Maji safi na salama

JAYJAY

JF-Expert Member
Oct 31, 2008
7,492
7,515
mara nyingi nimesikia ikisemwa maji safi na salama.naomba kuuliza,je maji yanaweza kuwa safi lakini sio salama au yanaweza kuwa salama lakini sio safi?
 
mara nyingi nimesikia ikisemwa maji safi na salama.naomba kuuliza,je maji yanaweza kuwa safi lakini sio salama au yanaweza kuwa salama lakini sio safi?
Maji yanaweza kuwa safi lakini si salama kwa matumizi ya binadamu, na pia yanaweza kuwa salama lakini si safi kwa matumizi ya binadamu.

Mfano: Maji ya kwenye bwawa la kuogelea (Swiming pool).

Vile vile Maji ya baharini, ambayo yamebeba sifa zote hizo.
Ni safi lakini si salama kwa matumizi ya kunywa binadamu...!
 
Maji safi na salama ni maji yaliyochemshwa na kuchujwa. haya ni safi kwa matumizi ya kunywa kwa mwanadamu
 
Maji safi yanaweza kutumika katika shughuli mbalimbali kama kuoga, kufulia, kuoshea vyombo n.k. Lakini maji Salama yanafaa kwa kunywa na ama kupikia!
 
Maji yanakuwa safi kwa macho na yanaweza kutumika kwa kuogea, kufulia n.k. Lakini si kwa kunywa. Maji salama ni pale yanapothibitika kuwa hayana madhara kwa binadamu. Na maji hayawezi kuwa salama bila kuwa safi!
 
Back
Top Bottom