Maisha ya UBUNTU na Kanuni zake 4

Bon Bantu

New Member
Aug 4, 2021
1
0
Filosofiasoko pekee Afrika inayokamilishana na UBUNTU kutegua kitendawili mama cha familia za waAfrika tangu mataifa ya Afrika tuanze kupata uhuru (Libya 1951) zaidi ya nusu karne iliyopita .

"Jinsi ya kupunguza ugumu wa maisha na kuongeza amani na furaha ya familia za waAfrika kwa kupata mfumo utakaojenga, thabiti na kuongeza mzunguko wa pesa na masoko ya bidhaa na huduma za kipekee sana tunazovumbua, kubuni, kuumba na kuzalisha Afrika"


Kwa uchunguzi wa Bon Bantu kitendawili mama cha waAfrika karne ya 20 ilikuwa ni:

"Jinsi ya kupata mfumo utaokaleta uhuru wa maTaifa ya Afrika toka katika mikono ya wakoloni"

Tunawashukuru wazee wetu karne ya 20 kwa vita na maarifa waAfrika tuko huru katika mpambano wa ligi kuu ya wanadamu duniani, mpambano wa ridhiki ya dunia.

Kitendawili mama cha kizazi chetu karne ya 21 ni:

"Jinsi ya kupunguza ugumu wa maisha na kuongeza amani na furaha ya familia zetu waAfrika kwa kupata filosofiasoko itayojenga, thabiti na kuongeza mzunguko wa pesa na masoko ya bidhaa na huduma tunazovumbua,kubuni, kuumba na kuzalisha Afrika"

Baada ya uchunguzi wa zaidi ya miongo miwili katika mifumo ya mzunguko wa pesa duniani na Afrika Bon Bantu akiwa katikati ya kilele cha furaha mwaka 2021 anatambua na kutambulisha filosofiasoko ya pekee Afrika inayokamilishana na UBUNTU kujenga, kuthibiti na kuongeza mzunguko wa pesa na masoko ya bidhaa na huduma zinazovumbuliwa, kubuniwa, kuumbwa na kuzalishwa katika familia za vijiji na mitaa ya bara la Afrika "filosofiasoko ya MAISHA YA UBUNTU na KANUNI ZAKE 4"

Bon Bantu anatambulisha filosofiasoko hii kama ustaarabu wa maisha ya familia za maJirani waAfrika tunaozingatia kanuni 4 katika mahusiano na ushirikiano wa kukamilishana mitaji (Ubunifu, Ufundi, Nguvukazi, Teknolojia, Ardhi,Vifaa, Mitambo,Fedha n.k) katika miradi (viwanda,ujenzi, teknolojia n.k) na katika manunuzi ya bidhaa na huduma za ubora wa kipekee sana tunazovumbua, kubuni, kuumba na kuzalisha katika vijiji na mitaa ya Afrika.

Kanuni 4 za ustaarabu wa MAISHA YA UBUNTU

Kanuni Na 1.
Familia za maJirani waAfrika tununue bidhaa na huduma za mahitaji ya kila siku ya familia zetu zile tu tumeshindwa kuvumbua, kubuni, kuumba na kuzalisha na tununue mahitaji haya kwa maJirani zetu katika vijiji na mitaa ya Afrika wanaozalisha bidhaa na huduma za uraibu wetu katika kijiji na mitaa ya Afrika. Kanuni hii inajenga msingi wa kuongeza mzunguko wa pesa katika familia, vijiji na mitaa ya Afrika.

Kanuni Na.2
"Familia za maJirani waAfrika katika vijiji na mitaa ya Afrika tukamilishane katika manunuzi kwa kuvumbua, kubuni, kuumba na kuzalisha bidhaa na huduma zinazoushinda uraibu wetu katika manunuzi ya mahitaji ya kila siku ya familia zetu."

Kanuni Na.3
Familia za maJirani waAfrika katika vijiji na mitaa ya Afrika tukamilishane mitaji (Ubunifu, Ufundi, Nguvukazi, Teknolojia, Ardhi, Vifaa, Mitambo, Fedha n.k) katika kutekeleza miradi (viwanda, karakana za bidhaa/huduma za mahitaji ya kila siku ya familia) kwa lengo la kugawana faida kulingana na mtaji wa kila Jirani wa mradi. Tutumie teknolojia ya kisasa ya mawasiliano ya wazi (kwa kukumia program tumishi maalum katika simu) kuthibitisha uadilifu katika kukamilishana mitaji,wakati wa kutekeleza miradi na katika kugawana faida kulingana na thamani ya mtaji wa kila jirani wa mradi.

Kanuni Na.4
Familia za maJirani waAfrika tutambulishe bidhaa na huduma zetu katika soko la Afrika dunia kwa lugha(rangi,nembo) maalum.

Katika lugha ya filosofiasoko hii pekee Afrika, maJirani waAfrika ni familia za waAfrika tunaozingatia kanuni 4 katika mahusiano na ushirikiano wa kukamilishana mitaji katika miradi na katika manunuzi ya mahitaji ya kila siku ya familia zetu katika vijiji na mitaa ya Afrika.

Kwa uchunguzi wa Bon Bantu , maTaifa yaliyofanikiwa kujenga mzunguko mkubwa wa pesa katika maTaifa yao wamechukua hatua mbili muhimu:

1.Kukamilishana na sekta binafsi kuhamisha maarifa ya dunia katika mapinduzi ya viwanda, teknolojia na mawasiliano

2.Kujenga filosofiasoko inayowaongoza kuteka kwa awamu sehemu kubwa ya mzunguko wa pesa katika sekta 10 zinazaoongoza mzunguko wa pesa wa dunia kwa kuvumbua, kubuni,kuumba na kuzalisha bidhaa na huduma zinazoushinda uraibu wa wanunuzi duniani katika sekta za

1. Teknolojia
2. Mawasiliano
3. Ujenzi
4. Burudani, utalii na michezo
5. Chakula
6. Afya
7. Madini
8. Nishati
9. Mavazi na
10. Huduma za fedha

Kwa uchunguzi wa Bon Bantu waAfrika katika maTaifa ya bara la Afrika kufikia karne ya 21 tumefanikiwa kujenga na kuhamisha maarifa ya kutosha kukamilishana na dunia kuvumbua, kubuni, kuumba na kuzalisha bidhaa na huduma za mahitaji ya kila siku ya familia zetu Afrika.Kitendawili kigumu kimebaki kupata filosofiasoko itakayopindua meza za filosofiasoko za ng'ambo hasa filosofiasoko toka ng'ambo ya mashariki iliyoteka na kuhamisha sehemu kubwa ya mzunguko wa pesa katika masoko na magulio ya mitaa na vijiji vya Afrika "filosofia ya kuvumbua, kubuni, kuumba na kuzalisha bidhaa na huduma za ubora na viwango kwa uwiano wa uwezo wa wanunuzi duniani"

Kwa uchunguzi wa Bon Bantu ni filosofiasoko ya ustaarabu wa MAISHA YA UBUNTU na KANUNI ZAKE 4 pekee karne ya 21 inayopindua meza ya filosofiasoko za ng'ambo na kusimamisha meza ya soko la bidhaa na huduma za kipekee sana Afrika zinazovumbuliwa, kubuniwa, kuumbwa na kuzalishwa katika vijiji na mitaa ya Afrika hivyo kutegua kitendawili mama cha familia za waAfrika kwa kujenga,kuthibiti na kuongeza mzunguko wa pesa na masoko Afrika.
 
Back
Top Bottom