Maiti kucharazwa bakora.!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
Hivi majuzi nilihudhuria msiba wa jamaa yetu mmoja ambaye alikuwa amejitoa roho kwa kile alichodai kuwa maisha ni magumu. Kwamba pamoja na kuwa na Elimu nzuri lakini ameshindwa kupata ajira.

Siku hiyo nilikuwa na mgeni kutoka Uganda na niliambatana naye kule msibani. Wakati tunapiga soga, pale msibani, yuko bwana mmoja akasema kuwa marehemu hatazikwa kwa mujibu wa taratibu za kidini (Marehemu alikuwa ni Mkristo) kwa sababu amejiuwa na kwa mujibu wa dini hiyo ni dhambi hivyo hakuna kiongozi wa dini atakayeshiriki msiba ule.

Yule rafiki yangu kutoka Nchini Uganda akadakia, akasema kule kwao mtu akijiuwa maiti yake inacharazwa bakora hadharani kabla ya kuzikwa. Aliendelea kubaisha kwamba kule kwao kujitoa roho ni jambo lenye kufedhehesha sana na ndio maana ukawekwa huo utaratibu wa kucharaza maiti bakora ili kuwatisha watu wasijitoe roho.

Mimi huu utaratibu nimeupenda, maana utapunguza matukio ya watu kujitoa roho kwa kuhofia maiti zao kucharazwa bakora…………………
 
ukiamua kujiua kwa matatizo ya one or two years, or even a life time, basi hizo bakora siku moja, tena ambazo hauta ziskia sababu umesha kufa, haziwezi kukurudisha nyuma. Mtu kujitoa roho ni act of great distress...
 
Hata watangaze kuwa ukijiua unachomwa moto, bado kama kujiua watajiua tu.

Hakuna dawa ya kuzuia mtu kujiua
 
RR kwani kujiuwa ndio solution?
 
labda watangaze kuwa anaetaka kujiua aende polisi akashootiwe. jamaa mmoja yeye alitaka kujiua porini ila alimuona simba anakuwa wanguwangu jamaa nduki!!1
 
Hata watangaze kuwa ukijiua unachomwa moto, bado kama kujiua watajiua tu.

Hakuna dawa ya kuzuia mtu kujiua

Dawa ipo bana, kama unapata ushauri nasaha waweza kuepuka kujitoa roho.................
 
Nani anakuwa mcharazaji bakora? Maana umesema hata viongozi wa dini wamejitoa.
 
\

Soma vizuri bana..........Uganda ndio wanacharaza bakora, ila hapa viongozi wa dini wanasusa kuzika.........
Kwa Uganda, wapo wana ukoo walioteuliwa kufanya kazi hiyo
 
Hivi majuzi nilihudhuria msiba wa jamaa yetu mmoja ambaye alikuwa amejitoa roho kwa kile alichodai kuwa maisha ni magumu. Kwamba pamoja na kuwa na Elimu nzuri lakini ameshindwa kupata ajira.

Siku hiyo nilikuwa na mgeni kutoka Uganda na niliambatana naye kule msibani. Wakati tunapiga soga, pale msibani, yuko bwana mmoja akasema kuwa marehemu hatazikwa kwa mujibu wa taratibu za kidini (Marehemu alikuwa ni Mkristo) kwa sababu amejiuwa na kwa mujibu wa dini hiyo ni dhambi hivyo hakuna kiongozi wa dini atakayeshiriki msiba ule.

Yule rafiki yangu kutoka Nchini Uganda akadakia, akasema kule kwao mtu akijiuwa maiti yake inacharazwa bakora hadharani kabla ya kuzikwa. Aliendelea kubaisha kwamba kule kwao kujitoa roho ni jambo lenye kufedhehesha sana na ndio maana ukawekwa huo utaratibu wa kucharaza maiti bakora ili kuwatisha watu wasijitoe roho.

Mimi huu utaratibu nimeupenda, maana utapunguza matukio ya watu kujitoa roho kwa kuhofia maiti zao kucharazwa bakora…………………
kuchapa maiti maiti hakuwezi kusaidia kupunguza matukio, kwani anayechapwa hasikii kitu!
 
Kwa wanasikolojia mtu anayejiua anahesabika kuwa mtu MKATILI sana..
Hiii inabebwa na mantiki ya kawaida tu ya kuwa kila binadamu ni SELFISH..means kila mtu anajipenda yeye kwanza..
Sasa kama mtu anajifikiria KUJIUA maana yake amejichukia kupita kiasi..na hata kama ataendelea kuishi na hii roho yake ya UKATILI basi huko mbeleni anaweza kufanya JANGA la hatari sana..Just imagime kilichotokea Norway..miezi michache iliyopita..
Kwangu mimi siamini kama wazo la Kujiua huwa linakuja overnight tu..zaidi ni accumulation ya 'griefs' ambazo huyu mwanadamu anakuwa amezibeba kwa siku nyingi..so, viboko havisaidii, badala yake heri wawe wanajiua ili kupunguza kuleta Madhara kwa Jamii KUBWA..
 
Kwetu umakondeni ukijiua unazikwa kama HERO- tafsiri yake ni kuwa wewe ni mtu usiyependa mchezo na si legelege. Kwani uliwahi kusikia mtu legelege anajiua?! Yu radhi awe ombaomba kuliko kifo- kazi kwenu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom