Majaribu ya wanawake kwa wanaume kuona kama wanafaa kimapenzi mara nyingi hutoa majibu ya uongo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,279
Wanawake huwa wanawajaribu wanaume kwa majaribu fulani ili waweze kujua kama wanaume hao wanafaa kuishi nao, bila ya kupima au kufanyia utafiti kama hayo majaribu wanayoyatumia kama yapo ndani ya uwezo wa wanaume husika wanaojaribiwa,

Hasara za kufanya hivi kwanza ni vigumu wewe mwanamke kugundua kama unadanganywa au lah! kwa sababu ni vigumu kujua uhalisia wa maisha ya mwanaume unayemjaribu.

Pia inaweza kupelekea ukawapoteza watu muhimu katika maisha maisha yako kwa sababu huwezi kutumia vigezo vinavyofanana kwa watu tofauti ambao wana maisha tofauti. Mfano swala la no sex before marriage si kila mwanaume anaweza kulikubali hivyo ni vibaya kutumia kigezo hicho kuwapima wanaume wawili au watatu tofauti na kuamini kwamba anayevumilia ndiye anayekufaa.

Pia kuna mwanamke anamjaribu mchumba wake labda amnunulie kitu fulani cha gharama lakini mwanaume kwa wakati huo anakuta ana majukumu mengine kama kujenga. Endapo mwanaume akishindwa kutimiza anaonekana hafai na kukimbilia kwa mwingine ambae anaweza kumpa hivyo vitu vya starehe ya muda na kumuacha mwanaume potential ambaye labda angevumilia wangefanya maisha pamoja....

Nawasilisha and nafungua milango ya kukosolewa na kuwa na mawazo tofauti na yangu ila milango ya matusi imefungwa..........
 
Wanaume wa siku hizi hawafanyiwi majaribio ... Unajaribh mwenzio anafanya .. Kama kulikuaga na kamtindo ka kumwambia rafiki ako amtongoze mpenzi wako uone kama ana msimamo hahhaha enzi za wajerumani walikua wanavunga ila sasa hvi yaani shoga akimbeep tu jamaa ndio anashughulikia mtongozo ... Utaambulia kilio na majuto
 
Iyo no sex before marriage hapana aiseeh ....je kama k ni zile kama za werevaa ..?......
 
TOKA ALIVYONIOMBA HELA NIKAMUAMBIA SINA NDIPO UHUSIANO WANGU ULIVYOVUNJIKA KWA YULE DADA,TENA ANANICHUKIA VIBAYA MNO JAPOKUWA AMEAJIRIWA SERIKALINI LAKINI YEYE KILA MUDA NI SHIDA TU
 
Dah kama mimi sipendi kabisa kuzungushwa na demu, yaani ukiniletea zile pozi za kukutongoza leo unikubalie mwakani jua utapoteza bahati.Nipo bize mbaya siwezi kukufuatilia kwa muda mrefu lkn mapenzi ya kweli ninayo
 
Back
Top Bottom