Torch
JF-Expert Member
- Aug 11, 2013
- 1,205
- 1,139
- Thread starter
- #61
Kudhumiiwa labda anahisi!
Kwenye hizo barua alizomuandikia DPP,sicho kiachotakiwa. Hapo fursa ya kuandika barua za msamaha na kulipa hajaitumia vizuri. Wanasheria wake wamempoteza. Hiyo barua aliyoandika kwa DPP inaenda kisheria zaidi,maana yake anataka kuendelea na kesi.
My take: Bado anayo nafasi aandike barua nyingine aombe msamaha na alipe tu kiasi kinachotakiwa.
1. Hizi hela zinatafutwa tu,ya nini uumie kwa ajili ya pesa?.
2. Bado hata akirudisha trillions kadhaa,nina uhakika bado atabakiwa na trillions zingine kadhaa,pamoja na miradi yake.
3. Yeye umri umeenda sana,kuna haja gani ya kujiumiza kwa ajili ya pesa uwe nazo nyiiiingi ili iweje katika huo umri?.
Sent using Jamii Forums mobile app