Majaji hawa 7 ndiyo adui wa demokrasia TZ

Malafyale

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
13,813
11,123
Majaji hawa 7 wa Mahakama ya Rufaa wakiongozwa na aliyekuwa Jaji Mkuu Augustino Ramadhan,akisaidiwa na majaji wenzake 6 ambao ni Eusebio Munuo, Januari Msofe, Benard Luanda, Mbarouk Mbarouk, Nathalia Kimaro na Sauda Mjasiri;hapo Juni 16, 2011 walikataa TZ isiwe na mgombea binafsi tena wakitupilia mbali andiko ndani ya katiba linalosema kuwa"Kila mtz ana haki ya kupiga na kupigiwa kura";Kama kupiga kura hatuhitaji kuwa na udhamini wa chama cha siasa iweje kupigiwa kura lzm udhaminiwe na chama cha siasa?

Bado nitazidi kuwaheshimu hadi siku yangu ya kufa Majaji watatu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Amir Manento, Salum Massati na Thomas Mihayo kwa kuruhusu mgombea binafsi kabla ya majaji wengine 7 wa Mhakama ya Rufaa kuhujumu demokrasia yetu!

Tuseme ukweli na wala kutoa maoni yako huru kusichukuliwe kama ni kuingilia uhuru wa mhimili mwingine wa dola!Kama mgombea binafsi angeruhusiwa unahisi hii fukuza fukuza ya wabunge na madiwani tunayoishuhudia sasa hivi ingekuwepo?
 
Ndiyo hivyo, kila sehemu kuna genge la wapenda madaraka! na sikuona kwa nini mgombea binafsi asiruhusiwe! Inawezekana pia hoja yao ilikuwa na mantiki kwani wengi wetu hajui walichosema kwa undani zaidi.
 
Amir Manento, Salum Massati na Thomas Mihayo..wanafaa kuwemo kwenye tume ya katiba mpya lakini iam sure hawawezi teuliwa sababu watahatarisha maslahi ya chama..
 
Suala la mgombea binafsi lilijadiliwa sana kwenye kesi ya Mtikila na ilionekana kabisa kumkataza raia ugombea binafsi ni kumnyima haki yake ya kikatiba! Lakini pia tukiangalia upande wa pili, kuna articles nyingi tu zinazoenda kinyume na the Bill Of Rights na hapa ndipo tatizo kubwa lilipo! BTW; naungana na wewe mtoa maada, kweli majaji wengi wanarudisha democrasia nyuma na mfano mzuri ni huyo Augustino, yaani ni pure physical figure tuu....dispense of justice kwake ni ziro!!!
 
Amir Manento, Salum Massati na Thomas Mihayo..wanafaa kuwemo kwenye tume ya katiba mpya lakini iam sure hawawezi teuliwa sababu watahatarisha maslahi ya chama..

Ndo matatizo ya party supremacy hasa ukizingatia mkubwa wa chama ndie mkubwa wa nyanja zote!!
 
Lakini ipo siku tutafika tuu, wananchi tutakapo amua kutoa kansa inalolisumbua Taifa letu
 
Majaji hawa 7 wa Mahakama ya Rufaa wakiongozwa na aliyekuwa Jaji Mkuu Augustino Ramadhan,akisaidiwa na majaji wenzake 6 ambao ni Eusebio Munuo, Januari Msofe, Benard Luanda, Mbarouk Mbarouk, Nathalia Kimaro na Sauda Mjasiri;hapo Juni 16, 2011 walikataa TZ isiwe na mgombea binafsi tena wakitupilia mbali andiko ndani ya katiba linalosema kuwa"Kila mtz ana haki ya kupiga na kupigiwa kura";Kama kupiga kura hatuhitaji kuwa na udhamini wa chama cha siasa iweje kupigiwa kura lzm udhaminiwe na chama cha siasa?

Bado nitazidi kuwaheshimu hadi siku yangu ya kufa Majaji watatu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Amir Manento, Salum Massati na Thomas Mihayo kwa kuruhusu mgombea binafsi kabla ya majaji wengine 7 wa Mhakama ya Rufaa kuhujumu demokrasia yetu!

Tuseme ukweli na wala kutoa maoni yako huru kusichukuliwe kama ni kuingilia uhuru wa mhimili mwingine wa dola!Kama mgombea binafsi angeruhusiwa unahisi hii fukuza fukuza ya wabunge na madiwani tunayoishuhudia sasa hivi ingekuwepo?

mbona mmesahau mkuu wa bunge mh. anna makinda?
 
hivi haiwezekani kufungua tena hii kesi ya kudai mgombea binafsi, au kuna hamakama ya kimataifa tunayoweza kwenda kufungua tena hili shauri wataalamu wa sheria tujuzeni. na ikiwa inawezekana je mnaonaje sasa tukajiunga kama watanzania tukawawezesha wanasheria makini kama mtikila wenye kuweza kufungua na kutete kesi tukapata ushidi na hatimae haki ikatenda?
 
Majaji hawa 7 wa Mahakama ya Rufaa wakiongozwa na aliyekuwa Jaji Mkuu Augustino Ramadhan,akisaidiwa na majaji wenzake 6 ambao ni Eusebio Munuo, Januari Msofe, Benard Luanda, Mbarouk Mbarouk, Nathalia Kimaro na Sauda Mjasiri;hapo Juni 16, 2011 walikataa TZ isiwe na mgombea binafsi tena wakitupilia mbali andiko ndani ya katiba linalosema kuwa"Kila mtz ana haki ya kupiga na kupigiwa kura";Kama kupiga kura hatuhitaji kuwa na udhamini wa chama cha siasa iweje kupigiwa kura lzm udhaminiwe na chama cha siasa?

Bado nitazidi kuwaheshimu hadi siku yangu ya kufa Majaji watatu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Amir Manento, Salum Massati na Thomas Mihayo kwa kuruhusu mgombea binafsi kabla ya majaji wengine 7 wa Mhakama ya Rufaa kuhujumu demokrasia yetu!

Tuseme ukweli na wala kutoa maoni yako huru kusichukuliwe kama ni kuingilia uhuru wa mhimili mwingine wa dola!Kama mgombea binafsi angeruhusiwa unahisi hii fukuza fukuza ya wabunge na madiwani tunayoishuhudia sasa hivi ingekuwepo?

Kwenye red, tunahitaji mgombea binafsi ili watu wasifukuzwe kwenye vyama au kudumisha demokrasia?

naunga mkono mgombea binafsi na naunga mkono watu wanaokwenda kinyume na taratibu za vyama vyao kuchukuliwa hatua zinazostahili.
 
Hawa majaji ni maadui wakubwa wa demokrasia adhabu wanayostahili ni kupigwa mawe hadi wafe.
 
Mgombea binafsi ataendesha serkali kama kampuni binafsi. Maamuzi yatakuwa ni kupata faida pekee. Yeyote atakae sababisha hasara atafukuzwa kazi. Hii ndiyo maana magamba hawawezi kuruhusu mgombea binafsi kwani watakosa kazi na kuswagwa mahabusu watakapo fanya ufisadi.
 
mkuu unawapigia chapuo hao uliowataja? au?

Jamaa ameweka wazi kuwa hawa ndiyo majaji walioruhusu mgombea binasfi ambao uamuzi wao ulibadilishwa na hao wa mahakama ya rufaa.

Hivi TZ hatuna constitutional court??
 
Back
Top Bottom