Majambazi ya manzese kumbe ni wanajeshi

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,144
ndugu zangu polen na pilika pilka za kufurahia uapishwaji wa RAIS mteule wa DUNIA B.H.OBAMA, kwa masikitiko makubwa hivi majuzi kuna majambazi yalivamia gari na kutaka kupora pale MANZESE,nadhan mlio nje mnapakumbuka sana wakati wa kufanya shopping kuja huko,,kwa sasa imebadilka kidogo...wakati wa tukio tulikuwa umbali kidogo lakini mbele ya gari letu kulikuwa na DEFENDER la POLISI,wale majambazi wakasimamisha magari mengi tu ile defender ikaamua kupita pembeni na ndipo ilipokuta wanaume wa shoka wametanda barabara nzima gafla ilipita pikipiki yenye askari wawili wenye silaha....kwa kweli yaliotokea nilikuja jamvini kuyaanika nikakuta mh mmoja ametoa taarifa...ila aliacha mambo mengi sana ya aibu kwa jeshi letu

1)GAFLA BINDUKI RASHASHA ZILIANZA KURUNDIMA KUMBE WAZEE WA DEFENDER WALIANZA KUTUNUKIWA NISHANI YA RISASI NA WAO KUENDELEA KUJIBU,,ILIPOFIKA ILE PIKIPIKI KWA KWELI TULIOKUWEPO TULICHEKA NA BAADAE KUSIKITIKA WALICHOFANYA NI KUKATA KUSHOTO NA KUSIMAMISHA KWA MBALI PIKIPIKI KWENYE DUKA MOJA LA PUMBA NA KUINGIA NDANI KAMA WAKIWA WANASIKILIZIA nini kimeendelea, hatimaem askari waliokuwapo kwenye defender baadhi wakala kona nao na kumuacha polisi mmoja ambae aliamua kuendelea kufyatua huku wengine 5 wakiwa pembeni mwa bar wameacha SILAHA KWENYE GARI...hakuna alie amini hili ila afande kova jitahidi kufwatilia..yule aliebaki alipunyuliwa risasi pembeni ya kicha akaendelea kukomaa wakaamua kukimbia na kuacha ile gari yenye fedha.....
muda wakiwa wanarushiana mmoja wao akapigwa bastolla mguuni akakimbia nayo hivyohivyo wakapora gari la mtu aliekuwa akipaki wakakimbia nalo mpaka mitaa ya tandale wakapora lingine na hakuna askari alieendelea kuwafwata

YALIYOJIRI

baada ya kufanikiwa kukimbia ,askari waliichukua na kuipeleka pale kituoni kwao mjini kati,walipoiangalia kwa makini kova akisaidiana na wenzake wakaitambua ni ya JESHINI...akapigiwaa mkuu wa lugalo kuna mzigo wako naomba uje kuuutambua,,walipofika wakakuta kweli iko na alama za jeshini..wakachukua zile namba wakaenda sehemu ya kuifadhia silaha kuangalia nani alikuwa mhusika ama alipewa kuitumia..ikakutwa ni kati ya silaha ambazo hazitoki mara kwa mara kwa hiyo wakaapata shida mpaka waliaongalia tena wakakuta ni katika zile silaha zisizotumika mara kwa mara, baaada ya hapo mku akaamuru kitengo kizima cha kuhifadhi silaha weka ndani,,wakapewa shurba tashnati kabla ya mhusika aliekuwa akilinda siku hiyo kusikia akaama na nyumbani kabisa na mpaka leo aijulikani alipo,

KASHESHE

yule alieumia alienda hospital moja kule vingunguti,walipofika wakaomba atibiwe bila pp3,wakala hela nyingi tu lakini akatokea nurse mstaarabu akapiga simu polisi kuna mtu ameomba kutolewa risasi hapa,,wakaja polisi wakamchukua walichoenda kumfanya anajua mwenyewe ndipo alipotaja yeye ni koplo wa lugalo,,alipewa silaha na aliekuwa zamu siku hiyo akataja na jina kumradhi chanzo chetu kimelisahau kidogo....mpaka hivi sasa anashikiliwa jeshini lugalo:

Nimeona nieleze ukweli huu ili tujiulize kama wanajeshi wanaotulinda ndio wanatuadhibu hivi kwa silaha rashasha kama hizi nani atkaetulinda

JE mh KOVA kukaa kimya hamuoni mnaitia aibu JESHI lenu ukiacha Kukimbia kwenye tukio

Swali lingine najiuliza iweje wale polisi walikimbia mapema ama walikuwa wanawajua wale ni wanajeshi

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Sasa wanajeshi (JW) kujihushisha ktk wizi na tabia inaanza au mshahara kidogo? Hivi mwanajeshi kima cha chini anaanza na shs ngapi?
 
Sweet,

Hadithi yako tamu kweli lakini ungeisoma mwenyewe kwanza kabla ya kupost maana hayo matypos si mchezo
 
Sweet,

Hadithi yako tamu kweli lakini ungeisoma mwenyewe kwanza kabla ya kupost maana hayo matypos si mchezo


Tumshukuru mtoa taarifa, wengi si wajuzi wa kutumia kompyuta au waandishi fasaha. Cha msingi ujumbe umeeleweka.

Hii inatisha wala si kitu kigeni. Inaelekea watunza siraha kwenye majeshi yetu si waaminifu.

Nakumbuka tukio jingine la kutisha lililosemekana kuhusisha wanajeshi ni lile la uporaji wa fedha za NMB pale kwenye mataa ya Ubungo!!. Watu wawili akiwemo askari polisi walipoteza maisha na pesa nyingi (zaidi 150M) kuibwa.

Wanajeshi walihusika na kukamatwa. Hii kesi kimya wala hitajwi, imeishia wapi??????
 
Haishangazi na wala si mara ya kwanza kwa wajeshi kutuhumiwa na ujambazi. Asilimia kubwa ya majambazi ya kutumia silaha ni wanajeshi (aidha alifukuzwa, kastaafu, au njaa na ya kutumia mafunzo vibaya). Nikisema wanajeshi yaani wooote JWTZ, Polisi, Magereza, KMKM, FFU etc).

La maana ni kujadili tatizo nini kwa wajeshi kujihusisha na njia zipi za kisasa za kuzuia uvamizi kama huo.
 
Mhh doubts! wakati wanaiba manzese ulikuwepo au chanzo chako kilikuwepo, silaha zilipopelekwa central ulikuwepo, zilipogundulika kuwa ni za lugalo ukaenda kufuatilia wanahusika walivyo adhibiwa, unapajua nyumbani kwa mtunza gala na unajua kama halali kwake kubwa zaidi unajua hospitali ambayo mwizi/askari aliyejeruhiwa alijaribu kutibiwa na pia unajua kuwa alijaribu kuwahonga wauguzi. SASA NDUGU YANGU WEWE UNAYEFUATILIA YOTE HAYA KWA UKARIBU WOTE HUU NI NANI? AU UNAKITU UNATAKA KUTUFAHAMISHA ILA UNATUZUNGUKA TU?
 
Kwa hiyo wanajeshi ni 'Mijambazi'
mbona haina shabaha sasa??? Anakamatwa na polisi, ingekua vitani ingekuaje???
Wakulu Tz ina majeshi mengi tuuu, wana kazi gani mbona hatusikii research zao? Vita hamna, Jeshi kuuuuuubwa, mnawapa mishahara midogo. Wana skills lakini hawazitumii.
What do u expect????
 
Chanzo chetu inawezekana kikawa kinatokea kituo cha polisi kati,na kinafahamu kwamba polisi wameamua kulinyamzia hili ili kulinda jeshi letu la wananchi na kashfa hii nzito.ndiyo maana mtoa mada ambaye anaonekana kuwa na taarifa yote ameweza kuelezea matukio yote kinagaubaga. Tunashukuru kwa taarifa yako nafikiri ipo haja ya hatua kali kuchukuliwa dhidi ya wanajeshi wetu wanaojihusisha na vitendo visivyoendana kabisa na maadili mema na kiapo walichoapa wakiwa wanavalishwa magwanda yetu. Pia nafikiri suala la kuwaweka makambini askari wetu ni muhimu si tu kwaajili ya nidhamu lakini pia linapunguza uwezekano wa askari wetu kujitumbukiza katika matukio kama haya.
 
Chanzo chetu inawezekana kikawa kinatokea kituo cha polisi kati,na kinafahamu kwamba polisi wameamua kulinyamzia hili ili kulinda jeshi letu la wananchi na kashfa hii nzito.ndiyo maana mtoa mada ambaye anaonekana kuwa na taarifa yote ameweza kuelezea matukio yote kinagaubaga. Tunashukuru kwa taarifa yako nafikiri ipo haja ya hatua kali kuchukuliwa dhidi ya wanajeshi wetu wanaojihusisha na vitendo visivyoendana kabisa na maadili mema na kiapo walichoapa wakiwa wanavalishwa magwanda yetu. Pia nafikiri suala la kuwaweka makambini askari wetu ni muhimu si tu kwaajili ya nidhamu lakini pia linapunguza uwezekano wa askari wetu kujitumbukiza katika matukio kama haya.

kuna gazeti nimelisoma leo linaeleza kwamba Rais Kikwete amewapandisha vyeo maafisa wa polisi waliopigana kiume katika wizi huu wa Manzese. Hafla hiyo ilihusisha pia kumtunuku nishani ya heshma ya utumishi wa muda mrefu, utii na utendaji kazi mzuri afande Kova. IGP alimuwakilisha mhe Rais.
 
Back
Top Bottom