Majambazi waendeleza ubabe

Majambazi waendeleza ubabe

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
15,203
Reaction score
25,378
Habari za hv punde zikitokea hapa ubungo pembezoni mwa bank ya NBC ni kwamba majambazi wawili wakiwa na usafiri wa pikipiki wamempiga risasi ya mguuni raia mmoja aliyekuwa kabeba mfuko uliokisiwa na fedha.
Risasi hiyo amepigwa baada ya kukaidi kutotaka kutoa huo mfuko aliokuwa amebeba.

Mpaka hv ninapoleta habari hii vijana wengine wa bodaboda wanawafukuzia kwa nyuma hao majambazi huko walipokimbilia.

Nawasilisha.
 
Katika hali ya ajabu askari walio hapa bank, walikuwa hawana hata mpango japo walikuwa wanashuhudia.
Vilevile hv punde askari wanaotumia defender nao ndiyo wnafika hapa, yaani ni nusu saa baada ya tukio.
 
Polisi wako bize kuchukua rushwa barabarani na kuvizia baa zinazouza pombe wakati wa kazi. Kwanini majambazi yasitambe mchana kweupe?
 
Hawa jamaa wamekuja nusu saa baada ya tukio ila kuna mwendesha bodaboda mmoja kakoswa koswa na risasi akiwa anawafukuza kwa nyuma.
 
Attachments

  • 1425551398267.jpg
    1425551398267.jpg
    77.8 KB · Views: 1,491
Hawa jamaa wamekuja nusu saa baada ya tukio ila kuna mwendesha bodaboda mmoja kakoswa koswa na risasi akiwa anawafukuza kwa nyuma.

Na wewe zurula na pesa nyingi tu ukitaka.polisi wapo kwa ajiri yako.
 
Kuchukua fedha nyingi bila escort ya polisi ni hatari.
 
Kuchukua fedha nyingi bila escort ya polisi ni hatari.
Kumtaarifu polisi kuwa unapesa unahitaji ulinzi wake, ni Sawa na kujikabidhi mdomoni mwa Simba.

Bora Jambazi kuliko polisi.
 
Kumtaarifu polisi kuwa unapesa unahitaji ulinzi wake, ni Sawa na kujikabidhi mdomoni mwa Simba.

Bora Jambazi kuliko polisi.
Kama polisi anatamani pesa ya mwendesha bodaboda wakati ana mshahara wake, zakwako anaweza zolinda kweli???.
Tafakari.
 
Kumtaarifu polisi kuwa unapesa unahitaji ulinzi wake, ni Sawa na kujikabidhi mdomoni mwa Simba.

Bora Jambazi kuliko polisi.

Ni bora ukutane na vibaka siku hizi kuliko kukutana na defender la polisi wa kova,ni hatari sana hawa viumbe!!

kwenye Pesa usimuamini hata askari hakawii kuuza mchezo

Kazi ya polisi ni kulinda raia na mali zao,kama tumefikia huku watu hawawaamini tena polisi ni shida.Changamoto sana kwa Kova na IGP.
 
Huyu alienda kuchukua mgao wa escrow kwa mfuko bila ulinzi wa jeshi la polisi kama hajafa amshukuru Mungu
 
Kazi ya polisi ni kulinda raia na mali zao,kama tumefikia huku watu hawawaatena polisi ni shida.Changamoto sana kwa Kova na IGP.
Wananchi hawana imani na jeshi la polisi wao wenyewe wanaweza kuwa wahusika wakubwa
 
Hao waliochukua hizo hela wala sio majambazi, ni polisi walikuwa doria. Mwenye hela awahi kujificha, maana atajikuta mabwe pande.
 
Habari za hv punde zikitokea hapa ubungo pembezoni mwa bank ya NBC ni kwamba majambazi wawili wakiwa na usafiri wa pikipiki wamempiga risasi ya mguuni raia mmoja aliyekuwa kabeba mfuko uliokisiwa na fedha.
Risasi hiyo amepigwa baada ya kukaidi kutotaka kutoa huo mfuko aliokuwa amebeba.

Mpaka hv ninapoleta habari hii vijana wengine wa bodaboda wanawafukuzia kwa nyuma hao majambazi huko walipokimbilia.

Nawasilisha.

Tuombe MUNGU wakamatwe ili wataje mtandao wao wote,inaweza ikasaidia kupunguza idadi yao kwa kiasi fulani.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom