Maisha yale hayatajirudia tena!

Maisha yale hayatajirudia tena!

APPROXIMATELY

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2021
Posts
2,035
Reaction score
2,737
Ndugu wana jamii habari zenu,ni jambo la kumshukuru MUNGU kuwa tunapumua bila kulipa ushuru, japo maisha magumu ila tunakomaa nayo maana tutamlalamikia nani?mwenyewe kasema '' usinichoshe tusichoshane''.

Mnajuwa nini ndugu zangu, kuna mda mwingine ukikaa chini ukiyatafakari maisha ya sasa na ya zamani unaona bora maisha ya zamani, ila ukifikiria hali ilivyo sasa unajikuta unapenda maisha ya sasa.

Katika harakati za ukuaji, haswa kwa mwanaume, ana pitia kipindi kigumu sana cha ukuuaji, ninaposema kipindi kigumu na maanisha hivi, mtoto wa kiume mpaka kukua anapitia maisha ambayo mwenyezi MUNGU anamnusuru na mambo mabaya mengi.

Napenda ni toe ushuhuda wa maisha niliyopitia nikiwa mdogo enzi zile, japo wengi huficha waliopitia ila mimi leo naweka bayana maisha yangu ya utotoni, naomba mfuatane nami katika mtiririko huu wa maisha ya mwanaume.

Kwa majina yangu ya kupewa na wazazi wangu naitwa David Alexandre ila kibongo bongo naitwa daudi, jamii forums MNanijua kama
APPROXIMATELY, nilizaliwa katika hospital ya mount meru iliyopo arusha, miaka ile ya 90 Na something.

Kipindi hicho wazazi wangu walikuwa wanaishi sekei, mama ni mchagga wa machame, baba ni maasai.

Tuna ndugu wengi sana, yani kwa sisi wa maasai tunamaboma mengi sana, kwa hapo sekei tunanyumba kibao, bado za ngaramtoni, arusha chini, sanawari na kisongo, wazee wetu walishika maeneo mengi Big up kwao.

Kwetu sisi mimi ni mtoto wa mwisho kwa mama yangu, ila baba ana wake 3 ambao wa kwanza ni mama yangu mwenye watoto 8, wa pili ni mama mdogo mwenye watoto 7, na watatu ni mama mdogo pia mwenye watoto 11, baba ni hatari anatimiza ile aya 'nendeni mkazaliane' babu yangu kwao walizaliwa watoto 36, baba ake na babu yangu alikuwa na wake 4, ndugu wa babu wamezinguka maeneo yote ya arusha ikiwemo iliboru, mianzini, kijenge, ngarenaro, matejoo, kijenge.

Mpaka hapo ushaona tulivyowengi arusha, nina ndugu zangu mwenye uwezo sana Alex yule mwenye mabucha kibao iliboru ni kaka mkubwa, nina kaka wengine wauza madini, wauza mazao jumla na reja reja, nimeandika haya ili uwe na uhalisia kidogo wa maisha ya arusha.

Katika kipindi cha ukuuaji nilipitia maisha ambayo yalikuwa ya hatari sana, sema ni neema za MUNGU tu leo hii nisingekuwa hapa duniani, ila namshukuru MUNGU kuniweka hai mpaka leo..

Chekechea nilianza nikiwa na miaka 3, nakumbuka nilikuwa najielewa kidogo ila sio sana, maana hata nyimbo za zamani nazikukumbuka kama mabata mabata wadogo, mwalimu wetu hapendi kelelee n.k,

Shule ya msingi nilisoma sanawari kwa darasa la 1 mpaka 3,ila darasa la 4 mpaka la 7 nilimalizia kaloleni.
Itaendelea......
 
Sehemu ya 2.

Nilisoma shule 2 za msingi kwa sababu hizi,kwanza nianze na shule ya sanawari primary school,hii shule ipo sanawari kipindi kile nasoma kwenye hiyo shule,kulikuwa na walimu ambao sitakuja kuwasahau mwalimu mdee na mwalimu mollel yani sitakuja kuwasahau,(kunipiga kama ngoma nimekuwa mandonga,MUNGU awachape na nyie popote mlipo).
Hakuna kitu nilikuwa sipendi kama kubeba fagio na dumu la usafi,kuchomekea sharti la shule,kushika namba asubuhi,nilichapwa sana kuchelewa shule nakumbuka mpaka mikono ilikuwa inakufa ganzi,matako yote hayafai kwa viboko.

Ishu iliyonifanya nipate huamisho kwenda kaloleni,ni balaa ni lilo lizua shule,kipindi kile kulikuwa na utaratibu wa kunyeshea mauwa ya shule,kunyeshea uwanja ili uote majani,sasa katika harakati za kunyeshea kiwanja,sijui kitu gani kilinifanya nianze kuzungusha dumu niliokuwa natumia kuchotea maji mtoni,lilikuwa dumu la chuma la korie,sasa baada ya kumwaga maji nikaanza kulizungusha uku nami nikizunguka ghafla mkono wa lile dumu ulikuwa wa plastic ulichomoka,dumu hilo likaenda mpiga mwanafunzi mwenzangu wa kike kichwani,paah lilimpiga kichwani akaanguka chini.

Walitumwa kundi la wanafuzi kunishika ,wakanipeleka mpaka kwa mwalimu nilikula viboko hatari,yani kila mwalimu alinichapa nikaambiwa nikamuite mzazi,imagine mtoto wa darasa la 3 napewa suspension sio powa,niliondoka shule nikiwa naumwa kwa viboko vya wale walimu,nilipitia Buchani kwa brother nikamuelekeza akaniambia haina haja ya kumuelekeza mdingi,maana mdingi alikuwa katili anapiga mfano hakuna,nakumbuka kuna siku baba alinipiga mpaka nikazimia,basi brother akamuacha mtu auze Buchani.
Alikiuwa na piki piki kubwa 250 Honda,akaliwasha akaniambia panda tukaenda mpaka shule siku hiyo hiyo niliyorudishwa,walimu wakamuambia brother kuwa nimempiga mwanafunzi mwenzangu na dumu mpaka limemkata,brother akawaambia mwanafunzi mwenyewe yuko wapi,walimu wakajibu kashaenda hospital,brother akawauliza hospital gani??wakamwambia zahanati ya sanawari,brother akawaambia walimu tunarudi,kweli tumeenda mpaka hapo zahanati brother akalipa huduma zote za hospitality na akawapa wazazi wayule mtoto wa kike elfu 50,ambaye huyo mtoto wa kike niliyempiga na Kopo sasa hivi ni mke wangu,.
Itaendeleea..
 
Tunaomba hii story uandike uimalize uzibe masikio kabisa maan kuna watu hapa ndani kuandika hawawezi lkn kweny story za wenzao wanatikisa matako tu.

Kua na roho
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom