Majambazi yapora Tanzanite ya billion 10

Majambazi yapora Tanzanite ya billion 10

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
Watu wenye silaha wavamia gari, kupora Kg 15 za madini ya Tanzanite yenye thamani ya Sh10 bn usiku wa kuamkia leo Manyara, Polisi athibitisha.
Chanzo:Mwananchi

================

WATU wanaosadikiwa ni majambazi wamepora madini ya tanzanite ya Kampuni ya TanzaniteOne ya Mirerani, wilayani Simanjiro, mkoani Manyara yenye uzito wa kilo 40 na thamani ya zaidi ya Sh bilioni 10.


Taarifa kutoka katika kampuni hiyo zilisema, uporaji huo ulitokea jana ndani ya kampuni hiyo saa tisa usiku.


Kwa mujibu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Dauglas Swartz, tayari wafanyakazi watano wa kampuni hiyo wanashikiliwa na polisi katika kituo kidogo cha Mirerani kuhusu wizi huo.


Alisema jana kwa njia ya simu kuwa, Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Manyara (RCO), Benedict Msuya alifika eneo la tukio kwa uchunguzi wa wizi huo.


"Ni kweli tumeibiwa madini ya tanzanite na baadhi ya wafanyakazi wanaodaiwa kuhusika katika tukio hilo wameshakamatwa na upelelezi bado unaendelea, niache kwa sasa,'' alisema mkurugenzi huyo.


Taarifa zilizopatikana ndani ya kampuni hiyo zinadai kwamba madini hayo yaliyokuwa yamefungwa katika mifuko miwili tofauti yenye uzito wa kilo 15 na kilo 25 na yameporwa mita chache kutoka mgodini eneo la kuingia chumba cha ulinzi.
 
Tanzanite ya 10b inasafirishwa usiku??!!!!

Kwanini majambazi hawakuwachinja kabisa wenye mzigo ili iwe fundisho kwa wengine???!!!

Mkuu kwa dhamani ya mzigo jamaa waliopiga kazi nimewakubali
Hiyo dili imesukwa na magaidi sio majambazi
Inaweza kuvunja rekodi ya kasusura!
 
Naomba kujua kwani huo mzigo ulikuwa wa nani?
Ilikuwaje mzigo mkubwa namna hiyo ukasafirishwa usiku ? kama si magendo ni nini?
 
Watu wenye silaha wavamia gari, kupora Kg 15 za madini ya Tanzanite yenye thamani ya Sh10 bn usiku wa kuamkia leo Manyara, Polisi athibitisha.
Chanzo:Mwananchi
Hivi Gold na Tanzanite ip ipo juu? Bcoz kg 25 za Gold haiwezi kizidi 3 bn. Kwa bei ya 1gm for 60,000 Tsh.
 
Usijekuta kuna inside job maana walijuaje kuna mzigo na thamani. je kulikuwa na police escort
 
Mkuu kwa dhamani ya mzigo jamaa waliopiga kazi nimewakubali
Hiyo dili imesukwa na magaidi sio majambazi
Inaweza kuvunja rekodi ya kasusura!
Unajua mkuu kuna kesi ukiambiwa hata kama ni mpelelezi ataishia kula hela ya aliyeibiwa na aliyeiba tu, maana kila akinusa anakula bingo na mwisho naye watamuua though!!!

Lakini pia kama ni mzigo wa watu zaidi ya mmoja amini hiyo ni "inside job"
 
Hivi Gold na Tanzanite ip ipo juu? Bcoz kg 25 za Gold haiwezi kizidi 3 bn. Kwa bei ya 1gm for 60,000 Tsh.

Mkuu usicheze na kitu inaitwa tanzanite
Huwezi kufananisha bei yake na Gold hata chembe
Hao jamaa kama walikuwa watatu basi wasipokamatwa umasikini kwao itabaki historia!!!
 
Dah afadhali labda mzunguko wa pesa utatupitia na sisi watu wa hali ya chini.Ningefurahi zaidi kama mzigo ulioibiwa ungekuwa ni wa makaburu,sababu wanajiona wao Miungu watu ,wameinyonya sana Mererani na Tanzanite yake bila kufanya maendeleo yoyote shenz type,mmxxuuuuuuuuuuuuuuu
 
SAFI! Mnatuibia madini yetu huku tunaona hivi hivi.., atleast hao kama ni wabongo wanaweza kwenda kusaidia ndugu zao.., kama sio waTanzania basi potelea pote..! mrahaba 0.00002% maana yake nini kama sio kututukana wabongo na kutufanya hatuna akili..??!
 
Hivi Gold na Tanzanite ip ipo juu? Bcoz kg 25 za Gold haiwezi kizidi 3 bn. Kwa bei ya 1gm for 60,000 Tsh.

Pamoja na kwamba namna ya upimaji ni tofauti, vito siku zote ni gharama mkuu...

Fanya tu utafiti mdogo wa kutembelea maduka ya sonara na ulinganishe bei ya pete yenye kito cha Tanzanite na pete yenye madini ya dhahabu...
 
Hivi Gold na Tanzanite ip ipo juu? Bcoz kg 25 za Gold haiwezi kizidi 3 bn. Kwa bei ya 1gm for 60,000 Tsh.

Aaaanh mkuu unaongelea dhahabu hizi watu wantunzana kwenye ngoma tu uzaramoni kwa wajomba zangu!!!!!

Humu tu uliza kina mama wanaomiliki Tanzanite iwe kwenye pete,kidani au hereni utajua shughuli yake!!!!!
Au wanaume waliowahi wanunulia vitu hivyo akina mama pia waweza pata taswira!!!
 
Back
Top Bottom