Maji ya mto yageuka 'rangi ya damu' Urusi

Maji ya mto yageuka 'rangi ya damu' Urusi

gimmy's

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2011
Posts
3,344
Reaction score
3,397
_91074111_redriverafpgpeace.jpg

Maji katika mto Daldykan yamekuwa ya rangi nyekundu

Wachunguzi wa masuala ya mazingira nchini Urusi wanajaribu kubaini sababu iliyoyafanya maji ya mto ulio karibu na kiwanda cha nikeli cha kampuni ya Norilsk Nickel kubadilika na kuwa ya rangi nyekundu.

Picha za maji ya mto Daldykan ambayo yamebadilika rangi zimesambazwa sana katika vyombo vya habari Urusi.

Gazeti la serikali la Rossiiskaya Gazeta linasema kuvuja kwa bomba la kusafirisha taka za mchanganyiko wa shaba nyekundu na nikeli huenda likawa kiini cha maji hayo kubadilika rangi.

Norilsk Nickel ndiyo mzalishaji mkubwa zaidi wa nikeli na palladium duniani.

_91067871_mediaitem91067869.jpg

Picha za runinga ya wizara ya ulinzi ya Zvezda TV

Kampuni hiyo ina vinu na tanuri nyingi rasi ya Taimyr eneo la Krasnoyarsk katika jimbo la Siberia. Ujenzi wa vinu hivyo vikubwa ulifanyika enzi za muungano wa Usovieti.

Kampuni hiyo ina kiwanda kwa jina Nadezhda karibu na mto Daldykan lakini maafisa wake wanasema hawajapata dalili zozote za uchafuzi kutoka kwa kiwanda hicho.

Rais wa kampuni hiyo ni bilionea Vladimir Potanin.

_91067874_5b051dc2-7e3c-4675-aea8-6293d9c9418b.jpg

Chanzo: BBC Swahili
 
haiwez kuwa damu..zitakuwa lava na ndo sababu yanakuwa ya moto
 
kwakuwa damu ni nyekundu na yenyewe yamekuwa mekundu basi yamekuwa damu! duh.. madaktari si wangejaa hapo kuchukua kupeleka hospital
 
haiwez kuwa damu..zitakuwa lava na ndo sababu yanakuwa ya moto
Nawewe kuwa mwelewa, umeambiwa vinu vimetema Nickel na Palladium, sasa lazima ujue kemia ya madini hayo na maji laini.
 
Back
Top Bottom