Wnanajamii, Salamu!
MASWALI -
1. Tunadhani tunaitendea haki nchi yetu kwa kukaa nchi za watu na kufanya kazi huko?
2. Endapo wote walio nje wangerudi TZ na kuwekeza elimu na mali zao, pamoja na hasira waliyonayo juu ya Ufisadi, umasikini je nchi yetu ingebaki hapo hapo ilipo kwa sasa?
3. Ni nini changamoto za kuishi ughaibuni, mazuri yake je? Yapi yana uzito zaidi?
4. Nini unawashauri wanaotaka kurudi TZ na wanaotaka kwenda Majuu?
KARIBUNI TUELIMISHANE!
Hii topic ni sensitive sana kwa maana kila mtu anatafuta maisha anapoona panamfaa bila kujali nani anasema nini. Isitoshe hakuna nchi iliyoendelea bila ya watu wake kutoka kwenda kutafuta na kuleta.Ndiyo maana kuna akina Vasco da Gama, Christopher Columbus,Magellan,Diego Cao, na wengine waliothubutu kutoka na kusafiri umbali mrefu kwa kutumia usafiri wenye kutisha na kupambana na shida, mikasa na dhoruba mbalimbali.Maswali uliyouliza hayana majibu rahisi.
1. Tunadhani tunaitendea haki nchi yetu kwa kukaa nchi za watu na kufanya kazi huko?
Kwani ni nani anapima huo utendaji haki? Haki ya nani dhidi ya nani? Kuna watu wameenda ng'ambo kwe fedha zao wenyewe bila sponsorship ya serikali. Wako waliouza mali zao ili wapate fedha za kuwapeleka huko waliko.Wasiporudi sidhani watakuwa wamemkosea mtu. Kuna wale waliosaini bond na serikali kwamba watapelekwa kusoma na wakimaliza watarudi kujenga taifa. Hawa wasiporudi labda kunaweza kuzua maswali.Lakini mwisho wa yote ni kwamba KILA MTU ANA HAKI KUTAFUTA MAISHA POPOTE.NI UAMUZI BINAFSI KWA MAANA HATA WATU WAKIRUDI, HIYOHIYO SERIKALI HAIJALI WATAENDESHA VIPI MAISHA YAO.
2.Endapo wote walio nje wangerudi TZ na kuwekeza elimu na mali zao, pamoja na hasira waliyonayo juu ya Ufisadi, umasikini je nchi yetu ingebaki hapo hapo ilipo kwa sasa?
WOTE HAWAWEZI KURUDI THATS FOR SURE. ISITOSHE KIWANJA KILICHOPO HAKITUTOSHI WOTE KWA MAANA, MAFISADI WALISHAJINYAKULIA KARIBU KILA KILICHOPO- KWA MAANA YA RASILIMALI NA FURSA ZILIZOPO. UWEKEZAJI HATA KWA WALIO NDANI YA NCHI TAYARI NI KITENDAWILI - UFISADI KUUTOKOMOMEZA NI KAMA NDOTO KWA MAANA NI LIJISARATANI LILILOKWISHA SAMBAA KILA MAHALI.UTAKATA NINI UACHE NINI.
UMASKINI WA NCHI HII UMEKUWA CREATED NA WACHACHE - WANAOJILIMBIKIZIA MALI KWA KUNYAKUA KILA KILICHOKO MBELE YA MACHO YAO - MAPORI,MADINI/MACHIMBO,MISITU,NYADHIFA,RASILIMALI FEDHA,N.K.ISINGEKUWA HIVYO BASI WANANCHI WANGEKUWA NA NAFUU YA MAISHA.
3. Ni nini changamoto za kuishi ughaibuni, mazuri yake je? Yapi yana uzito zaidi?
MAISHA NI POPOTE - NA CHANGAMOTO HAZIKOSEKANI.KINACHOJALISHA NI JINSI YA KUPAMBANA NAZO
4.Nini unawashauri wanaotaka kurudi TZ na wanaotaka kwenda Majuu?
HUWEZI KUUJUA UTAMU WA NGOMA HADI UMEICHEZA.USHAURI - ANAYEWEZA AJARIBU ASINGOJE KUSIMULIWA.
Jirani, habari za masiku tele jirani. Naona ulipotea mtaani maana nilikuwa nikiangaza angaza huku na kule labda nitaiona ile MB 450 SE Metallic in Colour ikiingia au kutoka kwenye crib yako lakini kwa siku kadhaa sasa sikufanikiwa kuiona. Karibu tena jamvini kwetu J. Hii topic kama ulivyosema ni very sensitive, nafasi ikiniruhusu leo baadaye nitachangia kwa kirefu.
MASWALI -
1. Tunadhani tunaitendea haki nchi yetu kwa kukaa nchi za watu na kufanya kazi huko?
2. Endapo wote walio nje wangerudi TZ na kuwekeza elimu na mali zao, pamoja na hasira waliyonayo juu ya Ufisadi, umasikini je nchi yetu ingebaki hapo hapo ilipo kwa sasa?
3. Ni nini changamoto za kuishi ughaibuni, mazuri yake je? Yapi yana uzito zaidi?
4. Nini unawashauri wanaotaka kurudi TZ na wanaotaka kwenda Majuu?
KARIBUNI TUELIMISHANE!
WoS,
Hata kabla ya kushamiri kwa Ufisadi, watu walikua wana hamu ya kwenda majuu..... wakayaacha hayo mapori na rasilimali wajanja wajitwalie.....
Jirani...nilikuwa nikiangaza angaza huku na kule labda nitaiona ile MB 450 SE Metallic in Colour ikiingia au kutoka kwenye crib yako...Haya jirani baadaye basi.
Wnanajamii, Salamu!
Napenda tujadili jambo ambalo kwa muda mrefu nimelitafakari. Kuna kipindi fulani, na hata sasa vijana wengi wa viwango tofauti tofauti vya elimu walikuwa na homa kubwa sana ya kutaka kwenda Majuu, hususan nchi za Marekani na Uingereza, ili kusoma au kutafuta maisha. Wengi walienda, baadhi wamerudi, wapo ambao wanataka kurudi na wengine wameapa kabisa kuwa hawatarudi kamwe.
Kwenda majuu imekuwa kama suala la Ndoa-wapo wanaotaka kuingia na wapo wanaotaka kutoka. Katika makundi yote hayo mawili, kuna wale ambao hawajui waanzie wapi kurudi, wataonekanaje, na wale amabo hawajui wataendaje. Wanaotaka kwenda na wanaotaka kurudi wote wanajiona wana haki ya kufanya hivyo na ni sahihi.
MASWALI –
1. Tunadhani tunaitendea haki nchi yetu kwa kukaa nchi za watu na kufanya kazi huko?
2. Endapo wote walio nje wangerudi TZ na kuwekeza elimu na mali zao, pamoja na hasira waliyonayo juu ya Ufisadi, umasikini je nchi yetu ingebaki hapo hapo ilipo kwa sasa?
3. Nini changamoto za kuishi ughaibuni, mazuri yake je? Yapi yana uzito zaidi?
4. Nini unawashauri wanaotaka kurudi TZ na wanaotaka kwenda Majuu?
KARIBUNI TUELIMISHANE!
Unaweza kuchangia maendeleo ya nchi yetu popote pale ulipo duniani na mara nyingi kama wewe ni mfanya kazi basi uwezo huo huongezeka zaidi kama unafanya kazi yenye kipato kikubwa ukilinganisha na kile cha Tanzania. Tukumbuke nchi za Mexico na China mapato yao makubwa katika fedha za kigeni yanatokana na remittances zinazotumwa na wananchi wa nchi hizo ambao wamehamia nchi nyingine duniani. Kenya miaka michache iliyopita ilipokea remittances iliyokaribia $500 miiloni kwa mwaka mmoja tu kutoka kwa Wakenya waliohamia kufanya kazi au biashara katika nchi mbali mbali duniani. Kiasi hicho kilikuwa ni kikubwa kuliko hata misaada na mikopo ikijumlishwa pamoja katika mwaka ule. Kwa hiyo kwa kumalizia kuna mazuri mengi kwa wananchi wa Tanzania hasa wenye elimu ya juu kufanya kazi nchi za nje kwao binafsi kama individuals na pia kwa nchi yetu kutokana na remittances wanazozituma kufanyia mambo mbali mbali ikiwemo kusaidia ndugu, jamaa na marafiki. Mkipata nafasi hizo wala msizilazie damu.
Unaweza kuchangia maendeleo ya nchi yetu popote pale ulipo duniani na mara nyingi kama wewe ni mfanya kazi basi uwezo huo huongezeka zaidi kama unafanya kazi yenye kipato kikubwa ukilinganisha na kile cha Tanzania. Tukumbuke nchi za Mexico na China mapato yao makubwa katika fedha za kigeni yanatokana na remittances zinazotumwa na wananchi wa nchi hizo ambao wamehamia nchi nyingine duniani..[/b]
Linganisha haya:
Mtu mwenye high school diploma nyamwezi na mtu mwenye high school diploma bongo
Mtu mwenye digrii moja, mbili, au tatu nyamwezi na mtu mwenye digrii moja, mbili, au tatu bongo
Homeless wa nyamwezi na homeless wa bongo
Raisi wa nyamwezi na raisi wa bongo
Mbunge wa nyamwezi na mbunge wa bongo
Welfare recipient wa nyamwezi na welfare recipient wa bongo (wait a minute najua hakuna hii bongo)
Mbeba boksi wa nyamwezi na mbeba boksi wa bongo
Yupi mwenye nafuu zaidi?