Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,655
Kilichotokea kimetokea huwezi kukibadilisha. Jukumu tulilonalo ni kujenga baadae mpya yenye matumaini na faraja. Kila mtu anapaswa kufahamu hilo.
Ni lazima tufundishe akili zetu kutafakari na kufuata yaliyo sahihi. Kila mtu anafanya makosa lakini kwa mtu mwenye busara huwa makini mno na njia zake. Anajua matendo yake huzaa matunda. Na ukiishafanya kitu umefanya ni vigumu kukirudisha. Kinachofuata ni majuto, na majuto ni mjukuu.
Busara ni mfalme tunapochukia ukweli na kuukumbatia uongo. Ukweli hutuadhibu. Kwasababu Mungu anapenda tuwe viumbe bora. Tunaponyooshwa ni kwa faida yetu. Kila wakati mambo yanapokwenda vibaya katika maisha yetu tunapaswa Kukaa na kutafakari ni wapi tumekosea na tunapojua tulipokosea ni wajibu wetu kubadilika.
Kama tulifanya makosa katika maisha yako huko nyuma bado tuna nafasi. Baadae iko kwaajili yako unaweza kubadili kitu sasa. Kitu kibaya ni kuendelea kufanya makosa. Milango ya mabadiliko iko wazi kabisa kwa kila mtu.
Sishangazwi watu wanabadilika na ni wajibu wetu sote kubadilika kama kuna mambo mabaya tunafanya .
Ni jukumu letu la kila siku kujitahidi kuwa binadamu wema. Na kutafuta amani kadiri tuwezavyo na watu wengine.
Kila mtu miongoni mwetu huwa tunatenda makosa lakini kinachomtenganisha mwenye busara na asiye na busara ni kurudia makosa.
Kwahiyo tunabadili njia zetu za maisha pindi tunapogundua mwelekeo wetu sio sahihi. Tunatafuta kilichochema ili kulinda roho zetu dhidi ya uharibifu.
Unapokuwa kiumri na busara lazima iongezeke ili uwe na uwezo wa kufundisha walio chini yako njia bora za maisha. Haya ndio matumaini ambayo kila mmoja wetu anapaswa kuwa nayo. Kuishi maisha yenye amani na utulivu yanayoongozwa na busara.