Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Mahakama kuu ya kikatiba nchini Brazil, imerejelea vikao vyake katika kesi ya kumuondoa Rais wa nchi hiyo, Michel Temer.
Mahakama hiyo ambayo imepewa majukumu ya kusimamia shughuli za uchaguzi mkuu, inachunguza iwapo pesa haramu zilitumika katika kampeini na hatimaye ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2014.
Huo ndio uchaguzi mkuu ambao Bi Dilma Rousseff alishinda, huku Bwana Temer akiwa mgombea mwenza.
Bi Roussef, alingolewa madarakani baada ya kupigiwa kura isiyokuwa na imani na mahala pake pakachukuliwa na Bw. Temer.
Bi Roussef, alishutumiwa kwa makosa ya kuhamisha hazina ya fedha za serikali kutoka akaunti moja hadi nyingine.
Kama matokeo Bw. Temer akachukua kiti cha Urais wa Brazil mnamo Agosti mwaka 2016.
Hata hivyo, kesi hii, ambayo ilisimamishwa kwa muda mwezi Aprili, itafutilia mbali matokeo nzima ya uchaguzi mkuu mwaka 2014, hii ikiwa na maana kuwa ataondolewa ofisini.