Mdomo bakuli
JF-Expert Member
- Jan 7, 2017
- 3,442
- 7,020
Mkuu watu wa kitengo wasingekupa hata chance ya kuandika haya kama kweli walitaka uwe mmoja wao!
imaginativeNikiwa kidato cha tatu mwaka 2008 nilipata rafiki kijana mpole,mstaarabu kweli kweli ambaye alikua anafanya kazi serikalini lakini sikujua hasa ni ofisi ipi alikua anaifanyia kazi mpaka baadaye baada ya miaka miwili akili ilipopevuka kidogo. Kwasababu nilikua nasoma day school jioni nilikua naenda kwake tunakula,kunywa na kubishana story za mpira kidogo. Siku moja nilimpeleka home majira ya usiku saa mbili usiku.
Tulipomaliza kula nilimsindikiza mie nikarud home, ile naingia ndani tu bibi yangu ambaye kwa wakati huo alikua mtumishi kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya kwa takribani miaka 20 aliniuliza kwa mshangao "unaongea nini na watu wa security??" Sikumuelewa nilijua ni complications za bibi yangu maana alikua mtata kweli kweli na kwasababu alinilea tokea mdogo na alinichagulia hadi rafiki wa kuongea nao.
Miaka miwili baadaye nikiwa kidato cha tano siku moja nilirudi toka shule ilikua likizo fupi, nikaenda kwa jamaa yangu kumpa hi bahati mbaya alikua ametoka ila nilipompigia simu alinambia niingie ndani kwan mlango aliegesha na angenikuta hapo baadaye kidogo. Kwenye meza ya chakula kulikua na laptop na baadhi ya documents nilienda kuchukua ile computer ili nichek kama movies zitakuwepo maana nilitoka bweni kuhenyeka na misuli ya masomo nilikua na ukame wa movies.
Nilipoigusa ile PC Nilishtuka nilipoona ujumbe uliokiua kwenye mfano wa emails uliokua unampa jamaa yangu maekekezo ya kumfuatilia kwa kina aliyekua waziri wa miundombinu na uchukuzi kwa wakati huo tena ukimkomandi "haraka sana". Sikujua huyo jamaa ni nani mpaka amfuatilie professor yule, chini ya zile documents kulikua na ID iliyoeyesha jamaa alikua ni nani. Nilikuja kufikiria maneno ya bibi yangu nikachanganya na akili yangu kuwa nilikua karibu mno na "jasusi" la serikali na tokea hapo nikaanza kuwa makini na watu nnaongea nao. Sikuwahi kumuuliza jamaa kitu chochote maana nilianza kumuogopa na nilikua na mtizamo hasi kuhusiana na majasusi
Mwaka 2015 nikiwa namalizia kadigrii kangu siku moja jumamosi saa kumi na mbili hiv asubuhi nilipigiwa simu na watu walijitambulisha kuwa ni ma ofisa kutoka "UTUMISHI" hivyo napaswa kuamka na kwenda chuo ntawakuta wakiwa hapo kwenye bwalo kubwa la mitihani na mikutano ya chuo sikujua wapi wametoa namba zangu maana nilipigiwa kwenye line ya voda ambayo huwa siitumii mara kwa mara na line yangu iliyozoeleka ya tigo niliizima. Mnyamwezi nikajisemea ukisikia "zali la mentali ndo hili" mwezi mmoja kabla ya final exams naitwa interview na serikali?
Nilipofika chuoni nilikuta wajomba wapo na wanafunzi wa kozi zingine kibao, mara nikaona na washikaji zangu sana wawili ambao nilikua nasoma na kuishi nao mtaani wapo. Nikiri kuwa ile interview ilikua ya ajabu ina maswali karibu kitabu cha kurasa 100... nilijiuliza hii ni interview ya namna gani?
Baada ya kumaliza chuo niliamua kubaki town kutafuta life nilijua mkoani kisingekua na fursa za ajira kama hapa town.... huu ndo wakati uliokuwa mgumu kwanuki boom lilikua limekata na mtaani palikua pamoto sana... ilikua kila ikifika jion nakaa kibalazani napiga story na masela niliosoma nao na tukaamua kubaki town kukomaa, miezi 9 ilikua imepita baada ya chuo kuisha, ikumbukwe kuwa katika masela sita tuliokua tunashinda kijiweni jioni wanne tulishiriki kwenye ile interview ya mwez wa sita kabla hatujamaliza chuo.
Kwa wakati ule kijiwe kilikua kinachangamka vibaya mno, tukaanza kupokea wageni tusiowajua ambao baadaye walikuja kuwa washkaji zetu sana kariba ya watu hawa haikutofautiana kabisa na jamaa yule wa miaka ya 2008 niliyowaambia mwanzoni kabisa mwa story hii, walikua washikaji wawili wapole sana, watanashati na wanaonekana kuwa na akili nyingi sana. Maswali yao na hoja zao zililenga kupata ufahamu wetu juu ya masula mbali mbali hasa ya kisiasa na kiuchumi ila hasa mitizamo yetu ya kisiasa.
Nilishindwa kuhisi chochote maana walijitambulisha kuwa wao ni wanafunzi waliohitimu chuo kama sisi ila wao walimaliza Mzumbe university morogoro. Kumbe walikua kazini bwana na kazi yao ilikua ni kuangalia mienendo yetu kabla ya kuitwa rasmi kitengoni wao wanaita "vetting " na hapa palikua pamoto maaana tulinza kuhisi kuchunguzwa kupita kiasi kila nikiamka mara aunt yangu wa mbeya anauliza "kuna watu wananipigia simu kuniuliza kuhusu wewe uliwapa namba yangu?" Kesho yake jamaa yangu niliyesoma nae shule ya msingi darasa la kwanza 1999 hadi darasa la saba 2005 nae anaulizwa ulizwa kuhusu mimi...nikiwauliza washikaji zangu nao ni hivyo hivyo.... hapo tukajua fika kua tulikua chini ya uangalizi wa kitengo....
TUTAENDELEA
NtakutafutaMasuala ya kuleta stori nusu nusu sio poa kabisa.
Siku nyingine jipange ulete kitu kilichokamilika
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Ntakutafuta
Kama alivyotafutwa jamaa
Una faa sana
Avatar tu inaonyesha[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Avatar tu inaonyesha
Ntakuweka kitengo cha ...
Hawa watu wapo mkuu
Mimi niliwakwepa kinoma ...
Haikua dream yangu kufanya kazi huko ingawa nna uchungu sana na nchi yangu
Watu wote walio karibu yangu ..
Ni watu wa huko
.walitaka waniifluence hadi shule ya kusom a
Looh .. Nikaona upumbav niende kutetea maccm yabak madarakan
... Mbinu nlizotumia siri yangu ...
.ila aaahahaha aisee
Mmoja nkamwambia labda .. TFDA ..
Ilikua zaman nikiwa form five[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Kama ni TFDA mkuu na mimi napamind sana, usinisahau aisee ukipata dili
Hakuna siri yoyote hapo mbona kawaida tu na mimi siku moja nitakuja kuelezea safari yangu kutoka skauti,jkt mpaka RTSUsiendelee unifichua siri za nchi unaifanya kazi ya hao jamaa kuwa ngumu iwapo unatoa siri jinsi wanavyofanya kazi.
Poa poa mkuu.Ilikua zaman nikiwa form five
Nshapotezea ...
Tanzania dah ...
Pambanen wakuu ...
Mimi ngoja ntafute maarifa zaidi
Nivunje rekodi ya yule jamaa aliyechukua phd ana miaka 30