Mpango Kama huu wa kutafuta kiki kwa kutumia SMG siku hizi unakubarika TZ?
Mpango huu wa kipuuzi hauwezi kukubalika sehemy yoyote ile ulimwengu huu. Tatizo ni kuwa wewe unatafuta kiki kwa kutukana halafu unawekwa ndani unapata maarufu fulani. Baadaye kisheria unatolewa rumande ila kiki umeshapata. Mwingine anafanya hivyo hivyo, naye anapata kiki. Sasa wewe unataka kupata kiki kwa namna tofauti. Ndio unatafuta kwa kushambuliwa na SMG ila gari tu iumizwe wewe ubaki salama. Bahati mbaya hupangi peke yako. Unaopanga nao wanabadilisha gia angani wanapanga uuawe kabisa. Hapo majuto mjukuu. Kuwezi kusema wale waliobadilisha gia kwa sababu ni aibu kubwa. Inabidi uwanganganie wale uliotaka waonekane wamekushambulia. Sasa kwa vile dereva alishirikishwa, je naye atakubali na hiyo ajenda unayotaka ionekane wakati hakutegemea wewe udhurike???