Umeeleza hapo kwenye nyeusi vizuri sana kwamba wananchi wa ubungo hawachakuchagua kwa sababu ya elimu yako. Kinachonipa shida ni kwamba NAPE na RIZ1 walitaka tu ueleze ELIMU YAKO
Badala yake wewe umeandika INSHA NDEFU, ambayo mimi sioni hata umuhimu wake.
Nilitegemea uwe very clear kwamba wewe ELIMU YAKO NI FORM SIX, KWISHNEY. Umeanza kujitetea as if hiyo elimu uliyo nayo ni ndogo sana na haitoshi kutekeleza majukumu yako na hivyo inabidi uongeze na sifa nyingine kitu ambacho SI SAHIHI
KUANZIA LEO FAHAMU KUWA WEWE NI JEMBE KUMZIDI HATA PROF. MAGHEMBE
Hebu ondoa pumba zako hapa, Mnyika ni University drop out. pimbi wewe.
 
Pumba nyingi mchele kidogo. Ngonjera zote za nini? naona unamatatizo zaidi ya huo "mtanziko" uliousisitiza huko juu. Nakuuliza hivi? umeshawahi kuonana na daktari wa magonjwa ya uchizi "psychiatrist"? kama bado, nakusihi uonane nae haraka sana, unaonesha una matizo makubwa zaidi ya "mtanziko".


Sawa ni pumba za JJ; zako ni pombe zilizolala utaishia uharo. Mtu mzima hovyo huna hata staha wala hekima ya nini cha kuzungumza hadharani? Yote haya sababu ya uccm
 
Nilikuwa katikati ya kazi jimboni nikaambiwa kwamba kuna mwito humu wa Nape na Ridhwan kutaka nieleze elimu yangu. WanaCCM walianza suala hili kwa ari, nguvu na kasi mpya niliposema kwamba nchi imefika hapa ilipo kwa sababu ya udhaifu wa Rais Kikwete, uzembe wa Bunge na upuuzi wa CCM.

Nikapuuza, naona sasa limeibuka tena kwa ari, nguvu na kasi zaidi baada ya yaliyojiri bungeni kuhusu hoja binafsi niliyowasilisha bungeni kuhusu maji na mkutano wa hadhara wa tarehe 10 Februari 2013 na masuala ambayo niliipa Serikali wiki mbili kuyatolea majibu ama sivyo nitaongoza maandamano ya wananchi kwenda Wizara ya Maji kutaka uwajibikaji na hatua za haraka.

Kwa mara nyingine tena zinafanyika jitihada za kuhamisha wananchi kwenye mjadala kwa kumshambulia mtoa hoja badala ya hoja, sasa ili turejee kwenye mijadala ya msingi ni muhimu niweke kumbukumbu sawa kuhusu masuala kadhaa kama yalivyoombwa.

Elimu yangu sio siri, nimegombea ubunge mara mbili mwaka 2005 na 2010 na mara zote nimeeleza kuhusu suala hili; Nape na Ridhwan wangetumia tu elimu yao wangetafuta kwenye mitandao na kukuta majibu wanayoyatafuta. Nieleze kwa muktasari tu; nimesoma shule ya msingi Mbuyuni Dar Es Salaam (nilikuwa mwanafunzi wa kwanza kwa mkoa wa Dar es Salaam).

Nilichaguliwa kwenda Shule ya Sekondari ya Ilboru wakati huo ikiwa ya vipaji maalum, sikwenda; wito ulinituma kwenda Seminarini. Nilisoma Franciscan Seminary Maua (FRASEMA) mpaka kidato cha nne; nilipata daraja la kwanza; nikiwa na alama A katika masomo tisa.

Ningeweza kwenda shule yoyote ya Serikali ya kidato cha tano na sita yenye mchepeo ambapo ningeutaka; lakini niliamua kubaki Dar es Salaam shule ya Tambaza kwa sababu nilitaka kusoma huku nikiendelea na harakati ambazo nilizianza kabla.

Hapa ndio ilikuwa chanzo cha mimi kuingia kwenye kazi ya kuhamasisha mabadiliko kwenye mimbari nje ya utumishi wa madhabahuni. Tukio lililobadili mwelekeo wa maisha yangu, mwaka 1998 nikiwa kidato cha nne; nimesoma na tumeanza mitihani tukatangaziwa kwamba mitahani yote imefutwa baada ya kuvujishwa.Tukarudishwa nyumbani kipindi hicho nikaenda kwenye mafungo kujitafakari kwenye mkoa mmoja nikarejea Dar es Salaam nikakutana na wanaharakati kadhaa wa asasi zisizo za kiserikali; maelezo kuhusu ufisadi yalinifanya nione nina wajibu kwa nchi yangu, nikarejea Seminarini kufanya mitihani nikiwa na fikra tofauti.

Matokeo yakatoka nimefanya vizuri, kwa mifumo yetu mibovu ya wakati huo kwa mara ya pili tena Serikali hii inayoongozwa na CCM haikutambua vipaji na nikapaswa niendelee kujilipia ada mwenyewe kama ilivyokuwa kwa ngazi nyingine za elimu zilizotangulia; hapa nikakata shauri kwamba nitatumia uwezo na uadilifu wote ambao Mwenyezi Mungu amenijalia kuwezesha mabadiliko katika taifa letu.

Nikaamua kuacha kwenda kwenye shule za bweni mikoani na kubaki Dar es salaam nisome Tambaza huku nikiendelea na kazi za harakati; wakati huo nikihamasisha masuala ya ukombozi wa vijana nchini. Pamoja na kusoma kutwa huku nikifanya kazi nilipata daraja la pili katika kidato cha sita.

Taasisi nilizoanzisha au nilizoongoza katika kipindi hicho na kazi nilizofanya sio siri na zinapaswa kujieleza zenyewe kwa matendo badala ya maneno. Katika kipindi hicho, wakati huo kukiwa hakuna Mfuko wa Elimu wala Bodi ya Mikopo nikashiriki katika ushawishi wa mabadiliko ya kimfumo; nilikwenda Dodoma, tukakutana na wabunge na mawaziri nikawasilisha mada “Towards a more functional education in Tanzania”, wakati huo nikiwa mwanafunzi wa Sekondari.

Kati ya wabunge waliosikiliza mada niliyoiwaisilisha wakati huo sasa ni Rais Jakaya Kikwete ( Ridhwan ukiwa nyumbani unaweza kumwuliza maoni yake aliyotoa siku hiyo kuhusu ugharamiaji wa elimu na suala la mauaji ya mwanafunzi wa Iyunga Michael Sikupya). Nilipotoka kwenye mkutano ule Dodoma mwishoni wa miaka ya tisini, nilikata shauri kwamba mwaka 2005 nitagombea Ubunge hii ni baada ya kushudia aina ya wabunge waliokuwepo.

Mwaka 2002 nilijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Es Salaam kusomea “Bachelor in Business Administration (BBA) kwenye programu ya jioni; nilifanya hivyo kwa kuamua kwa kuwa nilitaka nisome huku nikiendelea na kazi. Mkuu wa Programu hiyo wakati huo alishangaa sana kwa umri wangu (wakati huo shahada hiyo walikuwa wakisoma wazee watu wazima wafanyakazi) na matokeo yangu (kwa kuwa yaliniruhusu kwenda kuingia kusoma katika mfumo wa kawaida). Nikamweleza akanielewa kwamba sitaki kusoma kama wanachuo wengine wa kawaida, uamuzi wangu huo ulikuwa na gharama kwa kuwatafsiri yake ni kuwa nilipaswa kujisomesha binafsi.

Kwa hiyo mimi ni kati ya wale ambao hatudaiwi na nchi hii kwa maana ya kwamba sijawahi kuchukua ruzuku wala kusomeshwa na Serikali hii inayoongozwa na CCM; nimesoma kwa jasho la wazazi wangu na langu binafsi. Kwa hiyo, nijibu tu kuhusu elimu yangu ya juu kwamba nimesoma miaka mitatu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (mtu aliyosoma kwa kiwango hicho kwenye baadhi ya vyuo duniani hupewa associate degree).

Mwaka 2004 ikaanza misukosuko mbalimbali, mwaka huo ulikuwa ndio unatungwa muswada wa Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, haya matatizo yanayotokea leo niliyatabiri wakati huo. Niliwasilisha mada kwa wanachuo kwenye ukumbi wa Nkurumah kuchambua udhaifu wa muswada huo na kupata maoni ya wanafunzi kuhusu marekebisho yanayohitajika; wanachuo wakapitisha azimio la kwamba muswada huo upingwe.

Kesho yake nikiwa Morogoro kikazi kukafanyika mgomo hatimaye wanafunzi wakapigwa na kukamatwa.Nakumbuka nilikatiza kazi niliyokuwa nafanya nikarejea kwa kuwa Chuo kiliweka sharti kwamba lazima wanachuo waache mgomo ndio waliokamatwa waachiwe. Wakati huo Serikali ya wanafunzi ilikuwa haisikilizwi, mimi na wengine wachache tukajitolea kuzunguka kampasi na hosteli zote kushawishi wanafunzi kurejea masomoni na wakafanya hivyo.

Serikali ya CCM ikatoa maelekezo kwamba kama tumeweza kuwafanya wanafunzi warudi, hata kama sikushiriki mgomo na sihusiki na masuala ya mikopo kwa kuwa ni mwanafunzi ninayejilipia mwenyewe lazima nisimamishwe; nikiwa mwanafunzi pekee wa BBA niliyesimamishwa wakati huo.

Nikarejea baada ya muda tayari kukiwa na mvutano kati yangu na utawala, mwaka 2005 nikaamua kugombea Ubunge wakati huo nikiwa mwanafunzi; mvutano ukaongezeka zaidi. Na utawala wa Chuo ukawa unapata mashinikizo mengi kutoka kwa Serikali na CCM; wengine wakipendekeza nifukuzwe, wengine nifelishwe na wengine nisiruhusiwe kuingia katika maeneo ya Chuo jioni masomoni kwa kuwa nitakuwa nafanya kampeni.

Nikawa katika mtanziko(dilemma) wa kuchagua ama kuendelea na masomo na kujitoa au kupunguza nguvu kwenye kampeni (mbinu nyingi zilitumika wakati huo, sio sehemu ya majibu yangu ya leo) au niendelee na kampeni. Nafsi yangu ikanituma kuamua kuandika barua yakuahirisha masomo, baada ya matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2005 mazingira yalikuwa yamebadilika sana kuweza kurejea kumalizia mwaka au miezi michache iliyokuwa imebaki.

Mwaka 2006 nikiwa Marekani nilitafakari sana na kufikia uamuzi wa kuendelea na kazi hii ya kusimamia mabadiliko na kujiandaa na uchaguzi wa mwaka 2010. Mwaka 2010 niligombea tena na kushinda wakati huo huo nikiongoza kazi za kitaifa za kampeni makao makuu pamoja na Profesa Baregu na wengine; hakuna mahali popote nilipowadanganya wananchi kuhusu elimu yangu, kama nilivyoeleza hapo juu.

Naamini wananchi wa Jimbo la Ubungo walinichagua kwa uwezo na uadilifu wangu, na walijua pia kwamba nilikuwa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwa miaka mitatu. Naamini elimu ni kitu muhimu sana kwa kiongozi, lakini wapo wenye elimu kubwa ya vyeti lakini hawajaelimika na wapo wenye elimu ndogo sana ya vyeti lakini wanaelewa mkubwa wa kutimiza majukumu yao ya uongozi.

Tangu mwaka 2012 na 2013, nimekuwa kwenye mtanziko mwingine na viongozi wangu ndani ya chama wanafahamu; niliomba kuachia majukumu mengine yote katika chama ili nibaki na ubunge peke yake niweze kuwatumikia wananchi wakati huo huo niendelee na masomo zaidi ya elimu ya juu katika fani inayoendana na kazi ninayoifanya ya sasa na matarajio yangu ya baadaye.

Hata hivyo, kwa mwelekeo huu wa Serikali na CCM leo nieleze tu kwamba nikifanya hivyo itakuwa faida zaidi kwa watawala tunapoelekea mwaka 2015; hivyo, nimeamua kama nilivyoamua mwaka 2005; kwamba nitarejea masomoni baada ya CCM kuondoka madarakani na Tanzania kupata Serikali mpya itakayoongozwa na CHADEMA. Kwa sasa nitaendelea kujisomea kila siku ninapopata wasaa kwa kuwa elimu haina mwisho.

Wakili Ridhwan katika maandiko yake amefanya rejea ya suala Kihiyo wa CCM Temeke, nashauri arejee kwenye hukumu ya kesi ile na marekebisho ya sheria yaliyofanywa na Serikali yaCCM kuwalinda wabunge wake vihiyo baada ya hukumu.

Mifano hailingani kwa sababu mimi sijatoa maelezo ya uongo popote. Lakini hata kwa wabunge wa CCM wanaotoa maelezo ya uongo wa wapiga kura, marekebisho hayo yamewawekea wigo wa mianya yakutokea mahakamani. Zamani fomu zakuogembea zilikuwa na mahali pa kujaza elimu ya mgombea, sasa kipengele hicho kimeondolewa. Hivyo, suala la kughushi na kutoa taarifa za uongo haliko kama ilivyokuwa awali, isipokuwa kesi inaweza kufunguliwa ya ukiukwaji wa kawaida wataratibu za kampeni kwa kuwashawishi wapiga kura kwa taarifa za uongo (ndani ya ule muda wa kisheria wa kesi kufunguliwa ambao ulishapita).

Halafu ni jukumu la mlalamikaji sio tu kuthibitisha kwamba uongo ulitolewa bali uongo umeathiri vipi matokeo. Ndio maana leo kuna vihiyo wengi tu wa CCM ndani ya Bunge lakini ni vigumu kuwabana kwa mfumo wetu wa sasa. Baada ya majibu hayo marefu, naamini sasa Nape unaweza sasa kurejea kwenye kujibu; Elimu ya Mnyika ina uhusiano gani na CCM kuahidi kwenye ilani yake na kushindwa kutekeleza kwamba ifikapo mwaka 2010 asilimia 90 ya wananchi wa mijini ikiwemo Dar essalaam watakuwa wanapata maji safi na salama? Ridhwan kwa kuwa umeweza kufanya rejea unaweza pia kueleza ni kwanini Rais Kikwete mwaka 2011 aliahidi kuwa tatizo la maji Dar es Salaam litakuwa historia mwezi Februari 2013 lakini mwezi huo umefika na matatizo bado ni makubwa?

JJ

Majibu mazuri.
 
Complexity of Mental Process
This is innate to each person. we do differ. It is the scale of the complexity of your mental processing that determines the maximum level at which you can work at any time in your maturation and development if you valued the work and if you have the necessary skilled knowledge and experience.

It is a bad practice to waste time doing work that do not add value to the society. Using resources to discuss personal issues, we need to think and work on things that bring better life to people in the society.

Note that today we do use the fruit of people like Albert Einstein though in his school he faced some results that that was not ok but because he was thinking to another level he managed to bring fruits those we do enjoy today. You may read through the website address below

Albert Einstein Biography - Facts, Birthday, Life Story - Biography.com


[h=3]Early life and education for Albert-Einstein[/h] See also: Einstein family


Einstein at the age of three in 1882



Albert Einstein in 1893 (age 14)



Einstein's matriculation certificate at the age of 17, showing his final grades from the Aargau Kantonsschule (on a scale of 1-6, with 6 being the best mark).


Albert Einstein was born in Ulm, in the Kingdom of Württemberg in the German Empire on 14 March 1879.[SUP][10][/SUP] His father was Hermann Einstein, a salesman and engineer. His mother was Pauline Einstein (née Koch). In 1880, the family moved to Munich, where his father and his uncle founded Elektrotechnische Fabrik J. Einstein & Cie, a company that manufactured electrical equipment based on direct current.[SUP][10][/SUP]
The Einsteins were non-observant Jews. Albert attended a Catholic elementary school from the age of five for three years. At the age of eight, he was transferred to the Luitpold Gymnasium where he received advanced primary and secondary school education until he left Germany seven years later.[SUP][11][/SUP] Although it has been thought that Einstein had early speech difficulties, this is disputed by the Albert Einstein Archives, and he excelled at the first school that he attended.[SUP][12][/SUP] He was right handed;[SUP][12][/SUP][SUP][13][/SUP] there appears to be no evidence for the widespread popular belief[SUP][14][/SUP] that he was left handed.
His father once showed him a pocket compass; Einstein realized that there must be something causing the needle to move, despite the apparent "empty space".[SUP][15][/SUP] As he grew, Einstein built models and mechanical devices for fun and began to show a talent for mathematics.[SUP][10][/SUP] When Einstein was ten years old, Max Talmud (later changed to Max Talmey), a poor Jewish medical student from Poland, was introduced to the Einstein family by his brother, and during weekly visits over the next five years, he gave the boy popular books on science, mathematical texts and philosophical writings. These included Immanuel Kant's Critique of Pure Reason, and Euclid's Elements (which Einstein called the "holy little geometry book").[SUP][16][/SUP][SUP][17][/SUP][SUP][fn 1][/SUP]
In 1894, his father's company failed: direct current (DC) lost the War of Currents to alternating current (AC). In search of business, the Einstein family moved to Italy, first to Milan and then, a few months later, to Pavia. When the family moved to Pavia, Einstein stayed in Munich to finish his studies at the Luitpold Gymnasium. His father intended for him to pursue electrical engineering, but Einstein clashed with authorities and resented the school's regimen and teaching method. He later wrote that the spirit of learning and creative thought were lost in strict rote learning. At the end of December 1894, he travelled to Italy to join his family in Pavia, convincing the school to let him go by using a doctor's note.[SUP][19][/SUP] It was during his time in Italy that he wrote a short essay with the title "On the Investigation of the State of the Ether in a Magnetic Field."[SUP][20][/SUP][SUP][21][/SUP]
In late summer 1895, at the age of sixteen, Einstein sat the entrance examinations for the Swiss Federal Polytechnic in Zurich (later the Eidgenössische Polytechnische Schule). He failed to reach the required standard in several subjects, but obtained exceptional grades in physics and mathematics.[SUP][22][/SUP] On the advice of the Principal of the Polytechnic, he attended the Aargau Cantonal School in Aarau, Switzerland, in 1895-96 to complete his secondary schooling.
 
Elimu ni maalifa na sio vyeti, walikunyima nafasi ya kupata degree lakini mambo unayo yafanya na hoja unazozitoa ni kama mtu alie na PHD we nooooomaaaaaa!!!! jembe la Ukweli, tunamsubili nape aje na historia yake ya elimu
 
Kwa sisi tunaomfahamu John Mnyika kwa muda mrefu, naweza kusema kusema tu kuwa JJ ni mmojawapo ya wanafunzi bora kwa kiwango cha ufaulu wao kuwahi kutokea katika nchi hii.

Na kwa mtu yeyote mwenye akili huru, atakubali kuwa uelewa wa JJ katika mambo mbali mbali ni mkubwa sana kuliko hata baadhi ya wabunge wenye shahada za uzamili na uzamivu.

Naamini kabisa JJ angeamua kuwa academician, basi tungekuwa tukimuongelea katika ngazi ya kina Prof. Mwandosya, Prof Luhanga na magwiji wengine wa taaluma.

That's all I can say about him for now.
 
Cheti unaweza kukipata kwa :1.Kukariri bila kuelewa a(kumeza nakutapika kwenye mtihani)2 kuwahonga au kuwainfluency wahadhili kwa manufaa ya mitihani yako kwa namna yeyote ile e.g cheo cha baba ,hela , ngono n.K3kudesa kwa wezio au vyovyote vile Lakini elimu lazima ujifunze kiukweli na uwe mzuri kichwani. Kujifunza sio lazima ukae Drsn Wapo college drop out kama Bill gate ambao ukuzi na ueledi wao hauwezi kufananishwa na wengi humu mlio na digrii feki Myika is intelligent , his IQ is great no ubishi Kuna dalili zote kwamba Riz1 anatoka ukoo wa vilaza
Sio tu dalili ndo ilivo....si unacheki mshua tu uwezo wake wa kuunga unga!!!!mwaka juzi mdogo wake riz one kaangukia pua mbulula kweli shule nzima ye ndo kaibuka na four, wote tu ni vilaza!!!
 
Mnyika amezaliwa kizazi tofauti na kinachomhitaji ana mambo makubwa kuliko kwa hiki kizazi cha misukule. Just imagne mtu anaulizwa kwanini ahadi ya kuleta maji Dar Feb, 2013 haijatekelezwa anasema ilani ni ya miaka 5. Af sisi tunachecheka tu.
 
Back
Top Bottom