Maisha ya Osama kabla hajakamatwa yafichuliwa

Shine

JF-Expert Member
Feb 5, 2011
11,481
1,364
Osama-bin-Laden-532x300.jpg

TUME ya Abbottabad imesema kuwa Osama bin Laden aliishi kama mtu wa kawaida bila wasiwasi wowote kwa karibu miaka 10 na aliwahi hata kusimamishwa na polisi katika eneo la Swat huko Pakistan kwa kupeleka gari kwa kasi mno, lakini hakukamatwa.
Ripoti hiyo iliyofichuliwa na Televisheni ya al Jazeera na kuoneshwa juzi jioni, inaonesha kinagaubaga maelezo ya kusisimua kuhusu maisha ya Osama bin Laden, mtu hatari aliyekuwa akitafutwa kwa udi na uvumba, na aliyekuwa akivaa kofia la mchunga ng’ombe katika tambarare za Marekani, kuepuka kugunduliwa kutoka angani.
Ripoti hiyo ya kurasa 336, iliandikwa na tume ya Abbottabad inayoongozwa na jaji na iliyoundwa na Serikali ya Pakistan muda mfupi baada ya vikosi maalumu vya Marekani kumuua bin Laden Mei 2 mwaka 2011. Misingi ya ripoti hiyo ni mahojiano yaliyofanywa na vyanzo 201, wakiwemo jamaa wa familia yake na maofisa mbalimbali.
Matokeo ya uchunguzi huo ambayo hayajachapishwa rasmi, yanajumuisha ushahidi wa uzembe mkubwa katika karibu kila ngazi ya vyombo vya usalama vya Pakistan.
Ripoti inakosoa vikali namna Marekani ilivyofanya uvamizi katika makazi ya bin Laden huko Abbottabad, ikisema ilichukua hatua kama jambazi mhalifu. Inauweka katika kiti moto utawala wa Pakistan kwa kushindwa kugundua shughuli za Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA), katika ardhi yake, na hautupilii mbali uwezekano wa kuhusika maofisa walaghai katika idara ya ujasusi ya Pakistan, suala tete kuligusia katika uchunguzi wa hali ya juu namna hiyo.
Ripoti inatoa maelezo kuhusu usiku wa kifo cha bin Laden na kutoa taswira ya mtu aliyekuwa akibabakia na kama mwenda wazimu ambaye kila mara alikuwa mbioni kukwepa kutiwa mbaroni.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Bin Laden aliwasili nchini Pakistan msimu wa machipuko mnamo mwaka 2002, na wakati mmoja aliishi Haripur kwa miaka miwili kabla kuhamia katika makazi yake ya mjini Abbottabad na familia yake kubwa mnamo Agosti 2005.
Ripoti inasema maeneo yote alikoishi hayajulikani kikamilifu, lakini miongoni mwao ni FATA yani Waziristan kusini na Bajaur, Peshwar, Swat na Haripur.
Ripoti imegundua bin Laden aliingia Pakistan akitoa eneo la Tora Bora nchini Afghanistan, ambako majeshi ya Marekani yalikuwa yakimsaka mwaka 2002. Familia yake ilihamia Karachi, Pakistan kutoka Kandahar, muda mfupi baada ya mashambulio ya Septemba 11, 2001 nchini Marekani dhidi ya jengo la Shirika la Biashara la Kimataifa (WTO) mjini New York, makao makuu ya wizara ya ulinzi, Pentagon nje ya mji wa Washington, na uwanja mmoja huko Pennsylvania.
Osama hakupenda mali
Katika ushuhuda wao wake wa bin Laden walisema hakupenda sana mali zake binafsi na alikuwa na nguo chache sana. Ripoti hiyo imesema kabla kwenda Abbottabad bin Laden alikuwa na mavazi matatu ya kitamaduni yajulikanayo kama shalwar kameez aliyoyavaa wakati wa msimu wa kiangazi na mengine matatu kwa ajili ya msimu wa baridi.
Wakati alipojihisi anaugua, Osama bin Laden alijitibu mwenyewe kutumia dawa za kienyeji za Kiarabu. Kwa mujibu wa ripoti zisizo rasmi za Marekani, bin Laden alikuwa akiugua ugonjwa wa Addison, upungufu wa adrenalini mwilini, na kila mara alipojihisi mvivu angekula tufaha na chokoleti.
Maofisa wa Serikali na usalama nchini Pakistan hawakuweza kupatikana ili kutoa kauli kuhusu ripoti hiyo. Baadhi ya maofisa wa Marekani wameelezea wasiwasi wao wakiyashuku mashirika ya ujasusi ya Pakistan kwa kumlinda bin Laden, lakini Pakistan imelipuuzilia mbali wazo hilo.
 
Osama alikua na roho ya aina yake.
Alijua iko siku watamtia mkononi ndio maana hakujisumbua kujilimbikizia mimali.[/QUOTE

Yawezekana ila kwa maisha yake ya kujificha na kutokudumu shm ingemwia vigumu kujilimbikizia mali kama akina lowasa waloko na uhakika wa kulindwa na serikali
 
sasa hivi naona hali imetulia baada ya huyu jamaa kuuawa, kuna jamaa mmoja ndio sasa hivi amechukua nafasi ya Osama anaitwa Zawahir lakini hakuna kitu...

Al Qaeda kwa sasa hawafanyi milipuko ya kijinga kijinga

hapo ndipo ninapowakubali CIA wanapiga shughuli zao bila hata intelligence ya Pakistan kushtuka...

CIA hawa ndio wanajua kazi sio kama TISS ya Tanzania ni ya kijinga sana...

wenyewe wanachojua ni kung'oa watu kucha na meno badala ya kulinda raia...

Bomu limelipuka Arusha lakini hadi leo hii ni ubabaishaji mtupu yaani hawa TISS hakuna kitu...

CIA hawa jamaa ni noma...
 
osama walimkamata kwa shida katika report ya CIA ambayo siri zake zilivuja ni kwamba osama alikuwa na connection ya zaidi ya watu 20 ili uweze kufika au kitu kiweze kumfikia na pale tu walipombana yule bwana wa gereza la guantanamo na kuwaambia msihangaike na osama anzeni na network ya kutoka kwa fulani mwishowe mtampata , na mpaka leo ndiyo maana wamerakani wanahisi lile gereza lina mchango mkubwa katika kufanikisha maswala ya kiugaidi
 
Kweli mkuu ila nadhani TISS wangekuwa huru yani bila influence ya kisiasa siyo wabaya wanao uwezo wa kujitosheleza mfano angalia serikali ya awamu ya tatu kama walikuwa wakifanya kazi kwa makelele kibao ila ilikuwa vitendo tu
 
osama walimkamata kwa shida katika report ya CIA ambayo siri zake zilivuja ni kwamba osama alikuwa na connection ya zaidi ya watu 20 ili uweze kufika au kitu kiweze kumfikia na pale tu walipombana yule bwana wa gereza la guantanamo na kuwaambia msihangaike na osama anzeni na network ya kutoka kwa fulani mwishowe mtampata , na mpaka leo ndiyo maana wamerakani wanahisi lile gereza lina mchango mkubwa katika kufanikisha maswala ya kiugaidi

Kwa hakika ni kazi nzuri sana kwani alquda sasa wamebakia historia na hawana nguvu tena
 
sababu nyingine iliyo sababisha kuchelewa kukamatwa/kuuwawa kwake,ni kwamba jamaa aliachana kabisa na matumizi ya simu/email ktk kupashana taarifa na makamanda/washirika wake.hivyo ilikuwa vigumu kwa cia kuweza kum truck kirahisi.
 
sasa hivi naona hali imetulia baada ya huyu jamaa kuuawa, kuna jamaa mmoja ndio sasa hivi amechukua nafasi ya Osama anaitwa Zawahir lakini hakuna kitu...

Al Qaeda kwa sasa hawafanyi milipuko ya kijinga kijinga

hapo ndipo ninapowakubali CIA wanapiga shughuli zao bila hata intelligence ya Pakistan kushtuka...

CIA hawa ndio wanajua kazi sio kama TISS ya Tanzania ni ya kijinga sana...

wenyewe wanachojua ni kung'oa watu kucha na meno badala ya kulinda raia...

Bomu limelipuka Arusha lakini hadi leo hii ni ubabaishaji mtupu yaani hawa TISS hakuna kitu...

CIA hawa jamaa ni noma...[/QU

TISS HAINA TOFAUTI NA GREEN GUARD
 
ni kweli kabisa mkuu, TISS wamebaki kujisifu tu hamna kitu hawana tofauti na greenguard
 
osama walimkamata kwa shida katika report ya CIA ambayo siri zake zilivuja ni kwamba osama alikuwa na connection ya zaidi ya watu 20 ili uweze kufika au kitu kiweze kumfikia na pale tu walipombana yule bwana wa gereza la guantanamo na kuwaambia msihangaike na osama anzeni na network ya kutoka kwa fulani mwishowe mtampata , na mpaka leo ndiyo maana wamerakani wanahisi lile gereza lina mchango mkubwa katika kufanikisha maswala ya kiugaidi

Acha uwongo, mbona report ya mission yake ilishawekwa wazi tokea alipouwawa kaisome acha stori za vijiweni. Taarifa za Osama zilitolewa na detainee watatu wa alqueda waliopo Guantanamo. wa kwanza ni Mastermind wa 9/11 Khaleed Sheikh Mohamed (KSM), huyu ndie alimtaja Courier wa Osama ajulikanaye kwa jina la Al Kuwait ambaye ndiye anaebeba maelekezo na mawasiliano yote kutoka kwa osama na kupeleka kwa foot soldiers, Wa pili kumtaja Al Kuwait ni Abu Zubeida, Huyu Abu zubeida pamoja na Ramzi Yousef ndio waliolipua WTC kabla ya 9/11. Abu zubeida kwanza aliteswa na CIA kwa kutumia Enhanced Interogation techniques kama water borne akagoma kutoa information yoyote, mpaka CIA wakamtishia kumkabidhi kwa intelligence ya Saudi Arabia wakiamini ataogopa maana Saudi Arabia wanajulikana kwa kutesa, wakashangaa anawaambia wampeleke Saudi. Hapo ndio CIA wakacheza trick wakampakiza kwenye ndege na kuzunguka naye muda mrefu angani wakijifanya wanampeleka Saudi Arabia mwisho wakatua naye sehemu hukohuko marekani wakawachukua maofisa wa CIA waarabu wakiwa na nguo za jeshi la Saudi Arabia wakaanza kumuuliza maswali hapo ndio akamtaja Al Kuwait, halafu akawataja wafadhili wa Osama akiwepo Mtoto wa mfalme wa Saudi, Generali wa Jeshi la Saudi na maofisa wengine wawili wa serikali ya Saudi na akawapa namba ya motto wa mfalme wampigie ili awaamrishe wamwachie. watu wote waliotajwa na Abu zubeida CIA waliwaua kuanzia mtoto wa mfalme alikutwa amekufa akiwa vacation, yule General wa jeshi alikutwa amekufa jangwani kwa kiu na kukosa maji na wale maofisa wote. Huo ndio ukawa mwanzo wa Osama kukosa hela (financial suffocation). wakaanza kumfuatilia Al Kuwait Pakistani wakamtrace akitokea sokoni hadi nyumba aliyokuwa akienda Abbottabad. Osama aliishiwa hela mpaka wake zake walikuwa wanaenda kwa sonara wanauza mikufu na herein zao ili wapate hela ya kula. Ndio CIA wakamkodia nyumba karibu na nyumba ya Osama Afisa wake aliyekuwa anafanya kazi katika Shirika la Save the Children ambalo lilikuwa linafanya kampeni ya kinga ya magonjwa ya watoto. Na sio kwamba eti marekani walikuwa wanachukua DNA za watoto na ku-match na za Osama huo ni uwongo kwa sababu kinga iliyokuwa inaratibiwa na Save the Children ilikuwa ni ya Matone sasa kuwapa watoto matone uta-extract vipi DNA. Aliyebaki sasa ni second in command wa alqaeda daktari wa Misri Ayman Al Zawahil ambaye naye inaaminika amejificha kwenye mpaka wa Afg na Pak.
 
hawa jamaa CIA ni noma... wako safi sana shukrani sana mkuu kwa maelezo zaidi, sasa hapo picha ndio inakuja vizuri sana...
 
kipi nimekosea kueleza kwa kirefu ama kifupi source ni guantanamo chain ya osama na upatikanaji wa huduma ndiyo walianza nayo kabla ya mengineyo na walibaini mengi mno mkuu zaidi ya hayo ambayo mpaka leo wanaendelea kuchunguza
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom