Maisha Yangu na VVU mwilini

What a confident man! Big up mzee, natamani wanaume wote tungekuwa kama wewe!
 
Jamaa smart sana,kheri yako uliyepima na kujua status yako na kuikubali,maana kuwa na HIV sio mwisho wa maisha.
Nakushauri usiharakishe kutafuta mwenza,ongeza nguvu katika biashara zako,fikiria zaidi kuhusu kuwa na mafanikio makubwa.Ukishatulia kidogo then ndo umtafute mwenza.Ukifuata masharti ,utaishi hadi uzeeni,wengi wana HIV lakini hawajijui.
 
....Funguo inahitajika watu kama wewe kufanikiwa na mapambano dhidi ya UKIMWI.hatuwezi kuushinda UKIMWI kwa kuwa wanafiki na wenye unyanyapaa. Maisha lazima yanedelee, na UKIMWI au bila UKIMWI. Watu mlio katika ndoa, mnapaswa kujiangalia sana, takwimu kila kona ya Afrika zinaonyesha sasa maambukizi yanaenea zaidi miongoni mwa wanandoa, au watu waliokatika mahusioano yenye " uaminifu" kwa muda mrefu. Sababau zake ziko wazi; hawa ndio wasiotumia Kondomu. Wale "vicheche" na watu wa "hit and run" wanajijua kuwa ni watu wanaochukua risk, hivyo wanatumia Kondomu. Ndigu, Ufunguo, kwa kuwa umeshajitambua, umepiga hatua muimu ya kuaza kukabiliana na UKIMWI. Nikutie moyo, kwa dawa na huduma zillizopo, huna tofauti na wengi wetu. Nawajua watu wanaoishi maisha ya furaha, na yenye afya kwa zaidi ya 15 yrs. Nakutakia kila la heri kumpata mwenzako!
 
naamini katika miujiza ya mungu na kuwa hakuna linalomshinda mungu,jipe moyo,ishi kwa furaha na kusali,the future holds a surprise for you
 
Mkuu takugongea like nikiingia kwa lap,una moyo wa kishujaa , Mungu yu pamoja nawe mkuu! Salute..
 
Hiv sio mwisho wa maisha.....

Nakutakia upate mke mwema,
 
Heko kwa kupima kamanda. Nina mwaka wa 3 bado napangua tu tarehe za kupima. Nikifikiria tu huko naishiwa nguvu.
 
....ishu kama hii inabid uweke ur real name....
Kinyume na hapo ni vumbi tu...
 
Dauhhh
Yule wa kwanza ungemjulisha tu maana
Kama anao ataenda kuusambaza huko ....

Anyway
kila lakheri kumpata mtakae pendana....
 
Hebu tuulizane jamani,hivi ni wana jf wangapi tumepima? Kupima mchezo? Watu kibao wanapima na hawaendi kuchukua majibu.Ufunguo nikupongeze kwa busara yako ya kupima mara kwa mara,i can tell you it has saved your life.
Ushauri wangu:Tafuta daktari mmoja TU awe confidant wako,usitumie madaktari wengi,kazi yake ata monitor progress yako na kukupa ushauri wa mara kwa mara.Don't touch ARV's mpaka dokta akwambie.Kula vizuri , tumia multivitamins.
Kuhusu kuoa hilo wala sio tatizo mbona zipo dating agencies na websites where you can get hooked up na mrembo atakayekubali hiv status yako?
 
all the best kwani huu ugonjwa sio mwisho wa maisha..
Ni vema umejitambua na kuamua kuoa wengine.
Kama wote tungekuwa hivi...hali isingekuwa mbaya
 


Bishanga wewe umepima??maana wewe Baba Koku lol.
 
Mimi sikupi pole kaka yangu nakupa HONGERA kwa kupima na kuikubali hali yako. Wewe ni shujaa pengine kuliko wengi wetu humu. I salute you for that. Na kuonyesha ukomavu wako hukupenda kujificha, kwa kuwa unajua ungewaambukiza wengi. MUNGU akubariki kwa hilo na kukukirimia hitaji lako.
 
Kawaida tu ndugu yangu, wala si hatari kihivo!
Cha msingi zingatia masharti yote chini ya hali hiyo, kamwe usimwingize mtu kwa kutarajia, katika shida kama yako.
Ushindi wakwanza ulioufanya ni kukubaliana na hali hiyo...yanayofuata yote yanakuwa ni maisha ya kawaida!
 
Naweza kukuita jasiri, na unaonesha utaishi maisha marefu yenye amani inshallah. Ni wachache wanaojikubali walivyo, na wakachukua hatua za kuwalinda wengine.

Ushauri:
Si lazima umpate aliye positve pia, unaweza kumpata mke mwenye mapenzi ya kweli, UKAPATA USHAURI WA KITAALAMU mkaendelea kufurahia na mwenzi wako salama na mkapata mtoto/watoto wasio na maambukizi. Nasisitiza, hilo linawezekana baada ya kupata ushauri/maelekezo ya kitaalamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…