MAJAJI WACHAGULIWE! new Katiba, pia ma RC

Hute

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,537
6,458
Jamani, yule jaji wa Arusha aliyetoa hukumu Lema asigombee kwa 5 years, wakati Lema hajapatikana na ushahidi wa rushwa (rushwa ndo inafanya iyo 5 years), kuna dalili zote kuwa alipandikizwa. ccm wanapandikisha au wanatoa order from above kuwaamuru watu wa judiciary wahukumu kwa interest zao, watu wa judiciary nao kwasababu labda wakiwa majaji wa high court wanatarajia kupanda court of appeal, wanajipendekeza kwa interest zao.

Marekani majaji wanachaguliwa, sina uhakika, ila ni kama wanachaguliwa na bunge lao etc sina uhakika. ninachopenda ku submit ni kwamba, MAJAJI TZ WACHAGULIWE NA WABUNGE, NA WAWE NA SIFA SAHIHI, HILI JAMBO LIINGIZWE KWENYE KATIBA MPYA TUNAYOTARAJIA KUITENGENEZA. hii itaifanya judiciary iwe independent, na vilevile tutapata majaji waadilifu kama nchi zingine. hii itaweka usawa mbele ya sheria kwa wananchi wote, vyama vyote na mashirika yote etc.

Pia, wakuu wa mikoa wachaguliwe, wakuu wa wilaya wafutwe kabisa. nasema ma RC wachaguliwe kwasababu kwa sasa wanaishi kwaajili ya chama tawala, wasiposapoti chama tawala, kibarua chao kipo matatani. hivyo wanakuwa watumwa wa chama tawala na rais wake kwasababu ndiye aliyewateua, anaweza asiwateue tena wakati ujao.....wakichaguliwa na wananchi nafikiri itawafanya wawajibike sio kwa rais, bali kwa wananchi. WAKUU WA WILAYA WAFUTWE, HAO HAWANA KAZI YA KUFANYA. nawakilisha.
 
tungángánie hadi suala la majaji na wakuu wa mikoa kuchaguliwa liingizwe kwenye katiba mpya. hapo tutakuwa tumeponya vitu vingi.
 
actually, hii itakomesha majaji wanaoelekezwa na makada nini cha kuamua.....watakuwa accountable kwa wananchi, hatutaki kabisa kiendelee kutokea hiki kinachotokea kwa Lema kule Arusha. angalia hii ya sumbawanga, unaweza kushangaa pamoja na kwamba rushwa ilithibitishwa, utakuwa hajaambiwa asigombee kwa miaka mitano....wakati lema kaambiwa asigomee miaka mitano wakati hakula rushwa na kwa kawaida, wanaotakiwa wasigomee miaka mitano kisheria ni wale waliogundulika kutoa au kupokea rushwa.....mahakama zetu ni mali ya ccm.
 
Nafikiri post ambazo inatakiwa wahusika wachaguliwe na sio kuteuliwa na rais ni nying mno na hii nafikiri itasaidia kuleta uwajibikaji serikalini na katika sekta mbalimbali za UMMA mfano mashirika mbalimbali ya umma kama Tanesco, Tanapa, NIC, NSSF, NHC, Mabenki ya umma na mengine mengi. Hii nayo kali hata mkurugenzi wa AICC lazima ateuliwe na rais jamani.

Hapo kwenye mashirika wakichaguliwa na wabunge moja kwa moja bunge linakuwa na uwezo wa kuwawajibisha wanapovurunda na sio mpaka serikali ndio iseme.

Wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa wote wafutwe ila tuwe na kanda nazo ziongozwe na magavana watakaochaguliwa na wananchi moja kwa moja na hivyo wabunge kusimamia baadhi ya roles za wakuu wa wilaya>*
 
Back
Top Bottom