Majaliwa: Watanzania imarisheni uzalendo

Majs

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
232
Reaction score
520
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wote wahakikishe wanaboresha mshikamano wao pamoja na kuimarisha uzalendo kwa Taifa lao. Alitoa kauli hiyo juzi jioni wakati akizungumza na wanafunzi wa Tanzania wanaosomea udaktari nchini Cuba.

Waziri Mkuu yuko nchini Cuba kwa ajili ya ziara ya kikazi yenye lengo la kudumisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili. Alisema uzalendo kwa Taifa ni jambo muhimu. “Uzalendo ni muhimu sana kwa sababu tumekosa fursa nyingi za kimaendeleo kutokana na baadhi ya wananchi kutokuwa wazalendo kwa Taifa lao,” alisema Majaliwa kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na ofisi yake. Kutokana na hali hiyo, serikali inawasisitiza wananchi kuwa wazalendo na washirikiane kuhakikisha fursa za kimaendeleo zilizoko nchini zinaendelezwa.

Alisema serikali inatekeleza miradi mingi kwa lengo la kukuza uchumi kutoka wa chini kwenda wa kati, ni vema wananchi wakashirikiana nayo ili kufanikisha azma hiyo. Pia Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwasihi wanafunzi hao, kuzingatia sheria za nchini waliyoko pamoja na kukumbuka kurudi nyumbani mara wamalizapo masomo yao. Alisema serikali inatambua uwepo wao wa kimasomo nchini Cuba na kwamba inatarajia kupata mchango mkubwa kutoka kwao punde wamalizapo masomo yao.

“Nawaomba msome kwa bidii na mfaulu mitihani yenu. Elimu yenu iwasaidie katika ajira na muweze kurejesha mikopo mliyopewa na serikali ili iwanufaishe wengine,” alisema. Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliwataka mabalozi wote wanaoiwakilisha Tanzania katika mataifa mbalimbali kuhakikisha wanatangaza vivutio vya utalii.

Alisema Tanzania imejaaliwa kuwa na vivutio vingi vya utalii, hivyo ni vema mabaloziwakavitangaza jambo ambalo litasaidia kuongeza idadi ya watalii wanaokuja nchini. Miongoni mwa vivutio vya utalii vilivyoko nchini ni pamoja na mlima Kilimanjaro, visiwa vya Zanzibar, mbuga mbalimbali zenye wanyama wa aina tofauti tofauti.

Awali Mwenyekiti wa wanafunzi hao, Goodchance Tarimo alimhakikishia Waziri Mkuu kwamba watarejea nyumbani baada ya kumaliza masomo yao nchini humo. Alisema wao wana imani kubwa na serikali na wanaunga mkono jitihada zinazofanywa na viongozi wa Taifa kwa lengo la kuboresha maendeleo pamoja na kukuza uchumi. “Tunapongeza jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano katika kujenga uchumi wa viwanda, mapambano dhidi ya rushwa, ufisadi na ujenzi wa miundombinu ya kisasa,” alieleza.

CHANZO: Habari Leo
 
Huyo jamaa ni neutralizer wa maneno na action za bosi wake.. Yuko straight na smart kwenye maamuzi na action zake
 
Hivi uzalendo ni kwa wananchi tu mbona hatuoni viongozi wakionyesha mfano wa uzalendo.

Uzalendo wa kuwakamata wabunge wa upinzani na kuwaweka mahabusu, uzalendo wa kubagua nani afanye siasa na nani asifanye, uzalendo wa kuwanyang'anya wapinzani mashamba yao, uzalendo wa kuwafilisi wawekezaji wazawa na kuwakaribisha wezi wa nje ikulu, kwanini wasingemuita Manji ikulu wakaelewana jinsi ya kulipa kama walivyowaita wezi wa Acacia.

Sometimes viongozi wawe wanaona aibu wanapotaja neno uzalendo mbele za watu.
 
Maneno kuntu kutoka kwa PM!
Kuna watu hawalali kuhakikisha Taifa linaanguka mbaya zaidi watu hao ni watanzania!
 
Kuna watu hawalali kuhakikisha Taifa linaanguka mbaya zaidi watu hao ni watanzania![/QUOTE]
Ukitenda uovu na kuikataa haki taifa lazima liyumbe.maana imeandikwa HAKI UINUA TAIFA.
 
Maneno kuntu kutoka kwa PM!
Kuna watu hawalali kuhakikisha Taifa linaanguka mbaya zaidi watu hao ni watanzania!
Enzi za propaganda zimekwisha. Be analytical kwenye matamshi ya viongozi wetu nani anabomoa umoja wetu, kwa mfano kiongozi anasema watu wa mikoa mingine wasifanye biashara mkoa fulani
 
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wote wahakikishe wanaboresha mshikamano wao pamoja na kuimarisha uzalendo kwa Taifa lao. Alitoa kauli hiyo juzi jioni wakati akizungumza na wanafunzi wa Tanzania wanaosomea udaktari nchini Cuba.

Waziri Mkuu yuko nchini Cuba kwa ajili ya ziara ya kikazi yenye lengo la kudumisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili. Alisema uzalendo kwa Taifa ni jambo muhimu. “Uzalendo ni muhimu sana kwa sababu tumekosa fursa nyingi za kimaendeleo kutokana na baadhi ya wananchi kutokuwa wazalendo kwa Taifa lao,” alisema Majaliwa kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na ofisi yake. Kutokana na hali hiyo, serikali inawasisitiza wananchi kuwa wazalendo na washirikiane kuhakikisha fursa za kimaendeleo zilizoko nchini zinaendelezwa.

Alisema serikali inatekeleza miradi mingi kwa lengo la kukuza uchumi kutoka wa chini kwenda wa kati, ni vema wananchi wakashirikiana nayo ili kufanikisha azma hiyo. Pia Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwasihi wanafunzi hao, kuzingatia sheria za nchini waliyoko pamoja na kukumbuka kurudi nyumbani mara wamalizapo masomo yao. Alisema serikali inatambua uwepo wao wa kimasomo nchini Cuba na kwamba inatarajia kupata mchango mkubwa kutoka kwao punde wamalizapo masomo yao.

“Nawaomba msome kwa bidii na mfaulu mitihani yenu. Elimu yenu iwasaidie katika ajira na muweze kurejesha mikopo mliyopewa na serikali ili iwanufaishe wengine,” alisema. Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliwataka mabalozi wote wanaoiwakilisha Tanzania katika mataifa mbalimbali kuhakikisha wanatangaza vivutio vya utalii.

Alisema Tanzania imejaaliwa kuwa na vivutio vingi vya utalii, hivyo ni vema mabaloziwakavitangaza jambo ambalo litasaidia kuongeza idadi ya watalii wanaokuja nchini. Miongoni mwa vivutio vya utalii vilivyoko nchini ni pamoja na mlima Kilimanjaro, visiwa vya Zanzibar, mbuga mbalimbali zenye wanyama wa aina tofauti tofauti.

Awali Mwenyekiti wa wanafunzi hao, Goodchance Tarimo alimhakikishia Waziri Mkuu kwamba watarejea nyumbani baada ya kumaliza masomo yao nchini humo. Alisema wao wana imani kubwa na serikali na wanaunga mkono jitihada zinazofanywa na viongozi wa Taifa kwa lengo la kuboresha maendeleo pamoja na kukuza uchumi. “Tunapongeza jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano katika kujenga uchumi wa viwanda, mapambano dhidi ya rushwa, ufisadi na ujenzi wa miundombinu ya kisasa,” alieleza.

CHANZO: Habari Leo
Viongozi wetu mnatugawa wanachi, Leo walio upande wa upinzani wanaishi kwa mashaka kwani hata wakiongozana watatu wamevaa fulana zenye nembo ya Chadema watakamatwa kwa kuandamana! Taifa liko kwenye mgawanyiko mkubwa. Kila kukicha wapinzani wanakamatwa kwa kuonekana kwenye majimbo yasiyo yao! Jeshi la polisi macho na masikio yake yako kwa wapinzani zaidi kuliko wezi, wanajaa kwenye mikutano ya upinzani kuangalia nani yupo na nani kasema nini!
 
Awamu hii uzalendo utahubiriwa sana. Hongera kwa pm kuwa mzalendo wa kuwakamata wapinzani
 
Hivi uzalendo ni kwa wananchi tu mbona hatuoni viongozi wakionyesha mfano wa uzalendo.

Uzalendo wa kuwakamata wabunge wa upinzani na kuwaweka mahabusu, uzalendo wa kubagua nani afanye siasa na nani asifanye, uzalendo wa kuwanyang'anya wapinzani mashamba yao, uzalendo wa kuwafilisi wawekezaji wazawa na kuwakaribisha wezi wa nje ikulu, kwanini wasingemuita Manji ikulu wakaelewana jinsi ya kulipa kama walivyowaita wezi wa Acacia.

Sometimes viongozi wawe wanaona aibu wanapotaja neno uzalendo mbele za watu.
Noma sana
 
Back
Top Bottom