Sehemu ya 2.
Nilisoma shule 2 za msingi kwa sababu hizi,kwanza nianze na shule ya sanawari primary school,hii shule ipo sanawari kipindi kile nasoma kwenye hiyo shule,kulikuwa na walimu ambao sitakuja kuwasahau mwalimu mdee na mwalimu mollel yani sitakuja kuwasahau,(kunipiga kama ngoma nimekuwa mandonga,MUNGU awachape na nyie popote mlipo).
Hakuna kitu nilikuwa sipendi kama kubeba fagio na dumu la usafi,kuchomekea sharti la shule,kushika namba asubuhi,nilichapwa sana kuchelewa shule nakumbuka mpaka mikono ilikuwa inakufa ganzi,matako yote hayafai kwa viboko.
Ishu iliyonifanya nipate huamisho kwenda kaloleni,ni balaa ni lilo lizua shule,kipindi kile kulikuwa na utaratibu wa kunyeshea mauwa ya shule,kunyeshea uwanja ili uote majani,sasa katika harakati za kunyeshea kiwanja,sijui kitu gani kilinifanya nianze kuzungusha dumu niliokuwa natumia kuchotea maji mtoni,lilikuwa dumu la chuma la korie,sasa baada ya kumwaga maji nikaanza kulizungusha uku nami nikizunguka ghafla mkono wa lile dumu ulikuwa wa plastic ulichomoka,dumu hilo likaenda mpiga mwanafunzi mwenzangu wa kike kichwani,paah lilimpiga kichwani akaanguka chini.
Walitumwa kundi la wanafuzi kunishika ,wakanipeleka mpaka kwa mwalimu nilikula viboko hatari,yani kila mwalimu alinichapa nikaambiwa nikamuite mzazi,imagine mtoto wa darasa la 3 napewa suspension sio powa,niliondoka shule nikiwa naumwa kwa viboko vya wale walimu,nilipitia Buchani kwa brother nikamuelekeza akaniambia haina haja ya kumuelekeza mdingi,maana mdingi alikuwa katili anapiga mfano hakuna,nakumbuka kuna siku baba alinipiga mpaka nikazimia,basi brother akamuacha mtu auze Buchani.
Alikiuwa na piki piki kubwa 250 Honda,akaliwasha akaniambia panda tukaenda mpaka shule siku hiyo hiyo niliyorudishwa,walimu wakamuambia brother kuwa nimempiga mwanafunzi mwenzangu na dumu mpaka limemkata,brother akawaambia mwanafunzi mwenyewe yuko wapi,walimu wakajibu kashaenda hospital,brother akawauliza hospital gani??wakamwambia zahanati ya sanawari,brother akawaambia walimu tunarudi,kweli tumeenda mpaka hapo zahanati brother akalipa huduma zote za hospitality na akawapa wazazi wayule mtoto wa kike elfu 50,ambaye huyo mtoto wa kike niliyempiga na Kopo sasa hivi ni mke wangu,.
Itaendeleea..