Majesuit walivyojipenyeza kwenye makanisa

Jackwillpower

JF-Expert Member
Oct 4, 2017
2,299
3,411
Muundo wa Jesuit ndani ya makanisa; Uongozi wa Kanisa la Kristo si wa kutawala akili (mindset) za waumini bali wa udugu (utumishi).

Yesu alikataza kiongozi kutumikiwa bali kutumika kama Yeye alivyoacha yote na kutumika na kutoa nafsi yake kuwa fidia ya wengi. Njia ya kuwa mkubwa katika ufalme wa Yesu ni kujishusha naam kutumikia wengine na si kutumikiwa kama wafalme, marais na wenye mamlaka. Mathayo 20:25-28; 23:8-12.

Kama ni nabii, mtume, mchungaji, mwalimu na mwinjilisti tambua umeitwa si kuwa boss wa waumini au kutumikiwa bali kutumika (kuwa mtumishi wao). Ukiona mtu ana hadhi ya kiongozi wa kanisa na ana nguvu juu ya akili za waumini naam anaangukiwa kwa heshima na kauli yake ni amri na kwamba anaweza kumtoa huyu na kumrudisha huyu tambua huyo ni si mtu wa Kristo bali wa yule "ASI".

Wajesuit mnamo 1534 ndio waliokuja na mpango mkakati kabambe, walijiita askari wa Yesu ambao wanautoa uaminifu wao na utii kwa Yesu ama mwakilishi wake (Papa). Hivyo Wajesuiti walijiweka katika mamlaka ya papa, wakimuahidi utii bila masharti, Kufundisha, kukiri imani, kuhubiri na kujitoa kufungua uwanja mpana wa mamlaka ya Papa kwa dunia yote.

Inigo(Ignatius Loyola) kiongozi muasisi wa Jesuit alisema;

“Kwamba wote tuwe na nia moja na kukubaliana na kanisa, kama limetafsiri kitu chochote kuwa ni cheusi wakati kinaonekana machoni mwetu kuwa ni cheupe, tunapaswa kukitangaza kuwa ni cheusi. Maana bila shaka tunapaswa kuamini,.......” [Ignatius Loyola,

Spiritual Exercises, Rule 13 Henry Bettenson, ed., Documents of the Christian Church, 2nd ed. (London: Oxford University Press, 1963), p. 260.

Hivyo kujitolea kwao ni kama fimbo mkononi mwa mchungaji na maiti inayopelekwa isipotaka. Hawa waliupa Upapa nguvu nyingi kupitia shule na vyuo ambako walifunza watoto na vijana kutoa uaminifu wao (wa kimaiti) kwa viongozi wao.

Naam Jesuit ndio champion wakubwa katika baraza la Trento mnamo karne ya 16 wa kutetea kwamba Papa hakosei (infallible) na neno lake ni kama la Mungu au Yesu. Kumpinga au kumkosoa ni kama kumkosoa Mungu au Yesu.

Ulikuwa mchuano mkali sana, maana Waprotestant walidai Neno la Mungu naam Biblia ndio infallible na si Papa. Na kuwa Kanisa linaongozwa kwa msingi wa maandiko na si kwa mabaraza ya maskofu au papa. Jesuit waliinuka kidedea katika baraza la trento na Papa akawatukuza na kuwapa hadhi ya wanajeshi wa kanisa.

Kutokea hapo ukawepo mpasuko mkubwa kati ya Wakatoliki na Waprotestant, na hapo Wajesuit wakaanza njama za kuzuia uprotestant (counter reformation). Maana kama utaruhusiwa kuenea duniani pote Upapa utapoteza nguvu, maana umejengwa katika msingi kwamba wao wamekalia kiti cha Petro mwakilishi wa Kristo duniani na mkuu wa mitume.

Kwahiyo papa anapaswa kupewa heshima za Kristo duniani, hivyo kama Uprotestant utaruhusiwa kuenea basi Ukatoliki na Upapa utakufa. Mara moja majesuit walijieneza kila pande ili kuuzuia uprotestant.

Zingatia kuwa Uprotestant ulianzishwa katika kanuni kwamba Biblia na Biblia pekee ndio mwongozo wa kanisa. Na Rumi yenyewe ilidai kuwa Biblia si yote, mapokeo na Mabaraza ndio mwongozo wa kanisa. Na zaidi uprotestanti ulikanusha mamlaka ya Papa juu ya kanisa na kumpa papa cheo cha mpinga kristo.

Na ukaenda zaidi kupinga uundwaji wa madhehebu yenye kichwa (askofu mkuu) wakidai ni upapa kwa sampuli nyingine. Hivyo wakaanza kutengeneza kanisa kwa kulitoa kwa maskofu na papa na kuliweka katika mikono ya washiriki na Biblia. Jambo hili lilikuwa tanzi kubwa kwa Ukatoliki ambalo lilisababisha wafalme wamuasi papa kwa kuungana na imani ya kiprotestant.

Jesuit mara moja waliingia kazini maana Papa na kanisa walishindwa kuhimili kishindo cha waprotestant, maana hata mbinu za kuwaua zilishindwa kuwasimamisha.Watu Kama Martin Luther, Jonh Knox,John Calvin , Sir Isack Newton (huyu makabrasha yake mengi kuhusu Dini yamefichwa tumeachiwa haya ya physics na Mathematics ).

Waprotestant waliuliwa Sana wengine waliponea chupuchupu , lakini MAJESUIT wakaona mbona tunawaua lakini ndio wanazidi kuinuka

Jesuiti walikuja na mbinu kali si za kuwafutilia mbali waprotestant tena duniani bali kuwageuza kuwa Warumi wa kiroho.

Wajesuit wakaanza kuingia kwenye makanisa haya uyajuayo ,wakiingiza mafundisho yao yale yale kutoka Roma. Mfano Wahitimu wa Degree ya 18 ya Freemason huitwa Rose and Croix hawa ni maalumu kwa kuingiza alama za misalaba ndani ya madhehebu ya kikristo yote uyajuayo.

Huo Ni mfano tu Kuna kikundi Cha kuingiza Ushoga na kumuinua mwanamke makanisani ,(kumbuka campaign ya Ushoga huwa zinaenda sambamba na ile ya mwanamke kuwa juu ya mwanaume)

Tuendelee...

Biblia inaweka mamlaka ya Kanisa mahalia katika mikono ya waashiriki na wazee wa kanisa. (Matendo 20:28).

Lakini kwa ujanja wa Wajesuiti kwa miaka wamefanikiwa na kuweza kuondoa mamlaka ya Kanisa kutoka katika mikono ya washiriki na kuweka katika makao makuu ya madhehebu. Na sasa wakiwa juu ya makao makuu ya madhehebu wanasukuma karibu madhehebu yote ya Kiprotestanti katika mikono ya Vatican.

Wajesuit wanaenda kukamilisha: kusimika Kanisa la kiulimwengu na kuleta mwisho wa Uprotestanti. Unaposoma

"historia ya siri ya Wajesuiti,

"Utaona mfanano kati ya sekta za kidini na kisiasa. Unabii unaonyesha kupenya na kujiingiza kwa Wajesuiti katika serikali na mataifa ya ulimwengu wa kuendesha michakato ya kuharibu historia na kuweka utawala wa kidikteta, na kudhoofisha demokrasia kama vile katika nchi ya Marekani, kwa kuvuruga jamii, Kanisa, siasa, maadili, jeshi, elimu na kuleta machafuko ya kidini ili dunia ipate agizo jipya (kurejesha utawala wa zamani wa kidikteta wa madhabahu).

Leo makanisa yote ya kiprotestanti hata hilo lako unalojivunia kila siku yanaongozwa na makao makuu na yakiwa na kichwa chenye amri au baraza kuu.

Mshiriki hana sauti tena katika makanisa, amelazimishwa kutii kanuni zilizoandaliwa na wakuu na si Biblia. Ukipinga uovu wao utaitwa mkosefu, muasi anayewanyoshea wakapakwa mafuta kidole naam kufutwa ushirika pia.

Ukisoma Isaya 14:12

Utaona maazimio matano ya Lucifer , someni Biblia vizuri jamani ina Siri nyingi

Kuna kauli pale za "NITA" zipo 5, kuna kauli ya nitapanda mpaka pande za kaskazi.

Pande za kaskazi ndipo lilipokuwapo hekalu la Suleiman, na ndipo zinapotokea Dini 3 kuu (Uislamu, Ukristo na Uyahudi). Ukisoma tafsiri nyingine neno lililotumika pale lina maana ya madhehebu.

Kwasasa Uprotestant umesharudi Roma, leo Akifufuka Martin Luther na wanamatengenezo wengine watashangaa Sana harakati walipoziachia zimerudi hatua elfu 10 nyuma.

Kwasasa MAJESUIT wameunda Taasisi inaitwa Eukumen ambayo madhehebu yote yameungana na viongozi wa makanisa , madhehebu hukutana huko.

Ingia kwenye website yao utakuta list ya madhehebu na makanisa likiwepo la wewe unayesoma.
 
Kuna ukweli kny andiko lako Lutheran sheria kwa waumini zimekuwa kali sana tofauti na zamani hasa kupitia jumuia ambazo hapo mwanzo haizikuwepo.
Sasa hivi makanisa yote uyajuayo ,mengine viongozi Ni miungu watu
 
Wapentekoste mnaowaita walokole hawapo huko na hawafungamani na makanisa mengine kama wcc na hapa nchi cct
 
Kuna ukweli kny andiko lako Lutheran sheria kwa waumini zimekuwa kali sana tofauti na zamani hasa kupitia jumuia ambazo hapo mwanzo haizikuwepo.
Makanisan Kuna matatizo makubwa Sana

Hata kwenye Uislamu ndio kabisa
 
FPCT, TAG, EAGT, KLP taja kama kuna majesuit ndani yake tujue
Usibishe kitu Kama hujui , nitaanza na Moja Moja hapo kukuonesha ,Majesuit wameshayateka


Kwanza unajua hao wote uliowataja hapo Juu Wana chama Chao CPCT ,na mwakilishi wao huenda kwenye mkutano na vikao vya eukumen ?

(1.) Makanisa ya TAG;


(2.) Makanisa ya PAGT;

(3.) Makanisa ya VICTORIUS;

(4.) Makanisa ya CALVARY;

(5.) Makanisa ya FGBF;

(6.) Makanisa ya EAG(T);

(7.) Makanisa ya FPCT;

(8.) Makanisa ya RGC;

(9.) Makanisa ya GCCT;
 
Wapentekoste hawachangamani kwenye ibada ambazo makanisa yake yana maejesuiti
Yaani Kama Kuna sehemu wamefanya uchafuzi Basi Ni kwenye haya makanisa yanayojiita Wapentecoste au walokole


Hawa CPCT Wana uongozi wao wa juu kidunia ,hao kila siku hawaishi vikao kwenye umoja wa kuungana na Roma

Pitia hapa kwenye website ya muungano wa makanisa duniani




Huu mfumo ulivyokaa Ni Pyramid shepu

Waliochini Ni WAUMINI ambao mnapokea tu ,waamuaji Ni walio juu
 
The Case of Mackenzie Church and Shakahora Incident.

Kwa sasa tishio la ulimwengu ni Ukristo.
Kuna nchi ukijitangaza kuwa wewe ni Mkristo adhabu yake ni Kifo tu.

Ukikutwa na Biblia ni Kifo.
Hizi nchi zinazidi kuongezeka na ilisha fahamishwa.

Mathayo 10:16
Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.
17 Jihadharini na wanadamu; kwa maana watawapeleka mabarazani, na katika masinagogi yao watawapiga;
18 nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa.
 
Wasabato bana....😂😂😂hivi nyie Wasabato inaonekana adui yenu sio shetani bali Wakatoliki 😂😂😂 kilasiku mnakuja na mapokeo yenu ya kuwaponda Wakatoliki lakini cha kushangaza wanazidi kupata wafuasi wengi duniani kuliko dhehebu lolote la kikristo 😆😆
 
The Case of Mackenzie Church and Shakahora Incident.

Kwa sasa tishio la ulimwengu ni Ukristo.
Kuna nchi ukijitangaza kuwa wewe ni Mkristo adhabu yake ni Kifo tu.

Ukikutwa na Biblia ni Kifo.
Hizi nchi zinazidi kuongezeka na ilisha fahamishwa.

Mathayo 10:16
Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.
17 Jihadharini na wanadamu; kwa maana watawapeleka mabarazani, na katika masinagogi yao watawapiga;
18 nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa.
TAJA hizo nchi tuzijue?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom