Nyleptha
Member
- Jun 19, 2012
- 69
- 47
Amekuja kwangu akiwa na sura ya huzuni na majonzi tele, nikajua ana tatizo kubwa, nikaketi kumsikiliza habari aliyojia;
Ni mwanamke ameolewa miaka michache iliyopita yaani ndoa yao bado changa tu, ameajiriwa katika kampuni fulani binafsi wanamlipa mshahara wa kutosha kubadili mboga, mumewe alipata uhamisho kwenda mkoani kikazi kama mwaka tu umepita, wakapiga mahesabu wana miradi na wamejenga nyumba yao hapa, kipato chao ni cha kawaida tu hivyo wakaona mke aendelee na kazi hapa hapa ila mume ndio aende mkoani kusaka maisha halafu mume akipata nafasi atakuwa anakuja na mke anaweza kwenda pia.
Baada ya mume kuondoka mke ameendelea na maisha kama kawaida, ila TATIZO limeanzia pale ambapo rafiki yangu huyu amejikuta anavutiwa sana na mwanaume mmoja ambaye anakaa maneneo ya karibu na nyumbani kwake na mara kadhaa amekuwa akimkuta njiani na kumpa lifti na kuongea mawili matatu ya maisha. Kadiri siku zinavyokwenda anazidi kumpenda mwanaume huyu ambaye pia ni mume wa mtu! Hajui afanyeje kuepuka hali hii kwani ni mtu ambaye familia zao zimeshazoeana si rahisi kukatisha mahusiano ghafla kutaleta maswali sana, hawezi kuhama mtaa wala kubadili njia ni hiyohiyo moja, na wakati mwingine usafiri ni wa shida balaa inabidi tu akubali hiyo lifti. Huyo mwanaume hajaonyesha dalili yoyote ya kumzimikia rafiki yangu huyu wala kumtongoza, ni mdada tu ndio amempenda/tamani)!
Nimemshauri akae mbali na huyo jamaa na pia ajitahidi kwenda kumuona mumewe au amwambie mumewe aje haraka kuokoa jahazi, hayo yote ni majaribu tu kwa kuwa hajamuona mumewe siku nyingi! dada wa watu anasema hafikirii kumsaliti mumewe hata siku moja kwahiyo ndio anatafuta jinsi ya kukimbia jaribu hilo, anatamani apate wasaa amwambie ukweli, kitu ambacho naona si sahihi kwani anaweza akadraw attention ya huyo jamaa na kumfanya nae amuwazie kimapenzi na matokeo yake anaweza kumuweka katika majaribu zaidi wakafanya usaliti ktk ndoa zao.
Nimetoa ushauri kwa wengi lakini hili nimepungukiwa nondo, niongezeeni maoni yenu wadau! nimsaidieje huyu dada?
Ila ujumbe nilioupata hapa ni kwamba tusiache wake zetu mbali, sijui iwe ni kwa sababu gani lakini tufikirie marambili, pia kama mke yuko ktk hali hii je mumewe huko yuko ktk hali gani? anayashindaje majaribu? nimejiuliza sana.