Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
WAKATI uchunguzi mkali ukiendelea kimya kimya mara baada ya sakata la kusaka watumishi hewa ndani ya Serikali kuelekea ukingoni, imebainika kuwa tayari majalada zaidi ya 230 ya kesi za vigogo wanaohusishwa na ubadhirifu kupitia mishahara hewa yamekamilika na baadhi yameanza kufikishwa mahakamani.
Uchunguzi kuhusiana na suala hilo umebaini kuwa majalada hayo yameandaliwa baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa kina unaofanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Habari nyeti kutoka TAKUKURU zinasema kuwa wahusika wote walioshiriki kufanikisha ‘dili’ ya ulaji wa fedha za umma kupitia orodha bandia ya watumishi wa umma hawatasalimika.
“Serikali hii haina huruma kwa watu wanaoifilisi nchi kwa manufaa yao binafsi. Takukuru wanafanya kazi kubwa sana ya kumbaini kila aliyehusika na ubadhirifu huu,” chanzo kiliiambia Nipashe.
Source: Nipashe