Majesuit walivyojipenyeza kwenye makanisa

Majesuit walivyojipenyeza kwenye makanisa

Mfumo wa kiuendeshaji wa kisabato hauna kiongozi Mkuu wa sehemu kwa mfano Kijiji, kata, wilaya, Mkoa , Taifa au kikanda kama Afrika Mashariki. Ambao hukutana kwa kipindi fulani kupeleka taarifa.?
Mfumo upo hivo, but mfumo wa msonge au pyramid ambao muumin anakuwa mpokeaji tu umeingia hata sabato
 
sibishi, ila miaka ya nyuma makanisa haya yalikuwa na misimamo migumu kuhusu kujiunga na jumuiya za kikristo. Hii CPTC wameianzisha miaka ya hivi karibuni baada ya kuona wenzao wa CCT wako pamoja na wanatambuliwa na serikali kiasi cha kupewa airtime kwenye media za umma
Miaka ya nyuma Ni kweli kulikuwa na usafi

Now Shetan ameshaingia makanisani ndio maana kila siku Vituko vingi
 
Siku hizi viongozi wa dini hawataki kuguswa Wala kuhojiwa
 
Wamekuwa wakihangaika kupenyeza watu wao kuharibu ,na wamekuwa wakifeli
🤣🤣🤣🤣 wasabato mnajikutaga watakatifu sana aisee.

Na kwanini msihubiri mambo mema yatakayomfanya mtu atende mema na kuacha mabaya.

Nyuzi za wasabato humu ni kuuponda ukatoriki, huwa mnafundiwa haya mambo huko makanisani? Huwa mnalishwa sumu ya namna gani juu ya ukatoriki.

Ni sawa tu na wale waanzishao nyuzi kuukashfu uislam.
Hii kitu haina msaada juu ya kanisa lenu, ninapenda jinsi mnajitahidi kuikalili na kuilewa biblia kwa mujibu wa dhehebu lenu ila hii chuki dhidi ya ukatoliki inawaharibia sana, sioni kama inasaidia kiti.
 
System ya mpinga Kristo ni ipi?

Ni kikundi kidogo cha watu ambacho kinajiita makao makuu au mtu mmoja kufanya maamuzi ya kimaisha juu ya halaiki (a small group dictates how the majority should live).

Hivyo mfumo wa mpinga Kristo ni mfumo wa msonge (pyramid), ni udikteta wa kimfumo (Urasimu). Wa juu anatumikiwa na wa chini na kupangiwa jinsi ya kuishi. Kwahiyo ni system ambayo inajihodhisha nafasi ya Mungu duniani kwa kukalia uhuru wa dhamiri. Na roho hii ya mpinga Kristo inachukua nafasi zote (dini, siasa na uchumi). Hivyo basi ukiona upo kwenye serikali au dini yenye mfumo Kama huo basi jua upo ndani ya mfumo wa antichrist.

Ndani ya madhehebu leo, washiriki hawana usemi, haki zao zimeporwa na makao makuu au kikundi cha wachache ambao wamejipa wakfu wa kiungu kama wapakwa mafuta wa pekee, uaskofu wa kipekee ambao hawatakiwi kuhojiwa au kunyooshewa kidole, maana wanadai utalaaniwa kama ukiwakosoa, maana wao wanaongea na Mungu. Hivyo ukihoji jambo lolote ambalo limekaa kushoto utajibiwa tu hilo limetoka juu, hivyo usihoji, kwanza wewe nani? Na ukizidisha hoja zako utaambuliwa kuondolewa na kupewa jina baya. Kama ndio unayokutana nayo basi tambua upo chini ya mfumo wa mpinga Kristo.

Mfumo wa Kristo ni uhuru (liberty), ametuita ili tuwe huru kutoka dhambini na kutoka kuwa watumwa wa wanadamu. Hivyo imeandikwa Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kwelikweli.. Yn 8:31-36. Lakini mpinga Kristo hataki uhuru wa watu, bali utumwa, ni Yeye, "Asiyewafungua wafungwa wake waende kwao?Isa 14:17 SUV. Lakini Kristo ni Yeye, mwenye "kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,Lk 4:18 SUV"

Kuhusu utawala wa Kristo, ni utawala wa kitumikiana na si wa msonge

Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni. Wala msiitwe viongozi; maana kiongozi wenu ni mmoja, naye ndiye Kristo. Naye aliye mkubwa wenu atakuwa mtumishi wenu.Mt 23:9‭-‬11 SUV

Mahali pengine imeandikwa hivi,

"Lakini Yesu akawaita, akasema, Mwajua ya kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha. Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu ye yote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu; na mtu ye yote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu; kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.Mt 20:25‭-‬28 SUV"

[emoji3516] Hivyo kwanza Utawala wa Kristo una Baba mmoja ambaye ni Mungu, una kiongozi mmoja ambaye ni Kristo. Kwahiyo hakuna mwakilishi wa Kristo wa kipee duniani (vicar of Christ) sote tu mabalozi wake hapa duniani. Na ambaye anajisikia au kutaka ukubwa basi anapaswa kuwa mtumishi wa wengine, hivyo wa juu ndio anatumikia wa chini, ni utawala wa kitumishi kama Yesu alivyo mtumishi wa watumishi ingawa ni mtu mkubwa sana lakini aliwaosha wanafunzi wake miguu kazi ambayo ni ya kitumwa na zaidi akautoa uhai wake.

YESU amesema wakuu wa dunia, hututumikisha yaani wanaishi kwa protocol ya ukuu wa ngazi ngazi, hata kama umepangwa kutoa somo au speech lakini bahati mbaya akaja mkubwa wako itakubidi umpishe yeye. Lakini katika utawala wa Kristo, hakuna kitu kama hicho, wote tu ndugu (brother and sister) wote tukiwa chini ya kichwa kimoja yaani Kristo. Hivyo ukiona kwenye dhehebu lenu kuna utaratibu wa msonge yaani uongozi wa kingazi ngazi jua upo chini ya utaratibu wa kisekula (kidunia) na si kwa jinsi ya Kristo. Mpinga Kristo anadondosha kitu kutoka juu na kinashuka hadi chini, maana yeye yupo juu ya pyramid kama jicho la uongozi, na anayepinga, anaitwa msaliti au mzushi, hivyo afutiliwe mbali. Diotrefe ni mmoja aliyeanza utawala wa piramidi ndani ya Kanisa, Yesu alionya msitake kuwa wa kwanza (wakubwa) miongoni mwa ndugu, lakini Diotrefe alifanya hivyo alijiweka kuwa wa kwanza. Yohana anasema,

"Naliliandikia kanisa neno, lakini Diotrefe, apendaye kuwa wa kwanza kati yao, hatukubali. Kwa hiyo, nikija, nitayakumbuka matendo yake atendayo, atoavyo upuzi juu yetu kwa maneno maovu; wala hatoshwi na hayo, ila yeye mwenyewe hawakaribishi hao ndugu, na wale watakao kuwakaribisha, huwazuia, na kuwatoa katika kanisa.3 Yoh 1:9‭-‬10 SUV"

Diotrefe alijimilikisha Kanisa, akamzuia mpaka Mtume Yohana na kukataa nyaraka zake, na aliwapinga wajumbe waliotoka kwa mtume Yohana. Na zaidi aliwazuia na kuwafukuza ndugu wasiokubaliana naye. Hawa kina Diotrefe ndio mbwa mwitu wakali wasiohurumia kundi aliowatabiri Paulo. (Mdo 20:28+). Hivyo Paulo alivyowaandikia wathesalonike juu ya Siri ya uasi ya mpinga Kristo ambayo alisema ipo hata sasa inatendakazi aliwalenga watu aina ya Diotrefe. Na Yohana aliandikia Kanisa la efeso kulionya juu ya wapinga Kristo wengi waliondani ya Kanisa yaani sampuli ya kina Diotrefe wanaotaka ukubwa na kupingana na mafundisho ya Yesu na mitume. Hivyo leo hii wakati Kanisa katika upofu linamsubiri mpinga Kristo wa kisiasa hapo Yerusalem, ni dhahiri mpinga Kristo halisi na jeshi lake wapo ndani ya Kanisa kwa siri akitenda kazi zake kama kiongozi wa dini. (2 Watch 2:3-4). Wakati utafika atafunuliwa na kuwekwa wazi na watu watashangaa sana, na kusema hivi ni huyu na hawa? Na si yule ambaye tunamgonjea atese Wayahudi huko Yerusalem?. Dunia imeleweshwa mvinyo wa mpinga Kristo mpaka imekuwa na wazimu, inaamini chochote maadamu kimetoka juu (kwa wakuu wa serikali na madhehebu ya dini), hivyo haki za uhuru wa dhamiri za kiimani, kiafya, kisiasa na kiuchumi zimeporwa kutoka kwao na kuwekwa chini ya utaratibu wa mpinga Kristo ambaye amejificha nyuma ya serikali na dini. Wito ni kutoka Babeli kwa haraka ili usipokee mapigo yake. Ufunuo 18:4-5

Mwisho: Kanisa ni umoja wa udugu katika Kristo, ni familia ya Mungu Baba, na Kristo akiwa kaka mkubwa na sisi tukiwa wadogo zake, sheria ya Roho wa uzima ikitawala kati yetu katika pendo. Tukitumikiana kwa Neno la Baba huku wenyeji wetu ukiwa mbinguni. (War 8:29; Waf 3:20).
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] wasabato mnajikutaga watakatifu sana aisee.

Na kwanini msihubiri mambo mema yatakayomfanya mtu atende mema na kuacha mabaya.

Nyuzi za wasabato humu ni kuuponda ukatoriki, huwa mnafundiwa haya mambo huko makanisani? Huwa mnalishwa sumu ya namna gani juu ya ukatoriki.

Ni sawa tu na wale waanzishao nyuzi kuukashfu uislam.
Hii kitu haina msaada juu ya kanisa lenu, ninapenda jinsi mnajitahidi kuikalili na kuilewa biblia kwa mujibu wa dhehebu lenu ila hii chuki dhidi ya ukatoliki inawaharibia sana, sioni kama inasaidia kiti.
Hiyo INJILI unayotaka ya kupakana Mafuta ,nenda kwa mwamposa ,ukapokee magari na kulishwa keki


Ungelaumu Biblia kwanza inayowasema waabudu masanamu ,n.k

Roman Catholic ndiye anayeharibu Ukristo duniani ,

Mafundisho yote ya kipagani yaliyotapakaa kwenye makanisa Yeye ndiye mwanzilishi

Tukikemea pombe utasema Tunawasema wakatoliki

Tukikemea ibada za Sanamu utasema Tunawasema wakatoliki

Tukikemea ibada za Wafu utasema Tunawasema wakatoliki

Tukikemea ibada za kipagani utasema Tunawasema wakatoliki

N.k
 
Wasabato bana....😂😂😂hivi nyie Wasabato inaonekana adui yenu sio shetani bali Wakatoliki 😂😂😂 kilasiku mnakuja na mapokeo yenu ya kuwaponda Wakatoliki lakini cha kushangaza wanazidi kupata wafuasi wengi duniani kuliko dhehebu lolote la kikristo 😆😆
Maisha yao magumu ..
 
Hiyo INJILI unayotaka ya kupakana Mafuta ,nenda kwa mwamposa ,ukapokee magari na kulishwa keki


Ungelaumu Biblia kwanza inayowasema waabudu masanamu ,n.k

Roman Catholic ndiye anayeharibu Ukristo duniani ,

Mafundisho yote ya kipagani yaliyotapakaa kwenye makanisa Yeye ndiye mwanzilishi

Tukikemea pombe utasema Tunawasema wakatoliki

Tukikemea ibada za Sanamu utasema Tunawasema wakatoliki

Tukikemea ibada za Wafu utasema Tunawasema wakatoliki

Tukikemea ibada za kipagani utasema Tunawasema wakatoliki

N.k
Sasa si ukemee hivyo ulivyotaja hapo, aliesema ukikemea hayo atasema unawasema wakatoriki ni nani??

Huko kanisani kwenu pia ibada huwa ni kama hizi nyuzi mnazoleta jf??

Acheni inferiority complex aisee , wakatoliki hawana shida na usabato ila wasabato alooo kama mmechanjiwa.

Kila msabato humu lazima auseme ukatoliki why?? Ndivyo bi Elen alivyowaelekezeni??
 
Muundo wa Jesuit ndani ya makanisa; Uongozi wa Kanisa la Kristo si wa kutawala akili (mindset) za waumini bali wa udugu (utumishi).

Yesu alikataza kiongozi kutumikiwa bali kutumika kama Yeye alivyoacha yote na kutumika na kutoa nafsi yake kuwa fidia ya wengi. Njia ya kuwa mkubwa katika ufalme wa Yesu ni kujishusha naam kutumikia wengine na si kutumikiwa kama wafalme, marais na wenye mamlaka. Mathayo 20:25-28; 23:8-12.

Kama ni nabii, mtume, mchungaji, mwalimu na mwinjilisti tambua umeitwa si kuwa boss wa waumini au kutumikiwa bali kutumika (kuwa mtumishi wao). Ukiona mtu ana hadhi ya kiongozi wa kanisa na ana nguvu juu ya akili za waumini naam anaangukiwa kwa heshima na kauli yake ni amri na kwamba anaweza kumtoa huyu na kumrudisha huyu tambua huyo ni si mtu wa Kristo bali wa yule "ASI".

Wajesuit mnamo 1534 ndio waliokuja na mpango mkakati kabambe, walijiita askari wa Yesu ambao wanautoa uaminifu wao na utii kwa Yesu ama mwakilishi wake (Papa). Hivyo Wajesuiti walijiweka katika mamlaka ya papa, wakimuahidi utii bila masharti, Kufundisha, kukiri imani, kuhubiri na kujitoa kufungua uwanja mpana wa mamlaka ya Papa kwa dunia yote.

Inigo(Ignatius Loyola) kiongozi muasisi wa Jesuit alisema;

“Kwamba wote tuwe na nia moja na kukubaliana na kanisa, kama limetafsiri kitu chochote kuwa ni cheusi wakati kinaonekana machoni mwetu kuwa ni cheupe, tunapaswa kukitangaza kuwa ni cheusi. Maana bila shaka tunapaswa kuamini,.......” [Ignatius Loyola,

Spiritual Exercises, Rule 13 Henry Bettenson, ed., Documents of the Christian Church, 2nd ed. (London: Oxford University Press, 1963), p. 260.

Hivyo kujitolea kwao ni kama fimbo mkononi mwa mchungaji na maiti inayopelekwa isipotaka. Hawa waliupa Upapa nguvu nyingi kupitia shule na vyuo ambako walifunza watoto na vijana kutoa uaminifu wao (wa kimaiti) kwa viongozi wao.

Naam Jesuit ndio champion wakubwa katika baraza la Trento mnamo karne ya 16 wa kutetea kwamba Papa hakosei (infallible) na neno lake ni kama la Mungu au Yesu. Kumpinga au kumkosoa ni kama kumkosoa Mungu au Yesu.

Ulikuwa mchuano mkali sana, maana Waprotestant walidai Neno la Mungu naam Biblia ndio infallible na si Papa. Na kuwa Kanisa linaongozwa kwa msingi wa maandiko na si kwa mabaraza ya maskofu au papa. Jesuit waliinuka kidedea katika baraza la trento na Papa akawatukuza na kuwapa hadhi ya wanajeshi wa kanisa.

Kutokea hapo ukawepo mpasuko mkubwa kati ya Wakatoliki na Waprotestant, na hapo Wajesuit wakaanza njama za kuzuia uprotestant (counter reformation). Maana kama utaruhusiwa kuenea duniani pote Upapa utapoteza nguvu, maana umejengwa katika msingi kwamba wao wamekalia kiti cha Petro mwakilishi wa Kristo duniani na mkuu wa mitume.

Kwahiyo papa anapaswa kupewa heshima za Kristo duniani, hivyo kama Uprotestant utaruhusiwa kuenea basi Ukatoliki na Upapa utakufa. Mara moja majesuit walijieneza kila pande ili kuuzuia uprotestant.

Zingatia kuwa Uprotestant ulianzishwa katika kanuni kwamba Biblia na Biblia pekee ndio mwongozo wa kanisa. Na Rumi yenyewe ilidai kuwa Biblia si yote, mapokeo na Mabaraza ndio mwongozo wa kanisa. Na zaidi uprotestanti ulikanusha mamlaka ya Papa juu ya kanisa na kumpa papa cheo cha mpinga kristo.

Na ukaenda zaidi kupinga uundwaji wa madhehebu yenye kichwa (askofu mkuu) wakidai ni upapa kwa sampuli nyingine. Hivyo wakaanza kutengeneza kanisa kwa kulitoa kwa maskofu na papa na kuliweka katika mikono ya washiriki na Biblia. Jambo hili lilikuwa tanzi kubwa kwa Ukatoliki ambalo lilisababisha wafalme wamuasi papa kwa kuungana na imani ya kiprotestant.

Jesuit mara moja waliingia kazini maana Papa na kanisa walishindwa kuhimili kishindo cha waprotestant, maana hata mbinu za kuwaua zilishindwa kuwasimamisha.Watu Kama Martin Luther, Jonh Knox,John Calvin , Sir Isack Newton (huyu makabrasha yake mengi kuhusu Dini yamefichwa tumeachiwa haya ya physics na Mathematics ).

Waprotestant waliuliwa Sana wengine waliponea chupuchupu , lakini MAJESUIT wakaona mbona tunawaua lakini ndio wanazidi kuinuka

Jesuiti walikuja na mbinu kali si za kuwafutilia mbali waprotestant tena duniani bali kuwageuza kuwa Warumi wa kiroho.

Wajesuit wakaanza kuingia kwenye makanisa haya uyajuayo ,wakiingiza mafundisho yao yale yale kutoka Roma. Mfano Wahitimu wa Degree ya 18 ya Freemason huitwa Rose and Croix hawa ni maalumu kwa kuingiza alama za misalaba ndani ya madhehebu ya kikristo yote uyajuayo.

Huo Ni mfano tu Kuna kikundi Cha kuingiza Ushoga na kumuinua mwanamke makanisani ,(kumbuka campaign ya Ushoga huwa zinaenda sambamba na ile ya mwanamke kuwa juu ya mwanaume)

Tuendelee...

Biblia inaweka mamlaka ya Kanisa mahalia katika mikono ya waashiriki na wazee wa kanisa. (Matendo 20:28).

Lakini kwa ujanja wa Wajesuiti kwa miaka wamefanikiwa na kuweza kuondoa mamlaka ya Kanisa kutoka katika mikono ya washiriki na kuweka katika makao makuu ya madhehebu. Na sasa wakiwa juu ya makao makuu ya madhehebu wanasukuma karibu madhehebu yote ya Kiprotestanti katika mikono ya Vatican.

Wajesuit wanaenda kukamilisha: kusimika Kanisa la kiulimwengu na kuleta mwisho wa Uprotestanti. Unaposoma

"historia ya siri ya Wajesuiti,

"Utaona mfanano kati ya sekta za kidini na kisiasa. Unabii unaonyesha kupenya na kujiingiza kwa Wajesuiti katika serikali na mataifa ya ulimwengu wa kuendesha michakato ya kuharibu historia na kuweka utawala wa kidikteta, na kudhoofisha demokrasia kama vile katika nchi ya Marekani, kwa kuvuruga jamii, Kanisa, siasa, maadili, jeshi, elimu na kuleta machafuko ya kidini ili dunia ipate agizo jipya (kurejesha utawala wa zamani wa kidikteta wa madhabahu).

Leo makanisa yote ya kiprotestanti hata hilo lako unalojivunia kila siku yanaongozwa na makao makuu na yakiwa na kichwa chenye amri au baraza kuu.

Mshiriki hana sauti tena katika makanisa, amelazimishwa kutii kanuni zilizoandaliwa na wakuu na si Biblia. Ukipinga uovu wao utaitwa mkosefu, muasi anayewanyoshea wakapakwa mafuta kidole naam kufutwa ushirika pia.

Ukisoma Isaya 14:12

Utaona maazimio matano ya Lucifer , someni Biblia vizuri jamani ina Siri nyingi

Kuna kauli pale za "NITA" zipo 5, kuna kauli ya nitapanda mpaka pande za kaskazi.

Pande za kaskazi ndipo lilipokuwapo hekalu la Suleiman, na ndipo zinapotokea Dini 3 kuu (Uislamu, Ukristo na Uyahudi). Ukisoma tafsiri nyingine neno lililotumika pale lina maana ya madhehebu.

Kwasasa Uprotestant umesharudi Roma, leo Akifufuka Martin Luther na wanamatengenezo wengine watashangaa Sana harakati walipoziachia zimerudi hatua elfu 10 nyuma.

Kwasasa MAJESUIT wameunda Taasisi inaitwa Eukumen ambayo madhehebu yote yameungana na viongozi wa makanisa , madhehebu hukutana huko.

Ingia kwenye website yao utakuta list ya madhehebu na makanisa likiwepo la wewe unayesoma.
Kwa hiyo unataka kusema hili la kumfanya mwanamke kuwa kuhani(mchungaji) ni kampeni ya kiharakati ndani ya kanisa kama ilivyo sasa harakati ya kuwatambua mashoga / wasagaji na kuwabariki kuelekea ufungaji kamili wa ndoa ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo unataka kusema hili la kumfanya mwanamke kuwa kuhani(mchungaji) ni kampeni ya kiharakati ndani ya kanisa kama ilivyo sasa harakati ya kuwatambua mashoga / wasagaji na kuwabariki kuelekea ufungaji kamili wa ndoa ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio yanaenda sambamba ,kwenye Ushoga Pana Usawa Kwa wanawake
 
Wasabato bana....[emoji23][emoji23][emoji23]hivi nyie Wasabato inaonekana adui yenu sio shetani bali Wakatoliki [emoji23][emoji23][emoji23] kilasiku mnakuja na mapokeo yenu ya kuwaponda Wakatoliki lakini cha kushangaza wanazidi kupata wafuasi wengi duniani kuliko dhehebu lolote la kikristo [emoji38][emoji38]
hakuna utofauti wa shetani na ukatoliki. Papa ni msimamizi wa mfumo wa utawala wa shetani duniani kupitia dini.

swala la wakatoliki kuwa wengi, ni sawa, maana dunia yote nayo hukaa katika yule mwovu (shetani). Njia ni pana iendayo upotevuni. Stuka mkuu!!!!!


YESU NI MWOKOZI
 
Sio wasabato tu, wao ndio watunzi wakuu wa hizi hadithi lakini makanisa ya kiroho yamekopa hizi porojo na ni sehemu ya syllabus zao shule za wachungaji. Kwasasa hizi hadithi zinaenezwa zaidi na watu kutoka hayo makanisa ya kiroho.

Hizi porojo ukimpa hata mchungaji wa Lutheran au Anglican watazikataa wakati wao ndio founder wa reformation.
akifufuka Martin Luther leo itabidi afe tena, maana kile alichokiacha sicho kilichopo saivi. Ma Jesuit wameshaupiga uprotestant, sasa uko hoi! wame compromise na ukatoliki!

huwezi tenganisha u-papa na utawala wa shetani duniani.


JESUS IS SAVIOR
 
Sasa si ukemee hivyo ulivyotaja hapo, aliesema ukikemea hayo atasema unawasema wakatoriki ni nani??

Huko kanisani kwenu pia ibada huwa ni kama hizi nyuzi mnazoleta jf??

Acheni inferiority complex aisee , wakatoliki hawana shida na usabato ila wasabato alooo kama mmechanjiwa.

Kila msabato humu lazima auseme ukatoliki why?? Ndivyo bi Elen alivyowaelekezeni??
Mimi sio msabato, ila anachokisema huyo ndugu, ndivyo kilivyo. Amelichambua Neno la Mungu, Biblia. Acha kufungwa na dini, Toka humo!!!!!!


YESU NI BWANA
 
Back
Top Bottom