Habari
Kila siku anatuambiaga "msema kweli ni mpenzi wa mungu" Tundu lissu katuambia ukweli ndege yetu imekamatwa, wanamuita mchochezi na majina kibao kisa tu kasema ukweli.
Tusilitumie neno uzalendo vibaya, uzalendo /utaifa hauwezi kumilikiwa na mtu mmoja, Kila mtu anaweza Kuwa mzalendo kwa nafasi yake.
Neno uzalendo linatumika sana wanasiasa, lakini ukweli ni kwamba neno hili hutumika kulingana na maslahi ya anayelizungumza.
Kama kumetokea ubadhirifu wa mali za umma, vyama pinzani vinatakiwa kusema wapi?
kunyamaza kimya ndio uzalendo?
Au kusema ndio usaliti?
Nini maana ya uzalendo? Mtu kuipenda sana nchi yake ndio uzalendo?
Tunapimaje kwamba mtu anaipenda sana nchi yake?
Tanzania hatuna tatizo la ukabila badala yake kuna tatizo la watu kupenda sana vyama vya siasa kuliko nchi.
Mr mkiki.
Sent using
Jamii Forums mobile app