Hata Mimi naungana na Wewe kwasababu zifuatazo;
1. Hakuna mzigo wa thamani kiasi hiko usafirishwe unclassified..... Info zimekuwa leaked kimakusudi kabisa.
2. Na kubwa ni kwambazi huwa hawabakishi kama walivyofanya hao coz wamechukua 15kg kati ya kg Zaidi ya 30 zilizokuwa zinasafirishwa.
Watu wenye silaha wavamia gari, kupora Kg 15 za madini ya Tanzanite yenye thamani ya Sh10 bn usiku wa kuamkia leo Manyara, Polisi athibitisha.
Chanzo:Mwananchi
================
WATU wanaosadikiwa ni majambazi wamepora madini ya tanzanite ya Kampuni ya TanzaniteOne ya Mirerani, wilayani Simanjiro, mkoani Manyara yenye uzito wa kilo 40 na thamani ya zaidi ya Sh bilioni 10.
Taarifa kutoka katika kampuni hiyo zilisema, uporaji huo ulitokea jana ndani ya kampuni hiyo saa tisa usiku.
Kwa mujibu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Dauglas Swartz, tayari wafanyakazi watano wa kampuni hiyo wanashikiliwa na polisi katika kituo kidogo cha Mirerani kuhusu wizi huo.
Alisema jana kwa njia ya simu kuwa, Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Manyara (RCO), Benedict Msuya alifika eneo la tukio kwa uchunguzi wa wizi huo.
"Ni kweli tumeibiwa madini ya tanzanite na baadhi ya wafanyakazi wanaodaiwa kuhusika katika tukio hilo wameshakamatwa na upelelezi bado unaendelea, niache kwa sasa,'' alisema mkurugenzi huyo.
Taarifa zilizopatikana ndani ya kampuni hiyo zinadai kwamba madini hayo yaliyokuwa yamefungwa katika mifuko miwili tofauti yenye uzito wa kilo 15 na kilo 25 na yameporwa mita chache kutoka mgodini eneo la kuingia chumba cha ulinzi.
Hata singha singha wa Escrow akaunti tunaambiwa anavigezo vyote.Lost society....Jamii iliyopotea..Yaani hakuna hata mmoja so far aliyeona ujambazi na ujangili ni jambo baya???Je kama aliyeporwa ni mmiliki halali na ana vigezo vyote???Naioenea huruma nchi yangu hii.Kuiacha katika mikono ya vijana ambao kuiba na ujambazi ndio unashibikiwa na kushangiliwa!Mwishowe, mtaanza kuvamiana wenyewe kwa wenyewe.Nyerere aliwaita WaKenya "Manyang'au" kumbe manyang'au ni Watanzania!Aibu tupu ..... Totally disgusting!
Mkuu kwa dhamani ya mzigo jamaa waliopiga kazi nimewakubali
Hiyo dili imesukwa na magaidi sio majambazi
Inaweza kuvunja rekodi ya kasusura!
![]()
Madini ya tanzanite ya Kampuni ya TanzaniteOne ya Mirerani, wilayani Simanjiro, mkoani Manyara yenye uzito wa kilo 40 na thamani ya zaidi ya Sh bilioni 10 yameporwa na watu wanaosadikiwa ni majambazi.
Taarifa kutoka katika kampuni hiyo zilisema, uporaji huo ulitokea jana ndani ya kampuni hiyo saa tisa usiku.
Kwa mujibu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Dauglas Swartz, tayari wafanyakazi watano wa kampuni hiyo wanashikiliwa na polisi katika kituo kidogo cha Mirerani kuhusu wizi huo.
Alisema jana kuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Manyara (RCO), Benedict Msuya alifika eneo la tukio kwa uchunguzi wa wizi huo.
Ni kweli tumeibiwa madini ya tanzanite na baadhi ya wafanyakazi wanaodaiwa kuhusika katika tukio hilo wameshakamatwa na upelelezi bado unaendelea, niache kwa sasa,
Taarifa zilizopatikana ndani ya kampuni hiyo zinadai kwamba madini hayo yaliyokuwa yamefungwa katika mifuko miwili tofauti yenye uzito wa kilo 15 na kilo 25 na yameporwa mita chache kutoka mgodini eneo la kuingia chumba cha ulinzi. -- via HabariLeo
Hapa mimi napata wasiwasi inamaana kama Kilo 40 tu ni Bilioni 10/= Je Tanzania inazalisha Kilo ngapi za Tanzanite kwa mwaka? Maana kama Kilo 40= 10Bilioni sasa Tanzania ingetakiwa hata South Africa tumeshawapiga Bao Kiuchumi Kupitia tu Madini Haya.
Hivi Gold na Tanzanite ip ipo juu? Bcoz kg 25 za Gold haiwezi kizidi 3 bn. Kwa bei ya 1gm for 60,000 Tsh.
Hii ni production ya muda gani? siku moja?mbili?au....!
Mkuu ulikuwa na ubia kwenye hiyo kampuni? Hizi kampuni ndo zinafisadi raslimali zetu kwa ushirikiana na akina Balozi Ami Mpungwe, acha watu wapige mzigo bwana alaaaa! Fedha za ESCROW account wamesema hazikuwa za serikali, zilikuwa za watu binafsi, na sisi tunachojua Tanzanite One siyo kampuni ya serikali ni ya watu binafsi wezi fulani hivi. Kwa hiyo safi sana hayo majamaa yaliyofanikisha hiki. TUMEDHLUMIWA KIASI CHA KUTOSHA, TUMEIBIWA KIASI CHA KUTOSHA NA TUMEPUUZWA SANA!!!Lost society....
Jamii iliyopotea..
Yaani hakuna hata mmoja so far aliyeona ujambazi na ujangili ni jambo baya???
Je kama aliyeporwa ni mmiliki halali na ana vigezo vyote???
Naioenea huruma nchi yangu hii.
Kuiacha katika mikono ya vijana ambao kuiba na ujambazi ndio unashibikiwa na kushangiliwa!
Mwishowe, mtaanza kuvamiana wenyewe kwa wenyewe.
Nyerere aliwaita WaKenya "Manyang'au" kumbe manyang'au ni Watanzania!
Aibu tupu ..... Totally disgusting!
Haya majamaa ndo yanajua kazi siyo kuja kutukaba sisi makapuku huku mitaani wakati mafisadi wanakwiba madini yetu! Kama MUNGU ataweza kuyakinga haya majamaa na afanye hivyo, maana ndo yatakuwa yameuaga ujambazi na kwenda kuwekeza vitu vya maana! Sisi huku kwetu kulikuwa na jambazi sugu la wizi wa magari enzi hizo, baada ya kupiga mpunga wa kutosha likaachana na hiyo kazi na kuwekeza. Sasa hivi ni moja wa matajiri wanaofisadi wakulima kwenye kilimo cha pamba maana lina mashine za kuchambua pamba za kutosha!!!
Kwa hiyo na hii mijamaa kwa huo mpunga lazima yatawekeza kwenye vitu vya maana na kupanua wigo wa ajira. Huu mzigo ulikuwa unasafirishwa kwenda nje sisi tusingeambulia chochote hapo.
Wito kwa majambazi wote, hamieni kwenye migodi ili raia tupumue!!!
Hivi mkuu kesi ya Kasusura iliishia wapi? Hivi zilikuwa dola milioni 2 au 200?
Mkuu usicheze na kitu inaitwa tanzanite
Huwezi kufananisha bei yake na Gold hata chembe
Hao jamaa kama walikuwa watatu basi wasipokamatwa umasikini kwao itabaki historia!!!
Duh aisee are you sane?