carbohydates
Senior Member
- Oct 13, 2026
- 197
- 411
Iran, Saudi Arabia, Pakistan na Uturuki zimekubaliana kuendeleza mashauriano ya kiusalama na kuimarisha ushirikiano wa kikanda kufuatia mazungumzo ya ngazi ya juu yaliyofanyika mjini Tehran, Iran, Jumatatu.
Hatua hiyo inakuja wakati kukiwa na hofu ya kuibuka tena kwa mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran, pamoja na kuongezeka kwa mashambulizi ya Wahouthi dhidi ya Saudi Arabia.
Taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya mkutano huo wa kwanza kati ya Iran na wawakilishi waandamizi wa nchi hizo, imesema pande hizo zimekubaliana kuendeleza mazungumzo kuhusu amani, usalama na utulivu wa kikanda.
Mkutano huo uliandaliwa na Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, Mohsen Rezaei, na kuhudhuriwa na Waziri wa Ulinzi wa Saudi Arabia, Prince Khalid bin Salman, Mkuu wa Jeshi la Pakistan, Asim Munir, pamoja na Mkuu wa Idara ya Ujasusi ya Uturuki, Ibrahim Kalin.
Awali, Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, alikutana na viongozi hao watatu waliotembelea nchi hiyo, akizitaka nchi za eneo hilo kuondoa tofauti zao na kushirikiana katika kukabiliana na vitisho vya pamoja vya kiusalam