Majalada ya kesi 230 za vigogo waliotafuna mishahara ya watumishi hewa yakamilika

Na uchunguzi wa Lugumi kukwapua bilioni 37, ununuzi wa boti uozo kwa bilioni 8, escrow na Wabunge wa MACCM kupokea rushwa ya milioni 10 kila mmoja umefikia wapi!?

Mkurugenzi-mkuu-TAKUKURU-Valentino-Mlowola_0.jpg

WAKATI uchunguzi mkali ukiendelea kimya kimya mara baada ya sakata la kusaka watumishi hewa ndani ya Serikali kuelekea ukingoni, imebainika kuwa tayari majalada zaidi ya 230 ya kesi za vigogo wanaohusishwa na ubadhirifu kupitia mishahara hewa yamekamilika na baadhi yameanza kufikishwa mahakamani.

Uchunguzi kuhusiana na suala hilo umebaini kuwa majalada hayo yameandaliwa baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa kina unaofanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Habari nyeti kutoka TAKUKURU zinasema kuwa wahusika wote walioshiriki kufanikisha ‘dili’ ya ulaji wa fedha za umma kupitia orodha bandia ya watumishi wa umma hawatasalimika.

“Serikali hii haina huruma kwa watu wanaoifilisi nchi kwa manufaa yao binafsi. Takukuru wanafanya kazi kubwa sana ya kumbaini kila aliyehusika na ubadhirifu huu,” chanzo kiliiambia Nipashe.

Source: Nipashe
 
Utasikia serikali haina mpango wa kuendelea na kesi hizo......Tanzania zaidi ya uijuavyo
 
Na uchunguzi wa Lugumi kukwapua bilioni 37, ununuzi wa boti uozo kwa bilioni 8, escrow na Wabunge wa MACCM kupokea rushwa ya milioni 10 kila mmoja umefikia wapi!?
Mkuu sasa hivi huko ni kusafi sana, wanatafuta pesa kwa njia zote, nina uhakika hawa jamaa watakuwa mfano.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Itakuwa ni danganya toto tu Mkuu ya kuhangaika na vidagaa wakati mapapa ya ufisadi nchini yakiendelea kuogopwa, "sifukui makaburi ya kale" hivi kuna sheria yoyote nchini inayozuia kufukua makaburi ya kale!? Sheria hii ipo kwenye msahafu upi wa sheria za nchi!? Kama hakuna sheria kama hii kwanini Sizonje atunge sheria yake ambayo haiendani na sheria za nchi!? Kwa manufaa ya nani Mkuu!?

Yale makaburi ya kale mengine ukiyafukua unajizika mwenyewe, wewe huoni Yona na Mramba waliionja Segerea, sasa hivi serikali inafanya kazi, hawa ingawa ni vidagaa kulinganisa na Lugumi jipu la uso lakini hii kesi isikililize inakwenda.
 
Ndiyo Watanzania tunachotaka kitokee hicho wache wajizike wenyewe kwani walivyoamua kufanya ufisadi dhidi ya Watanzania walifikiri nini!? Kwamba Watanzania hatuoni uozo wao mkubwa wanaoufanya dhidi ya nchi yetu!? Inakuwaje mtu afanye ufisadi mkubwa kama huo halafu apigiwe debe na mafisadi wenzie ili aingie Ikulu!? Wakati umefika sasa wa kusema enough is enough we as Tanzanians we're tired of these corrupt people.

Yale makaburi ya kale mengine ukiyafukua unajizika mwenyewe, wewe huoni Yona na Mramba waliionja Segerea, sasa hivi serikali inafanya kazi, hawa ingawa ni vidagaa kulinganisa na Lugumi jipu la uso lakini hii kesi isikililize inakwenda.
 
Hilo Tanzania haliwezekan labda hao wapigaji wawe ni wapinzani vngenevyo ni accrobats tu
 
Uchunguzi wa mv bagamoyo,,lugumi,,wabunge wa fisiem kuhongwa mil.10 kumi umefikia wapi?? Tunataka kuona mahakama ya mafisadi ikiyashughulikia majizi
 
Makaburi mengine yanachimbwa na mengine hayachimbwi.... Double Standard wengine wanalindwa... Wengine wanakuwa ni ma Bangusilo
 
Mkurugenzi-mkuu-TAKUKURU-Valentino-Mlowola_0.jpg

WAKATI uchunguzi mkali ukiendelea kimya kimya mara baada ya sakata la kusaka watumishi hewa ndani ya Serikali kuelekea ukingoni, imebainika kuwa tayari majalada zaidi ya 230 ya kesi za vigogo wanaohusishwa na ubadhirifu kupitia mishahara hewa yamekamilika na baadhi yameanza kufikishwa mahakamani.

Uchunguzi kuhusiana na suala hilo umebaini kuwa majalada hayo yameandaliwa baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa kina unaofanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Habari nyeti kutoka TAKUKURU zinasema kuwa wahusika wote walioshiriki kufanikisha ‘dili’ ya ulaji wa fedha za umma kupitia orodha bandia ya watumishi wa umma hawatasalimika.

“Serikali hii haina huruma kwa watu wanaoifilisi nchi kwa manufaa yao binafsi. Takukuru wanafanya kazi kubwa sana ya kumbaini kila aliyehusika na ubadhirifu huu,” chanzo kiliiambia Nipashe.

Source: Nipashe

ESCROW uchunguzi umefikisha miaka mwili sasa!
 
Eti uchunguzi kimyakimya!! Majarada 230!!! ni Tanzania hii na serikali hii ifanye mambo kimyakimya? Mbona ungesikia kiki hiyo " Mijizi 230 imegundulika"!!
 
Back
Top Bottom