StormTrooper
Member
- Jul 18, 2018
- 17
- 12
Chemistry bhana...nakumbuka unaingia exam room unakuta swali hujawahi kusikia tangu form one... Unaenda swali la pili linasema explain your answer in question one above...unaishiwa nguvu unasonga swali la tatu...kumbe linasema discuss your answer in question number two... Unawaangalia wenzako walio karibu na wewe ni vilaza bora wewe...unaona hamwezi discuss... Unaenda swali la nne wanauliza two types of bonds na wewe unajua ni eurobond na james bond pekee unauma kalamu... Kidogo unasikia mwenzako anaomba extra paper unashindwa kuelewa wewe umelogwa ama nini??? Kabla huyo kukaa mwingine anasimama na kusema swali la saba lina shida na ni hilo pekee uli calculate ukapata 0.076524. Unaamua kulalia meza na unaota kuna mjomba ako yuko jeshi ataku organaizia uingie jeshini after chuo...unaamka ghafla unapokumbuka kumbe mjomba ako ni wa jeshi la wokovu..
