Maisha yangu yapo Hatarini jamani...Nifanyeje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maisha yangu yapo Hatarini jamani...Nifanyeje?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kituku, Jun 28, 2011.

 1. Kituku

  Kituku JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 239
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hali ya maisha yangu jamani imeanza kuwa tete, kamshahara kangu ni ka kima cha chini... vibiashara vidogo vidogo ndo vinavyoniongezea kashilingi ka kusukuma maisha yangu... Hapa mtaani kwetu hatuna umeme leo siku ya tano... hvi hii serikali yetu inatufikiria kweli wananchi wa kawaida? wanataka tukaibe?

  Kwangu sababu za kutokapatikana umeme wanazotoa haziniingiii akilini, na inaniuma sana kwa kodi nazokatwa kwenye kamshahara kangu na vilevile hata kwenye vibiashara vyangu.. zinakwenda wapi? auhawa viongozi wetu hawaexperience hili tatizo huko Oyesterbay na masaki? au serikali imewapa super power jenerators?

  Kinachonishangaza nimeenda kulipa billl ya umeme deni langu limezidi 10,000 ya bili ya kawaida ninayolipa, kila mwezi bili inazidi na mgao upo palepale.. jamani jamani..

  Namchukia sana huyo mtu anaeitwa Ngeleja... sijui nikimuona kama sijatema mate, Namchukia sana Kwikwete mtu asiyejua au hata kuzungumza na wananchi walipa kodi masuala hatari kama haya, Nachukia sana wabunge wanaopitisha hoja kwa 100%, Namchukia sanaWaziri mkuu kwa kuwa hana tamko lolote la nguvu na la ukali analotoa juu ya tatizo hilo la kitaifa.. , soko gani la ajira liliongezeka hapa, wanataka vijana warudi mtaani?

  .............kwanini wasifanye janga la umeme ni janga la kitaifa... Kila siku tuna mpango tuna mpango... this is too much...
  N
   
 2. Averos

  Averos JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2011
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 648
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  We hujui kuwa tuko katika zama za maisha bora kwa kila mtanzania!, uko wapi wewe!?
   
 3. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hakuna jipya kwenye utawala huu,labda yafanyike mageuzi makuwa ndiyo unafuu wa maisha kwa kila mtanzania utapatikana!!
   
 4. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Pole sana.......naguswa na stori yako,lakini wao hawaguswi ng'o
   
 5. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,518
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Kila siku nafikiria hivi rais wetu yupo nchini kweli? mbona hasemi kitu au kule magogoni kuna umeme unatoka USA? kweli inasikitisha sana na nchi hii itakuwa mbaya pale tutakapo choka na kuamua kuingia barabarani mtatukoma haki ya Mungu lazima nikanunue AK47 siku hiyo....tuna mkenya hapa kazini anatutukana sana hatujijui umeme tuwauzie halafu tunabaki na mgao? nini maana ya miaka 50 ya uhuru? kweli nina hasira sana na nchi hii hawajui tu....UDOM, SAUTI, DUCE, UDSM na kote kwingine wanarudishwa home eti hawana tuition fee, wakati hizo pesa zinatumwa direct kutoka HESLB na kwenda chuoni sasa mwanafunzi unamrudisha wa nini si fukuza mkurugenzi wa mikopo? shit.
   
 6. Kituku

  Kituku JF-Expert Member

  #6
  Jun 28, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 239
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hii tanzania ya amani wanayosema ipo siku watajutia na wataisikizia uhamishoni... Raisi, waziri mkuu hata hata tamko??? wiki watu hatuna umeme na wanalijua wanafanya wamefumba macho... unafiki mtupu
   
 7. Kituku

  Kituku JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 239
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nayasubiri kweli mapinduzi ya nchi hii... nitashiriki nakula yamin (naapa)
   
 8. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #8
  Jun 28, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Megawati 50 zitaongezwa kwenye gridi hivi punde, pia kuna megawati 200 zitapatikana mara baada ya mitambo mipya. Tuna mpango wa wa kupata megawati 196 kutokana na makaa ya mawe na megawati nyingine 150 zitatokana na kuongezwa kwa matumizi ya gesi ya songosongo.
  Sasa wee unalalamika lalamika nini?

  CCM Hoyeeeeeeeeeee!!!.....
   
 9. Mpenda Kwao

  Mpenda Kwao Senior Member

  #9
  Jun 28, 2011
  Joined: Apr 29, 2008
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hapo kwenye bold " Kwere kaishiwa uongo ndio maana hotuba za kila mwezi hazipo tena kwani kashamaliza uongo wote kwa watanzania"
   
 10. Mpenda Kwao

  Mpenda Kwao Senior Member

  #10
  Jun 28, 2011
  Joined: Apr 29, 2008
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33

  kwa mipango ya kwenye makaratasi tu hatujambo!!
   
 11. nyengo

  nyengo JF-Expert Member

  #11
  Jun 28, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 433
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Nawachukia watu wote wanaoshabikia sera mbaya za ahadi ahadi za CCM
  Namchukia Malaria Sugu, Faiz Fox, Riz1 na wote wanaotetea upupu wa CCM ndani na nje ya JF
  Namchukia........
   
 12. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #12
  Jun 28, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  Mageuzi umekosea. ebu fatilia hali ya misri na wamisri before and after mageuzi uone majuto waliyonayo. Jamanai serikali inaonekana kuchemsha katika hili ebu basi matajiri wakubwa wazalendo na wananchi wote tuisaidie serikali. kwani tukiendelea kulalamika sana tunaumia sisi wenyewe. ebu wana siasa wote kwa pamoja na wadau wote wanaojiita wanaharakati wafanye dharula ya kuweka tofauti za kisiasa na wakae pamoja kutafuta ufumbuzi wa kitaifa wa kudumu. mambo hayaendi tanesco kwa sababu siasa imeingizwa kila sehemu kiasi kwamba wazo hata likiwa zuri lakini likawa limetolewa na chadema au Cuf ccm wanaona halina mpango, kwa style hii anayeumia ni mwananchi.
   
 13. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #13
  Jun 28, 2011
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kumbe Megawatt na umeme ni vitu viwili tofauti kwani kila wakiulizwa wanaongeza megawatt ila matokeo tunayoona siyo kusikia ni kuwa umeme hakuna - Nachukia, najutaJK kuitwa rais wangu - rais anayejijali yeye na watu wake tu- rais asiyejua shida za watu wake

  Na amini ipo siku CCM na watu wao watakuwa makumbusho na historia
   
 14. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #14
  Jun 28, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  raisi wetu mara ya mwisho kumuona kwenye vyombo vya habari au kumsikia ni wakati wa mabomu ya gongolamboto tu, zaidi ya yote namsikia akiwa kwenye tafrija au safarini.
   
 15. Kituku

  Kituku JF-Expert Member

  #15
  Jun 28, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 239
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Natamani ningekuwa malaika, nikatua kila kwenye nyoyo za wabunge woote bungeni na kurudisha nia zao za umoja (si siasa) na kufanya maamuzi mazuri kwamba ukiacha budget ya wizara ya afya, Elimu na chakula, pesa zote zilizobaki zingeshughulikia kwanza suala la umeme, then budget ya mwakani ndo tukarudi kwenye miundo mbinu, utalii, maposho /semina na safari za viongozi wa serikali... hiyo pesa ingetumika kutatua tatizo la umeme kwanza
   
 16. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #16
  Jun 28, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  you are not alone.... tupo wengi mkuu

  change must come now!! and we can drive it
   
 17. e

  evaluator Senior Member

  #17
  Jun 28, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 177
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  nchi haina uongozi tena,tuliye mkabidhi amebonyeza auto button yaani inajiendea yenyewe tu....sijui wakati wa kutua itakuaje.kama wananchi walio wengi wange kua nafikira kama zangu ni bora tungewapa CDM watutatulie hili tatizo!
   
 18. Kituku

  Kituku JF-Expert Member

  #18
  Jun 28, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 239
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Me nasema si lazima Chadema tu...hata angetafutwa mtu binafsi hata kama bakhresa tukamwambia tuendeeshee nchi kwa muda tu... maana ukisema chadema watasema uchochezi siasa......Hii nchi JK imemshinda kabisa.. ni umbumbumbu tu wananchi wachache wanaonunuliwa kwa doti za kaka, fulana, kofia na mabango ya kuziba matundu ya mchwa nyumbani mwaooo........Pumbafuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
   
Loading...