ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,279
- 7,681
Wabongo tunaona rahisi kubomoa ghorofa kuliko kuadjust ramani ya bomba!
Wivu mbaya...
Wivu mbaya...
Wabongo tunaona rahisi kubomoa ghorofa kuliko kuadjust ramani ya bomba!
Wivu mbaya...
Mihadarati..a.k.a dawa za kulevya. Nadhani wema ni jina tu la hizo nyumba, angekuwa yule wa bongo muvi ingekuwa ndio stori kila siku kwenye magazeti ya shigongo almaarufu udaku
Sidhani kama kuna wivu mkuu, ukute mwenye hayo maghorofa anashangilia huo mradi unampa pesa, huyo ni obviously atalipwa pesa ya kutosha tu, labda kama alivamia eneo ambalo lilishatengwa kwa ajili ya mradi. Hata wenye mradi ukiona wanakubali kuingia gharama za kumlipa huyo jamaa basi ujue hawana option, yaani hawana eneo lingine la kupitisha, na hapo kwenye hayo majengo ndiyo wanaona nafuu zaidi!
Wema Sepetu?
Mapouder ni madawa ya kulevya
Mkuu Saint Ivuga rudi ufafanue mapouder ndio nini mimi sijaelewa.
Mkuu hapo hakuna cha kulipwa coz bomba la Maji tunayotumia wakazi wa Dar ndo lilipopita;wanataka kubadilisha hilo bomba la zamani na kuweka jingine kubwa kupunguza kero ya maji hapa jijini.
Kwa ufupi,hayo majengo pamoja na mengine ambayo yameshabomolewa ili mradi uanze waliuziwa hayo maeneo na wenyeji ambao wanafahamu kbsa kuwa kuna bomba ka maji kutoka Ruvu limepita chini.Chezea bongo ww!
Unadhani yeye ana bahati mbaya kama akina Masogange?
du! ni movie au mapouder! agent
nashangaa mbaka leo hii polisi na kitengo cha kuzuia dawa za kulevya hawajamkamata na kumuhoji wakati wema hana biashara ya halali yenye kipato cha kumiliki mali hizo.
Wabongo tunaona rahisi kubomoa ghorofa kuliko kuadjust ramani ya bomba!
Wivu mbaya...
Acha tu kuna muarabu jirani na hilo jengo amesema mtu wa dawasco akija kubomoa ghorofa lake basi anampiga risasi ya kichwa na yeye anajimaliza,inauma kuwekeza m za kutosha halafu m2 aje kuvunja bora wa divert hlo bomba kuliko kuyabomoa.
Habari Wana JF,
Majengo ya Wema yaliyopo barabara ya bagamoyo yapo mbioni kubomolewa kupisha ujenzi wa bomba la maji al-mmarufu mradi wa m-canada,bomba ilo linatoka ruvu chini linapelaka maji mji mpywa wa bush.
WEMA BUILDING:TEGETA KWA NDEVU
View attachment 107617
WEMA BUILDING:BOKO BASIHAYA
View attachment 107618
Nawasilisha
Watu wasioelewa wanawalaumu hawa waliojenga magorofa, lakini hawa watu wana building permit.
Kuna kipindi afisa mkuu wa ardhi wilaya ya Kinondoni alisimamishwa kazi muda mrefu sana kwa sababu ya hizi "deal" za kugawa viwanja feki. Walianzisha tabia ya kutengeneza ramani tofauti iliyopo ofisini na hali ilivyo field na hivyo kuhalalisha ugawaji wa hati. Wengine ndio kama hivyo wameuziwa kwenye miradi.
Sasa just imagine hilo jengo likibomolewa ni ajira ngapi zimepotea?
Huu uhuni unatuumiza wenyewe in the end...