Majalada ya kesi 230 za vigogo waliotafuna mishahara ya watumishi hewa yakamilika

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,510
28,416
Mkurugenzi-mkuu-TAKUKURU-Valentino-Mlowola_0.jpg

WAKATI uchunguzi mkali ukiendelea kimya kimya mara baada ya sakata la kusaka watumishi hewa ndani ya Serikali kuelekea ukingoni, imebainika kuwa tayari majalada zaidi ya 230 ya kesi za vigogo wanaohusishwa na ubadhirifu kupitia mishahara hewa yamekamilika na baadhi yameanza kufikishwa mahakamani.

Uchunguzi kuhusiana na suala hilo umebaini kuwa majalada hayo yameandaliwa baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa kina unaofanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Habari nyeti kutoka TAKUKURU zinasema kuwa wahusika wote walioshiriki kufanikisha ‘dili’ ya ulaji wa fedha za umma kupitia orodha bandia ya watumishi wa umma hawatasalimika.

“Serikali hii haina huruma kwa watu wanaoifilisi nchi kwa manufaa yao binafsi. Takukuru wanafanya kazi kubwa sana ya kumbaini kila aliyehusika na ubadhirifu huu,” chanzo kiliiambia Nipashe.

Source: Nipashe
 
Nilikuwa naeleke kuamini kuwa nguvu za uchawi maana kuna jamaa yangu alipiga hela ndefu ya kampeni ya chanjo ya kitaifa ya surua. Tume iliyoundwa na wizara ya afya walikundua madudu ya kustaajabisha, wauguzi marehemu walisaini malipo, watoa chanjo walilala hotel kubwa jirani na makwao.
Baada ya ile tume kuondoka zimepigwa tambiko na zindiko za hatari, hadi tukaamini tumewamaliza kumbe mafaili yapo mikononi mwa TAKUKURU? Mbona mnaleta habari mbaya hizi, poa ngoja twende Gamboshi sasa!
 
Bado wale wa Vyeti feki sijasikia hatua zilizochukuliwa zaidi ya halmashauri ya mbalali ambayo iliwatimua watumishi waliothibitishwa walikuwa na Vyeti feki
 
Nilikuwa naeleke kuamini kuwa nguvu za uchawi maana kuna jamaa yangu alipiga hela ndefu ya kampeni ya chanjo ya kitaifa ya surua. Tume iliyoundwa na wizara ya afya walikundua madudu ya kustaajabisha, wauguzi marehemu walisaini malipo, watoa chanjo walilala hotel kubwa jirani na makwao.
Baada ya ile tume kuondoka zimepigwa tambiko na zindiko za hatari, hadi tukaamini tumewamaliza kumbe mafaili yapo mikononi mwa TAKUKURU? Mbona mnaleta habari mbaya hizi, poa ngoja twende Gamboshi sasa!
Serikali ya Tanzania haijawahi kushinda kesi za hivyo , ubabe wake uko kwenye kesi za uchaguzi .
 
Kuna mambo mengine ambayo nikiyatafakari siwezi kuyaamini. Katika mambo hayo nakuwa mpagani yaani asiye na imani katika hayo! Unaweza kusikia kuwa hawana hatia au kesi zimefutwa ama kingine chochote!
 
Wasipoweka watu rumande au kuwafilisi basi tena nitaona serikali hii haina cha uzito, na nitaendela ku enjoy matendo ya Raisi wa Nigeria maana yeye ananyoosha watu haswa.
 
Back
Top Bottom