Bengalisis
JF-Expert Member
- Jun 8, 2018
- 1,851
- 2,771
*Tough Time In Marriages/ Nyakati Ngumu katika Ndoa*
Moja kati ya changamoto kubwa sana katika nyakati hizi ni Wanandoa kukubali kupita pamoja katika nyakati ngumu.
mwandishi wa Kitabu Cha "Tough Time Never Last,Tough People Do" cha Robert Schuller anaeleza umuhimu wa kupita nyakati ngumu katika maisha yetu. Ukiona watu Couples wanapost wanafuraha naonaga watu wengi sana huwa wanaponda wanasema *"mnajifanya nyie ndo hamna ugomvi"* issue sio kweli ninaamini wanachangamoto kubwa nyingi lakini pengine wametambua namna ya kupambana na hali zao kama sio yao.
Ndoa zinachangamoto nyingi sana lakini hakuna moment ndoa inakuwa "strong" kama mkawa na issue ya ki ndoa mkaikabili hata kama ni mwaka mkapambana halafu mkavuka pamoja ndoa inazidi kuwa imara. Uimara wa ndoa uko katika Kutikiswa tena na dhoruba Kali. Katika kesi kadhaa za ndoa ambazo nimewahi kuzifahamu asilimia kubwa sana ni zile za *"Mimi sijafanya"*.. *"yeye ndo anamakosa"* yaani zinatafuta nani ana haki nani hana nani amekosea na alianza lini.
Kuna nyakati unakuta moto unawaka ndani ya ndoa lakini hakuna anayetoka nje wote mpo ndani unakosa raha unakosa amani lakini upo ndani mnapambana ndani mpaka suluhu ipatikane hii Yote ni gharama ya mapenzi na gharama ya ndoa. Nyakati ngumu huwa haziishi inapaswa kukabiriana nazo...ninatambua Kuna nyakati zinavunja sana moyo kwenye ndoa unatamani kutoka ukapunge upepo kidogo lakini as longer as umedhamiria kuishi na Huyo mtu ni vema ukapita katika moto wa ndoa.
Tambua hata hao unawaona wana furaha wana nyakati ngumu wanapitia lakini wamedhamiria kukabiriana navyo. Kuna nyakati mnakaa ndani mnaliaaa mnalaumiana lakini mmedhamiria kujenga ndoa yenu pamoja. Suala la uimara ni la wote wawili na sio mtu mmoja.
Mkiamua kwa dhati Mtavuka salama ingawa sio rahisi Mara zote. Penye nia pana njia.
Tough Time Never Last, But Tough People Do.