Majeruhi wa ajali ya Regia afariki dunia

Majeruhi wa ajali ya Regia afariki dunia

RIP Pauline, mpe hi Regia mwambie tuna mmiss jamvini
 
OMG..rest in peace mama. huu mgomo tuliuunga mkono sasa tunalazimu kutengea maamuzi na kusema sasa basi...tunahitaji suluhisho kwa haraka, serikali na hawa madaktari waache kutunushiana misuli, raia wasiokuwa na hatia wanapoteza uhai. Madaktari pateni moyoni wa huruma mlegeze maamuzi yenu mrudi kazini muokoe maisha ya watanzania/raia wengine wasio na hatia
 
Nahisi Regia (rip) aliona hilo la mgomo wa Madaktari mapema sana, ndiyo maana aliamua kwenda zake moja kwa moja!....asingevumilia kuona hii maneno!
Nakusifu regia kwa uamuzi ule!...RIP dear!

Pole nyingi kwa marehemu huyu!...umetutonesha kidonda kilichoanza kupona!

Duh! hii nayo eti ya great thinker!
 
Mhudumuuuu!serengeti nyingine baridi please!Nimechoka na habari za kunitoa machozi kila uchao!
 
Jamaaaaaaaaaaaaaani!!Bwana alitoa,Pinda,Mponda,Nyoni wametwaa..RIP Mama

Hata JK naye anahusika kwa kuwa kama yeye yupo na hafanyi chochote kutatua mgogoro, au kuwafuta kazi waliopewa dhamana ya wizara ya afya... Uwaziri Mkuu basi na yeye anahusika Moja kwa moja.

Shame shame shame on you "Government for (your relatives)" and no longer Government for the people.


Inauma sana na naomba kuwakumbusha hao wasinziaji wetu pale dodoma. Ni rahisi kufikiri kuwa wakiumwa watapelekwa India lakini wanasahau kuwa kuna case za emergency kama za ajali n.k ambazo humpata yeyote wao wakiwamo na ni budi mwathirika kupata huduma ya haraka (ambayo haiwezi kuwa ya India kwa sababu ya umbali) ili kunusuru uhai!

We haya wee, Mungu wetu anaona yote muyafanyayo na anaweza kuwalipiza kwa haraka kuliko mnavyodhani! We fikiria kwa mfano ..kikao cha bunge kinaisha tarehe 10 Februari, na wote mnategemea kurudi makwenu kwa magari ...je mna uhakika wote mtafika salama bila ajali? na je kama baadhi yenu mkipata ajali mnadhani kuna ndege inayotua Dakawa au Gairo ili ikuwahishe India ukazuie kuvuja kwa damu kabla ya kukupa tiba???? Shauri yenu msije mkasema sikuwaambia.... leo ni tarehe 7 Feb 2012 bado mna siku 2 au 3 za kujirekebisha na kuchukua uamuzi wa busara kabla ya kuvunja kikao ambacho 80% ya wabunge wanaume mlikuwa mmelala huku mkiwawaza vyangudoa mliowachukua usiku. Narejea, mkipata majeruhi ya ajali mtapona tu endapo mtapata huduma ya haraka ya kwanza , na pengine ya pili na mwisho hapo Muhimbili siyo INDIA - aka Apollo.


Mungu Ibariki Tanzania na watu wake wote (isipokuwa wabunge, mawaziri na raisi ) amen

Kila mbunge/ Waziri mwenye sikio na asikie ufunuo ambao unaletwa kwenu na mtanzania mwathirika wa mgomo wa madaktari,

Amen
 
Huu ni wakati wa kusimama na kupigana vita vikakamavu- rais A hsad wa syria.
 
Inasikitisha sana.....r.i.p Pauline!
 
Mama Paulina Myovela alijeruhiwa katika ajali iliyomuua Regia Mtema amefariki dunia Muhimbili,
baada ya kukosa huduma kutokana na mgomo wa madaktari.Na mpaka sasa ndugu wapo Muhimbili
toka asubuhi wakitaka kuchukua mwili wa marehemu wamekwama kupata mwili wa mpendwa wao
kutokana na mgomo wa madaktari.

Matatizo kweli, na asingefariki kama siyo ugumu wa serikali ya kikwete.
 
Back
Top Bottom