Maisha ya ndoa yamenishinda

Maisha ya ndoa yamenishinda

NIKIMU

Senior Member
Joined
Jan 25, 2015
Posts
182
Reaction score
96
Naishi na mzazi mwenzangu nahisi hana nyota ya mafanikio nifanyeje kila ninachofanya sifanikiwi kabla ya kuwa nae mambo yalikuwa hayakwami.

Naombeni ushauri kwa nyogeza tu alinichanganya baada ya kumfumania na mchepuko mwaka na nusu sasa ananiomba msamaha mpaka leo anajutia na kulia kila wakati nilimsamehe ila nafsi yangu inaumia kila siku namuhurumia ila nateseka mno hasa nikimuona mchepuko wake naombeni ushauri nahisi kukonda
 
Nyie ndio mnaoa ili mke aje kukutoa kwenye umaskini wakati wewe binafsi ndio inatikiwa upambane uitoe familia kwenye umaskini. Kitu kinachoungasha mke na mume inatakiwa iwe ni upendo sio material things.

Achana na mambo ya Nyota ya mafanikio na mauza uza mengine.. mafanikio anatoa aliyekuumba. Acha kumtegemea mkeo kua sababu ya mafanikio..
-sorry
 
Naishi na mzazi mwenzangu nahisi hana nyota ya mafanikio nifanyeje kila ninachofanya sifanikiwi kabla ya kuwa nae mambo yalikuwa hayakwami naombeni ushauri.
Unavyoendelea kuishi kwa kuamini mambo ya nyota hali itaendelea kuwa hivyo hivyo au zaidi., badilika achana na mambo hayo hayana maana yeyote, fanya kazi ujenge familia yako
 
Naishi na mzazi mwenzangu nahisi hana nyota ya mafanikio nifanyeje kila ninachofanya sifanikiwi kabla ya kuwa nae mambo yalikuwa hayakwami naombeni ushauri.
Ushaenda kwa mganga tayari kakudanganya kuwa nyota yako imefifishwaa. Jombaaa komaaa maisha ya ndoa si vitu ila jali utu!!!!
 
Naishi na mzazi mwenzangu nahisi hana nyota ya mafanikio nifanyeje kila ninachofanya sifanikiwi kabla ya kuwa nae mambo yalikuwa hayakwami naombeni ushauri.
Kwanza hauna adabu unaingia katika balaza la wazee wa busara kama sisi bila salamu na umevaa mandala yako.... Hiyo ni kukosa adabu Shuwain.

Pili, haujajitambulisha kuwa wewe ni mtu me au ke?!

Haujatupa ufahamisho juu ya uhalali wa kuishi na huyo ulie nae.... Unazaa na mtu unaenda ishi nae kama mume au mke halali hata haujampitisha katika chujio la maadili na utambuzi.....

Hebu jaribu kuwa presentable basi ndipo uombe ushauri
 
Back
Top Bottom