Mwili wa askari wa TANAPA aliyepotea porini Kigosi, umepatikana ukiwa umeteketezwa kwa moto

Hjalte

Member
Oct 20, 2023
25
100
Askari wa TANAPA ambae niliweka taarifa ya kudaiwa kuuawa na kundi la wafugaji katika Pori la Kigosi wilayani Kahama mkoani Shinyanga, Julius Katambi, mwili wake umepatikana akiwa ameuawa na kisha kuchomwa moto ndani ya pori hilo.

Katambi alikwenda kukamata mifugo ya wafugaji katika pori hilo Oktoba 20, 2023 akiwa na mgambo wawili, ambapo baada ya kuwakamata wafugaji na mifugo yao porini humo, walimuomba kuteta naye pembeni ili asiwakamatie mifugo yao na baada ya muda wakiwa wanateta, ulisikika mlio wa risasi, uliofanya wenzake (mgambo) kukimbia kujiokoa na hakupatikana tena hadi jana jioni Oktoba 31 ambapo mwili wake ulipatikana ukiwa umeteketezwa kwa moto pamoja na silaha aliyokuwa nayo.

Wafugaji kadhaa wanashikiliwa na Vyombo vya Dola wakihusishwa na mauaji ya askari hiyo.

--- ----- ----

Awali, wakati ilipotoka taarifa ya kupotea kwa askari huyo, Jamii Forums ilipowasiliana na Uongozi wa TANAPA kupitia kwa Kaimu Kamishna wa Uhifadhi kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Juma Kuji, kuhusu ukweli wa taarifa hizo, hawakupatikana kutoa ufafanuzi.

Alipotafutwa Afisa Uhifadhi Mwandamizi Kitengo cha Mawasiliano TANAPA, Catherine Mbena na kuulizwa juu ya taarifa hizo awali naye alisema “Nitakurudia”, baada ya hapo hakutoa ushirikiano.

Taarifa ya awali ya kupotea kwa Askari huyo hii hapa - Askari wa TANAPA apotelea porini, ahofiwa kuuawa na wafugaji na kuzikwa
 
Back
Top Bottom