Kipenzi Changu
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 59,662
- 140,285
Nchi ngumu sana hii.
Inakuweje na wewe umeamua kuwa upande wa WASALITI?
Nchi ngumu sana hii.
Labda anamaanisha ndo anasoma sasa na uteuzi tayari ulifanyika.
Issue ni kupewa ujaji kabla hajapata hiyo degree ya sheria. huoni tatizo hapo?Kwani LLB ya Open University siyo degree ya sheria?
Tena kwa taarifa yako wengi waliograduate LLB UDSM wamekuwa wakitumia madesa ya Open University yaliyoandaliwa na walimu wa sheria UDSM.
Issue ni kupewa ujaji kabla hajapata hiyo degree ya sheria. huoni tatizo hapo?
Miaka mitano ikipita na hilo sharti maalum la digrii ya sheria halijatimizwa huyo mtu aliyeteuliwa anapoteza ujaji? Kama ulivyoandika kwenye bandiko namba 22, jaji Mbarouk alipandishwa na Kikwete kuwa jaji wa rufaa zaidi ya miaka 5 baada ya kupewa ujaji, na hadi anateuliwa na Kikwete, alikuwa hajatimiza hilo sharti maalum la digrii.
Ibara ya 109 Ibara ndogo ya 9 inasema kuwa "Iwapo Rais atatosheka kwamba ijapokuwa mtu mwenye sifa mojawapo ya hizo sifa maalum hakuwa nayo sifa hiyo kwa muda usiopungua miaka mitano, lakini mtu huyo ana uwezo, ujuzi na kwa kila hali anafaa kukabidhiwa madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu na kuna sababu za kumfanya mtu huyo astahili kukabidhiwa madaraka hayo, basi Rais aweza kutangua lile sharti la kuwa na sifa maalum kwa muda usiopungua miaka mitano, na baada ya kushauriana na Tume ya Kuajiri ya Mahakama, Rais aweza kumteua mtu huyo kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Hapo unaweza kuona jinsi Katiba inavyompa Rais madaraka ya kuteua majaji kiasi kwamba anaweza kutangua lile sharti la kuwa na sifa maalum yaani degree ya sheria.
Kama Katiba isingempa Rais Madaraka ya kutangua lile sharti la kuwa na sifa maalum yaani degree ya sheria, then asingeweza kumteua jaji ambaye hana degree ya sheria.
Kwa maana nyingine inawezekana tatizo siyo JK bali sheria yenyewe.
Labda tu kwa kuwapangia/kuwateua kwa kazi nyingine - kama Jaji wa 'masjala'!No, No, hata aliyewachagua hana mamlaka ya kuwatoa, hata atakayekuja, hana mamlaka ya kuwatoa mpaka kwa tume maalum ikijumuisha wajumbe (majaji? )toka nje ta Tanzania -commonwealth countries
Inakuweje na wewe umeamua kuwa upande wa WASALITI?
Kwani LLB ya Open University siyo degree ya sheria?
Tena kwa taarifa yako wengi waliograduate LLB UDSM wamekuwa wakitumia madesa ya Open University yaliyoandaliwa na walimu wa sheria UDSM.
Mkuu,
Issue ni kuwa huyo Jaji kapewa u jaji without LLB.
Haijalishi ni ya wapi
Miaka mitano ikipita na hilo sharti maalum la digrii ya sheria halijatimizwa huyo mtu aliyeteuliwa anapoteza ujaji?
Kama ulivyoandika kwenye bandiko namba 22, jaji Mbarouk alipandishwa na Kikwete kuwa jaji wa rufaa zaidi ya miaka 5 baada ya kupewa ujaji, na hadi anateuliwa na Kikwete, alikuwa hajatimiza hilo sharti maalum la digrii.
Nashukuru, sina la ziada.Katiba iko silent hapo unless kama kuna sheria au utaratibu mwingine. Hata hivyo, "kwa muda usiopungua miaka mitano" unaitafsiri kivipi?
Hicho kifungu kinahusu uteuzi wa Majaji wa Mahakama Kuu siyo Mahakama ya Rufaa. Nafikiri Ibara sahihi ni 118(3) inayosema kuwa "Majaji wengineo wa Mahakama ya Rufani watateuliwa na Rais, baada ya kushauriana na Jaji Mkuu, kutoka miongoni mwa watu ambao wanaweza kuteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano kama ilivyoelezwa katika ibara ya 109 ya Katiba hii au kutoka miongoni mwa watu wanaoweza kuteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar kwa mujibu wa Sheria zinazotumika Zanzibar.
Inasemwa kuwa Jaji Mbarouk anatokea Zanzibar. Kama ni kweli, Ibara ya 94(1) ya Katiba ya Zanzibar inasema kuwa "Mtu hatoweza kuteuliwa kuwa Jaji au Kaimu Jaji wa Mahkama Kuu mpaka: (a) awe na shahada ya Sheria ya Chuo Kikuu kinachotambuliwa au Chuo cha aina hiyo..".
Hata hivyo, Ibara ya 94(5) inasemakuwa "Ikiwa Jaji wa Mahkama Kuu ameteuliwa kuwa Kaimu Jaji Mkuu au kwa sababu nyengine yoyote ile hawezi kufanya kazi zake za Ujaji au ikiwa Jaji Mkuu atamshauri Rais kwamba kwa hali ilivyo Mahkama Kuu inahitajia Jaji mwengine, Rais akishauriana na Tume ya Utumishi ya Mahkama, anaweza kumteua mtu yeyote kuwa Jaji wa Mahkama Kuu bila ya kujali umri ulioelezewa katika kifungu 95(1) cha Katiba hii."
Kama Jaji Mbarouk ni "miongoni mwa watu wanaoweza kuteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar kwa mujibu wa Sheria zinazotumika Zanzibar", basi anaweza kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa.
Kama huyu jaji anatokea Tanzania Bara, then Lissu anaweza kuwa na very strong argument. Lakini kama anatokea Zanzibar then, Rais wa Zanzibar anayo madaraka ya kumteua mtu yeyote kuwa Jaji wa Mahakama Kuu hata kama akiwa na umri wa miaka 101.
Again hapo tatizo linapanuka na kuhusisha pia Katiba ya Zanzibar. Tatizo siyo mtu bali sheria yenyewe. Hata kama ukimbadilisha Rais, bado atakuwa na madaraka yale yale ya kuteua majaji ambao hawana LLB. Tatizo la sheria lilikuwepo tokea zamani, sema hakuwa kuteuliwa jaji katika mazingira hayo.
cc Bramo