Zero IQ
JF-Expert Member
- Dec 21, 2016
- 13,985
- 25,198
Uzi huu utakuwa updated kila mara kwa sababu moja tu nataka nicreat kitu ambacho vijana watakaokuja kusoma baadae inshalah kama forum yetu itazidi kuchanja mbuga wajue wapi mr Zero IQ alikotokea na wapi anakoelekea
Uzi ni kwa lengo moja tu nitaandika njia zote nilizopitia na nitakazopitia mpaka pale nitakapokuwa na maisha yanayoeleweka,
Kwanza nianze Mimi zero Iq siyo mtu msomi sana useme nimesoma mpaka majengo yatake kunibomokea hapana Elimu yangu ni Certificate in pharmaceutical science tu na sidhani kama nitaendelea zaidi ya hapo kwa sababu flani flani za uchumi
wa familia ukizingatia Ada ya mwaka mmoja tu kwenye hiyo kozi ni mtaji tosha,
Baada ya kumaliza hiyo certificate nilijitahidi kuomba omba kazi na ata hapa jf nilikuja na baadhi ya mabandiko yangu lakini sikufanikiwa,
Nilichofanya sasa baada ya hapo;
Baada ya kuona kazi hakuna na kitaa hapaeleweki kuna jamaa yangu alikuwa na lile jiko la kuchomea mahindi nilimuazima na kuanza kuchoma mahindi kwenye kijiwe,
Baada ya kuona biashara inaenda vizuri kuna jamaa nao walianzisha na wao pale kijiweni hivyo kukawa na changamoto,
Baada ya kuona hivyo mi nikaachana na mahindi nikaanza kuchoma mishikaki ,kiukweli nilivyogeukia mishikaki ilikuwa inanilipa nusu kwa nusu yaani kama nyama ya elfu 15 basi lazima nikimaliza nipate faida ya elfu 15,
Ukitoa zile stick za kuchomea na mkaa kwa siku nilikuwa nalaza kwenye elfu 10 mpaka 12 , nilifanya ile kazi kwa muda kidogo huku najiwekea akiba ,
Nilidunduliza kwa kujibana mpaka ile Akiba yangu ikafikia laki 5,
Nikaichukua na kuingia sokoni na kununua,
1:Kabati la aluminium kwa sababu ya kufungua kijiwe cha chipsi sh. laki na Nusu (150000)
2:Jiko la kuchomea mishikaki elfu 45
3:Jiko la kukaangia chipsi la mkaa elfu 35
4:Meza ndogo ya plastick elfu 15
5:Meza ya mbao ya kuwekea kabati elfu 45
6:Viazi gunia elfu 53
7:mafuta ya kula ndoo ndogo 33
8:Mkaa gunia elfu 28
9Karai,sahani,keni Na Nk. Gharama ni kawaida tu kama elfu 40 hivi,
Baada ya hapa nikatafuta eneo nikawa nalipia elfu 30 kwa mwezi nikafungua kijiwe,
Ofcourse biashara ilikuwa inaenda sana japo changamoto nazo hazikosekani Baada ya kama miezi miwili hivi ya kazi nikapata tatizo pale kwenye familia yetu
Baada ya kujipiga piga hapa na pale nikayumbisha mtaji maana kwetu mi ndio pekee mtoto wa kiume alafu macho yote kwangu ilifikia hatua nilitamani kuuza vile vifaa ili tu nipate hela ya kusove lile tatizo lililojitokeza
Nilileta bandiko hapa la kuuza Vifaa vya chipsi lakini napo pia sikupata mteja ,
Baada ya muda kidogo kupita kuna jamaa alinikopesha hela kwa miadi ya kumlipa nikianza biashara kweli nilisave lile jambo nikafungua na kuendelea na ile biashara ya chipsi,
Baada ya muda kweli nilipata ile hela nikamrudishia jamaa mi nikaendelea na biashara muda huo wote nilikuwa nakomaa tu mwenyewe,
Baada ya kukaa mzigoni nikapata kiasi kidogo cha pesa nikaamua kuwekeza kwenye banda jingine la chipsi na kumuweka dogo afanye kazi pale,
Huko kwenye banda la pili biashara siyo haba nayo naona inaenda enda na malengo yangu ni kufungua banda la tatu if god wish soon as possible
Ninavyoongea hapa na kuandika Uzi huu ni kwamba Mimi Zero Iq sina hela za kusema nina hela ila nashukuru mungu ya kununulia Vocha napata ipo siku wish nitakuja kuzikamata Kanuni yangu ni moja tu Hakuna kukata Tamaa kamwe ata jamii nzima isimame na kunicheka ,
Update zote nitazitupia hapa kila nitakachokifanya mpaka pale nitakapofikia........!
Maswali pia Nitajibu.