Majambazi yaua watano Manyara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majambazi yaua watano Manyara

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jun 8, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Mussa Juma na John Dotto, Arusha

  WATU watano, wameuawa kwa kupigwa risasi baada ya gari walilokuwa wamepanda kutekwa na kundi la majambazi katika kijiji cha Sunya, Kata ya Sunya Wilaya ya Kiteto, mkoani Manyara.

  Majambazi hao waliokuwa zaidi ya matano, walifanikiwa kupora mamilioni ya fedha kutoka kwa watu waliokuwa katika gari hilo ambao wengi wao ni wafanyabiashara wa mitumba na mifugo wilayani Kiteto.

  Tukio hilo la aina yake lilitokea juzi majira ya saa 1:30 jioni, baada ya majambazi hao waliokuwa na silaha za moto na za jadi, kufunga barabara kwa majabali na kuteka gari hilo lililokuwa na wafanyabiashara waliokuwa wanaelekea katika mnada kijiji cha Mutura.

  Kamanda wa polisi mkoani Manyara, ACP Parmena Sumari alithibitisha jana kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa kikosi cha askari tangu juzi usiku kilitumwa kufuatilia tukio hilo.

  "Ni kweli majambazi yalivamia hilo gari na yameuawa watu watano, wanawake wawili, wanaume wawili na mtoto mmoja na bado tunafuatilia juu ya majina yao na namba za gari, "alisema Sumari.

  Kamanda Sumari alisema katika tukio hilo watu wengine watano walijeruhiwa kwa risasi na hadi jana walikuwa wamelazwa katika kituo cha afya cha Sunya wilayani Kiteto.

  Kamanda huyo, ambaye alieleza yupo safarini, alisema hadi jana mchana bado alikuwa hajapata taarifa kamili na aliwataka waandishi wa habari hizi kuwasiliana na msaidizi wake ambaye hata hivyo naye alisema bado hana taarifa kamili.

  Mkuu wa wilaya ya Kiteto, Frank Uhaula alithibitisha jana kutokea mauaji hayo katika wilaya yake na kueleza kuwa uchunguzi na msako wa watuhumiwa wa tukio unaendelea.

  Afisa Mtendaji wa kata ya Sunya, Charles Adola alisema kuwa hadi jana mchana walikuwa bado wakiendelea na msako na bado utambuzi wa waliouawa ulikuwa unaendelea.

  Adola alisema kabla ya majambazi hayo hayajaua, yalipiga risasi kadhaa hewani kulazimisha gari kusimama na liliposimama, waliwauawa watu hao na kuwajeruhi wengine huku na kupora fedha na mali nyingine.

  Tukio hili ni mfululizo wa matukio ya ujambazi ambayo yameanza kuibuka tena katika maeneo mbali mbali hapa nchini.Majambazi yaua watano Manyara
   
 2. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2010
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Poleni woote ndugu mliofikwa na matatizo na lio hospital
   
 3. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Jamani ubinadamu hakuna kabisa siku hizi! Sasa kitoto nacho kina hela gani mpaka wakiue! MUNGU atawalipa waliofanya haya kwa wakati wake! Poleni ndugu zetu na MUNGU azilaze pema roho za marehemu: Amen
   
 4. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Mi tatizo langu ni hawa polisi. Why on political related issues nguvu inakua kubwa kuhandle situation lakini kufuatilia majambazi inakua issue. Ebu bwana UWT anzeni kutulinda wa TZ mna mtandao mkubwa mnachoshindwa kufuatilia source of income ya watu subject to what they are doing toka ngazi ya kijiji ni nini? :angry: :angry: :angry: :angry: :angry: Tutaishia kupeana pole na kujazana ujinga, jana tu uwanja wa taifa after the match vibaka wanajigawia watu while Kova sijui alikua wapi while prior of the match alitangaza kutakua na vikosi kazi zaidi ya vinne na karandingas, sasa vibaka walikotoka ni wapi?
   
 5. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  inasikitisha sana..huku unasikia polisi waua raia,.. kule majambazi yaua raia..kwingineko raia wachoma moto kituo cha polisi..ukizama mitaani huko ndo ...raia waua kibaka... duh, mungu rehemu.
   
 6. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Katika yote wanaiba then wanaua tena na mtoto asiyejua hili wala lile? Vichwa hivi vinaongozwa na ushetani utokanao na madawa hususani bangi. Tanzania tumebaki kuishi kwa hofu mno kila kukicha. Tutapataje maendeleo na kupunguza umaskini wa kipato kwa familia kama kila kidogo unachohangaikia kinakuja kuchukuliwa tena si kwa amani bali kwa mtutu wa bunduki na vifo. Tusaidie Ee Mung wa Rehema.
   
Loading...